Kocha wa Arsenal Arsene Wenger akizungumza na waandishi wa habari baada ya mechi.
Arsenal imepata ushindi wake wa kwanza katika ligi ya Premier ya nchini Uingereza msimu huu baada ya kuidungua Liverpool 2-0 nyumbani kwao.
Hii ndio mara ya kwanza kabisa kwa Liverpool kuanza msimu kwa kichapo cha mabao 2-0 katika uwanja wao katika kipindi cha miaka 50,Magoli yote mawili ya Arsenal yalitupia kambani na wachezaji wapya Santi Cazorla na Lukas Podolski .
Mshambuliaji wa Ujerumani Podolski ndiye alikuwa wa kwanza kuipatia Arsenal bao katika dakika ya 31. Na katika dakika ya 68 Cazorla alipeleka kilio na kubadili ubao wa matangazo kuwa 2-0.
Podolski akitupia goli la kwanza
Podolsi akishangilia goli
Magoli hayo pia ndio yalikuwa ya kwanza kwa Arsenal tangu msimu huu uanze kwani katika mechi zao mbili za awali walitoka sare ya 0-0 na wapinzani wao.
Kufuatia ushindi huo Kocha wa Arsenal alisema kuwa uimara wa vijana wake unaongezeka katika kila mechi na kuwa amefurahishwa na matokeo ya timu yake.
Baada ya kucheza mechi tatu, Liverpool ambayo iko nchini ya mkufunzi mpya Brendan Rodgers ina pointi moja peke yake.
Hii inaweza kufananishwa na matokeo mabaya ya timu hiyo katika msimu wa mwaka 1962-63 chini ya Bill Shankly.
Katika mechi hii washambulizi Luis Suarez na Fabio Borini hawakuwa na kubwa uwanjani.
Nae mchezaji mpya wa kiungo Nuri Sahin wa Liverpool pia hakuonyesha makeke yake uwanjani.
Santiago Carzola akishangilia baada ya kutupia goli la pili
Golikipa wa Arsenal Manone akishangilia ushindi
Patashika Steven Gerrard na Abou Diaby
Liverpool 0-2 Arsenal
No comments:
Post a Comment