We kipara unaenda wapi? Mshambuliaji wa Denmark akichanja mbuga
Lars Bender alifunga bao la ushindi la Ujerumani siku ya Jumapili zikiwa zimesalia dakika 10 kabla ya kipenga cha mwisho, na kuiwezesha nchi yake kuwa miongoni mwa nchi nane ambazo zitashiriki katika michuano ya robo fainali.
Lars Bender akishangilia waya huku mlinda mlango wa Denmark akitambaa
Mechi nyingine ya kundi hilo la B ambayo ilichezwa wakati mmoja, kati ya Ureno na Uholanzi, Ureno walifuzu kwa ushindi kama huo wa magoli 2-1.
Bender, mwenye umri wa miaka 23, na ambaye ni mchezaji wa Bayer Leverkusen ya Ujerumani, aliizima ndoto ya Denmark ya mwaka 1992, walipowashinda Wajerumani katika fainali.
Mashabiki wa Ujerumani wakiwa wanakula bata huku wanafuatilia soka
Mashabiki wa Ujerumani wakishangilia baada ya chama lao kutinga robo fainali za EURO 2012
Ujerumani iliweza kuongoza katika mechi hiyo dakika ya 19 wakati Lukas Podolski alipofunga, lakini Michael Krohn-Dehli aliweza kuisawazishia Denmark dakika sita baadaye na kuipatia nchi yake matumaini ya kufika robo fainali.
Wachezaji wa Ujerumani hawakupendezwa na safari kutoka kituo chao cha nyumbani cha Gdansk, Poland, hadi Ukraine, lakini kutokana na ushindi wa Lviv, wameweza kufuzu kuingia robo fainali na watafurahia kuicheza mji ambao wameezeka kambi yao.
Kabla ya mechi ya Jumapili, mara ya mwisho Denmark ilipopambana na Ujerumani katika mashindano makubwa, ilikuwa ni fainali ya 1992, wakati Yugoslavia ilipopigwa marufuku kucheza, na hatimaye Denmark iliwashangaza wengi ilipoishinda Ujerumani katika fainali.
Timu ya Ujerumani ya mwaka huu ndio timu yenye vijana wenye umri mdogo zaidi katika mashindano ya mwaka huu, kwa jumla wachezaji wengi wakiwa na umri wa miaka 25 na siku 107.
Hii ni mara ya kwanza kwa Ujerumani kukamilisha mechi za makundi kwa rekodi safi mno ya asilimia 100.
GERMANY Vs DENMARK
No comments:
Post a Comment