Thursday, December 6, 2012

MAKALA YA KUUKARIBISHA MWAKA 2013


Zikiwa zimesalia siku 25 kumaliza mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013 hatuna budi kumshukuru mwenyezi mungu muumba wa mbingu na ardhi na kila kitu kilichomo ndani yake kwa kutuwezesha kufikia mpaka hapa tulipo leo hii na tumuombe atujaalie kuuona mwaka mpya wa 2013.

Tutumie wakati huu ambao bado tuna baraka zake kwa kutuwezesha kupumua mpaka hivi sasa katika maombi, yatupasa kumuabudu kila mtu kwa wakati wake na kwa dini yake pasipo kumkwaza mtu mwingine. Tutumie muda huu kuomba msamaha kwa wale wote ambao kwa namna moja au nyingine umewakosea na vivyo hivyo usipokee tu msamaha nawe pia uwasamehe wote waliokukosea kwa namna moja au nyingine na hata kama hawajakusamehe kwa yale uliowakosea.

Ni muda mzuri wa kuwa karibu na familia na kujadili masuala yanayohusu familia yako na jamii inayokuzunguka, Kutafakari nini kimefanyika katika mwaka huu 2012 ambao kwa unyenyekevu tuna uaga na kuukaribisha mwaka mpya wa 2013 na nini kitafanyika katika mwaka mpya 2013.

Mimi binafsi napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kuniwezesha kuwa hai mpaka dakika hii ninayoitumia kuandika makala hii,Kumshukuru kwa kuniwezesha kutimiza malengo fulanifulani katika mwaka wa 2012 na kunipa uwezo wa kuwa na mipango mipya kwa mwaka ujao wa 2013 na ninamuomba anisimamie na kuniongoza kufanikisha mipango yangu  ya siku za usoni.

Napenda nitumie fursa hii nikiwa kama binadamu wa kawaida ninaamini kuwa katika maisha yangu ya kila siku ninafanya mema na pia ninayo mabaya ninayoyafanya aidha kwa kujua au kutokujua na kuna watu wanaokwazika na mabaya hayo,nina imani kama nimekukosea aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya ni kwasababu mimi ni binadamu na sio mkamilifu na kwa kulitambua hilo ninaomba MSAMAHA kwa wale wote niliowakosea mpaka kufikia leo hii tukijiandaa na kuupokea mwaka mpya wa 2013. Kwa moyo mkunjufu bila kumung'unya maneno wala bila kupepesa macho na bila kukunjakunja vidole ninasema kwamba wale wote walionikosea NIMEWASAMEHE.

SISI sote hapa duniani ni ndugu na binaadamu wote tuko sawa tofauti yetu ni katika rangi ya ngozi,dini,Utaifa,Makabila,Maumbo na haiba. Hapa duniani tunapita safari yetu ni moja na njia ya kufanikisha safari hiyo ni KIFO. Hatuna budi kupendana,kuthaminiana na kusaidiana katika nyakati zote za shida na raha.

Kama mtanzania ninawaomba watanzania wote tutumie fursa hii pia kuiombea nchi yetu iweze kuwa katika UTULIVU tulio nao nasi kwa pamoja tudumishe AMANI na UPENDO tulionao. Akhsante kwa muda wako ulioutumia kusoma makala hii Mungu akubariki sana na akulinde na mabaya, akutangulie uweze kufika 2013.

Khalid Japhary Gomeka,
jiffjeff@yahoo.com
www.facebook.com/KhaledDeGomeka
www.twitter.com/KhaledDeGomeka
+255 712 18 45 98
+255 688 29 27 27

No comments:

Post a Comment