PAPA AFUNGUKA INTERNET NI ZAWADI KUTOKA KWA MUNGU
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis
amesema kuwa Internet ni zawadi kwa dunia nzima kutoka kwa Mungu lakini
akaonya kuwa matamanio ya kutaka kuwasiliana zaidi kutumia Internet
kunawatenga watu kutoka kwa familia na marafiki zao.
Amewataka waumini wa kikatoliki kujiunga na
mfumo wa dijitali. "Internet... inatoa nafasi ya mafanikio mengi. Hiki
ni kitu kizuri bila shaka ni zawadi kutoka kwa Mungu,'' alisema Papa.
Katika ujumbe wake kwa dunia nzima ambao hutolewa kila mwaka, Papa
amesema kuwa mfumo wa dijitali, unapaswa kuwa mtandao wa watu wala sio
nyaya tupu.
Papa mwenyewe ana akaunti kwenye Twitter ambayo ina wafuasi zaidi ya milioni kumi.
Amehimiza kuwa mawasiliano yanapaswa kuhusisha hisia na mawazo, watu kukutana na kujuliana hali.
Kadhalika amewataka waumini wa kikatoliki
kutodhani kuwa ni mawazo yao na imani zao pekee ambazo ni muhimu wakati
wakiwasiliana na watu wa dini nyinginezo.
No comments:
Post a Comment