Katika mtanange huo mkali na wa kusisimua uliopigwa katika dimba la Stamford Bridge huku ukishuhudiwa na mashabiki wapatao 40,172, ulishuhudia Swansea ikiongoza mashambulizi na washambuliaji hatari Michu na Graham na kuiadhibu vikali Chelsea.
Iliwachukua takribani dakika 38 tu mashabiki wa Chelsea kuanza kuviona viti vichungu pale mfumania nyavu hodari MPC Michu alipotupia kambani goli la kwanza na la kuongoza kwa upande wa Swansea.
Mpambano uliongezeka kasi na kutiwa chachu na Vijana wa darajani kutaka kuchomoa bao huku wageni Swansea wakitia ngumu na wakitaka kuongeza bao ili kujihakikishia ushindi, hamad mungu sio Abramovic wala sio Benitez Mashabiki wa Swansea walilazimika kuachia viti na kuruka hewani kwa furaha na kuamsha makelele pale Mshambuliaji hatari na mwenye akili nyingi D Graham kutikisa nyavu katika dakika ya 90 na kuandika bao la pili kwa Swansea.
Hawa watu Michu na Grahamu hata ukiwauliza mashabiki wa Arsenal watakuambia ni watu gani, hivyo mpaka mwisho wa mpambano Mashabiki wa Chelsea walinyanyuka na kupangusa matako yao na kuondoka vichwa chini huku wale wa Swansea wakitamani kukesha uwanjani kusherehekea ushindi wa 2-0 katika dimba la Stamford Bridge.
Michu akishangilia goli la kwanza
Ivanovic akimdhibiti mchezaji wa Swansea
Graham akimtoka mlinda mlango wa Chelsea
Asipigeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!! Graham akiwapa shida mabeki wa Chelsea.
Ishakuwa sooo!! Ndivyo Fernando Torres anavyowaza baada ya kichapo
Chelsea 0-2 Swansea
No comments:
Post a Comment