Tuesday, September 18, 2012
DARAJA LA KIGAMBONI KAZI IMEANZA
Ujenzi wa Daraja la Kigamboni ukiendelea, na pichani ni daraja la muda
Ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam, umeanza kwa kishindo na jana Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli alitembelea eneo hilo na kuwahimiza makandarasi kukamilisha kazi hiyo kwa muda uliopangwa.
Daraja hilo linalojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), linatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu huku likigharimu Sh214 bilioni.
Ujenzi wa daraja hilo unafanywa na Kampuni ya China Railways Construction na China Major Bridge Engineering Company, zote za nchini China.
Akizungumza na makandarasi hao, Waziri Magufuli aliwataka waongeze kasi ya ujenzi na kuahidi kwamba Serikali itatoa ushirikiano wa hali na mali ili kukamilisha kazi hiyo.
"Nataka niwahakikishie kwamba Serikali itaendelea kuwa bega kwa bega nanyi. Lakini najua nyie ni wachapa kazi, mnaweza kufanya kazi usiku na mchana na kufanya ujenzi uchukue miezi 30 badala ya 36 ya sasa," alisema Dk Magufuli.
Wajomba kazini
Waziri wa Ujenzi Dkt John Magufuli sambamba na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam wakiangalia vifaa vya kampuni inayotengeneza daraja linalounganisha Kigamboni na Kurasini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment