Menez akishangilia baada ya kutupia goli la kwanza
Ufaransa ilipata ushindi wake wa kwanza katika kundi D katika mechi ya Ijumaa ya Euro 2012, baada ya kuwashinda wenyeji Ukraine katika uwanja ulioloa maji kufuatia mvua kubwa iliyotandika katika uwanja wa Donetsk.
Wingu limetanda
Mchezo ulisitishwa baada ya dakika nne tu, kufuatia uwanja kujaa maji, na timu zilirudi uwanjani baada ya saa nzima kupita.
Lakini waliporudi, kulikuwa hakuna njia nyingine ya kuiokoa Ukraine, kuanzia wakati Jeremy Menez, mchezaji wa St Germain ya Ufaransa, alipowaongoza Wafaransa katika kufunga mabao, akitupia mpira kambani kutoka yadi 12.
Yohan Cabaye alitupia kambani bao la pili na hilo lilikuwa ni bao la kwanza katika mechi ya kimataifa kwa mchezaji huyo wa klabu ya Newcastle inayocheza katika ligi kuu ya England.
Bao hilo lilipatikana kwa urahisi kufuatia kosa la wachezaji wa ulinzi wa Ukraine namna walivyocheza katika uwanja huo wa Donbass Arena.
Wachezaji wa timu zote walikuwa na kibarua kigumu katika kucheza katika hali ya joto kali na uwanja ulioloa, na ndio maana mwamuzi Bjorn Kuipers kutoka Uholanzi awali alikuwa ameamua kusitisha mechi hiyo.
Ilibidi juhudi za dharura kufanyika ili kuyafyonza maji hayo, na baadaye mwamuzi kuidhinisha mechi kuendelea.
Mvua imeanza kutandika goma linaendelea Nasri akimchachafya mlinzi wa Ukraine
Mvua inaendelea kutandika na mashabiki wabishi wamo
Hatoki mtu uwanjani mpaka kieleweke mtanange unaendelea
Oyoooo mpaka kielewekeeeee!!!
Radi inatandika kisawasawa
Asiekubali kushindwa si mshindani..hatimae mwamuzi alisimamisha mtanange baada ya mvua kuendelea kushuka na maji yakijaa dimbani
Isiwe taabu ngoja tukaisikilizie nje, mwamuzi na wachezaji wakitoka uwanjani kufuatia mvua kubwa kunyesha
Tukausheni maji jamani leo hapa hatoki mtu, wafanyakazi wa uwanja wakikausha maji baada ya mvua kukatika
Kocha wa Ukraine akitest je maji kweli yamekauka au!!?
Ukraine 0-2 Ufaransa
No comments:
Post a Comment