Burkina Faso, imetinga fainali baada ya kuilaza Ghana kwa njia
ya mikwaju ya penalti baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 katika dakika 120 za
mchezo, ukiwa ni mchezo wa pili wa nusu fainali za kombe la mataifa ya
Afrika.
Katika kipindi cha kwanza Ghana mnamo dk 12 walijipatia bao kwa mkwaju wa penati iliyopigwa na Wakasso. Bao hilo lilidumu mpaka mapumziko Ghana wakiwa kifua mbele,Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikitafuta bao na dk 59 bundi aliangukia katika lango la Ghana na mshambuliaji hatari A.Bance aliipatia Burkina Faso bao la kusawazisha na matokeo kuwa 1-1 katika dimba la Mbombela mchezo ukihudhuriwa na mashabiki 35,000.
Ghana ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa kucheza fainali, walishindwa kutamba mbele ya vijana wa Burkina Faso na kulazimika mikwaju ya penalti inatumika.
Ghana walipata penalti mbili tu, huku mbili zikipigwa nje na moja ikipanguliwa na mlinda mlango wa Burkina Faso.
Sasa Ghana itachuana na Mali kumtafuta mshindi wa tatu siku ya Jumamosi.
Jumapili, ndiyo siku yenyewe ya kujulikana bingwa. Je, ni Nigeria au Burkina Faso? Dakika 90 zitatoa jibu la kitendawili hicho.
A.Bance mfungaji wa goli la Burkinabe
Wakasso akiipatia goli Ghana kwa mkwaju wa penati mapema kabisa ya mchezo.
Mlinda mlango wa Burkinabe akiokoa hatari langoni mwake
Wachezaji wa Burkina Faso wakishangilia kutinga fainali baada ya mlinda mlango wao kupangua penati ya mwisho.
Mlinda mlango wa Burkina Faso
Asamoah Gyan Chini ya Ulinzi
Burkina Faso Vs Ghana penalty kickouts
No comments:
Post a Comment