Friday, June 15, 2012

EURO 2012 SPAIN YAISUKUMA IRELAND NJE YA MICHUANO YAICHAKAZA 4-0



Torres (juu)akiachia  nduki iliyojaa moja kwa moja wavuni na kuvungua ukurasa wa mabao (chini) akishangilia.

Fernando Torres alifanikiwa kutupia kambani magoli mawili katika mechi ambayo Uhispania kwa urahisi ilifanikiwa kuilazimisha Jamhuri ya Ireland kukusanya virago na kuondoka katika mashindano ya Euro 2012.

Mkwaju wa Torres uliopigwa kwa kasi ya kutakata kutoka yadi kumi ulianzisha mfululizo wa magoli, mara tu baada ya bao hilo la kwanza kuingia wavuni katika dakika ya nne ya mchezo.

Mara tu baada ya kipindi cha pili, David Silva aliongezea bao la pili katika dakika ya 49.

Torres alifanikiwa kutupia bao lake la pili katika mechi hiyo katika dakika ya 70, huku mchezaji wa akiba Cesc Fabregas naye alitupia kambani bao la nne kwa nduki kali iliyokaribia kuchana nyavu za goli katika ya 83. Shukrani za pekee zimuendee mlinda mlango wa Ireland Shay Given kwa kuokoa michomo mingi ya Wahispania na hivyo kupunguza kapu la magoli.

Matokeo hayo yameiwezesha Uhispania kuipita Croatia na kuongoza kundi C.
Uhispania sasa itakutana na Croatia siku ya Jumatatu, mechi ambayo inatazamiwa kuwa ngumu.



Fabregas (juu)akitupia kambani goli la nne kwa shuti kali (chini) akishangilia.

Mchezo wa Jamhuri ya Ireland bila shaka ulikuwa na dosari nyingi, na katika mashindano yao makubwa baada ya kipindi cha miaka kumi, wamefungwa magoli mengi kirahisi.

Katika kila mechi waliocheza ya Euro 2012, katika kila nusu ya mchezo ilipoanza, walifungwa bao chini ya dakika nne za mwanzo, hii ikiwa ni pamoja na katika mechi walioshindwa na Croatia magoli 3-1.


Mashabiki wa Ireland ambao kwa kiasi kikubwa walionesha uzalendo kwa kushangilia mwanzo mwisho bila kujali kichapo walichokishuhudia kutoka kwa Uhispania..WaTanzania tuigeni uzalendo huu pindi timu zetu zinapocheza

Kabla ya mechi hiyo, Jamhuri ya Ireland ilikuwa haijawahi kupokea kichapo cha zaidi ya magoli matatu katika mashindano makubwa.
Lakini hayo sasa yametokea, wakifungwa magoli mengi mara mbili katika kipindi cha siku tano.


Fundi XAVI akifanya mamboz katika mtanange huo

Dogo hapa huendi kokote!!... Silva akidhibitiwa na walinzi wa Ireland

Kwa Uhispania ambayo ilitoka sare ya 1-1 iipocheza na Italia katika mechi yao ya kwanza, hili ni onyo muhimu kwa wapinzani, kuonyesha kwamba nchi hiyo ina nia ya kuandikisha historia kwa kuwa mabingwa katika mashindano makubwa.

Ujumbe umewasilishwa kikamilifu chini ya saa 24 tangu Ujerumani nayo ilipoonyesha uhodari wake kwa kuilaza Uholanzi magoli 2-1.
SPAIN  4-0  REPUBLIC OF IRELAND

No comments:

Post a Comment