Monday, May 28, 2012

SHEREHE ZA UBINGWA SIMBA ZAFUNIKA DAR


KLABU ya Simba ililiteka Jiji la Dar es Salaam ambalo lilivaa sura nyekundu kwa muda, jana Jumapili.
Wachezaji na mashabiki wa klabu hiyo walikuwa wakikatiza mitaa mbalimbali ya jiji hilo wakisherehekea ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2011/2012.
Msafara mkubwa wa magari, pikipiki na watembea kwa miguu, ulipita kwa shangwe katika barabara kubwa na mwisho ukaelekea kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala, Zakhem kwa ajili ya kuhitimisha sherehe hizo.
Kazi ilianzia makao makuu ya klabu hiyo, Msimbazi, Kariakoo saa sita mchana, ambako maelfu ya wananchi walifurika wakiwa na magari, pikipiki na wengine wakitembea kwa miguu huku wengi wao wakiwa na flana na bendera za Simba.
Msafara ulitoka Msimbazi kupitia Barabara ya Morogoro kuelekea Ubungo, lakini ulipofika maeneo ya Jangwani, kiungo Uhuru Selemani, alipandwa na ‘mizuka’ na kushuka ndani ya gari kubwa la wazi walilokuwemo wachezaji na kuanza kucheza na mashabiki kabla ya kupanda tena garini.
Wachezaji wa Simba walionekana ni wenye furaha kubwa walipokuwa wakikatiza mitaa mbalimbali na walifungua shampeini kadhaa kuonyesha furaha yao.
Kila msafara ulipopita, mashabiki wengi walikuwa pembeni ya barabara wakipunga mikono na bendera juu kwa furaha kubwa.





Msafara wa magari ukiwa umebeba wapenzi wa Timu ya Simba



Golikipa namba 1 wa Simba na timu ya Taifa Juma Kaseja alishindwa kujizuia katika sherehe hizo pale lilipotajwa jina la marehemu Patrick Mafisango


Wachezaji wakila bata kwenye sherehe hiyo ndani ya Dar Live



No comments:

Post a Comment