Wednesday, May 25, 2011
MAN UNITED WAMSAJILI KIPA WA ATLETICO.
Kocha wa Man united ya Uingereza Sir Alex Furgeson amefunguka na kusema kuwa tayari klabu yake imeshanyaka saini ya golikipa wa Atletico Madrid ya Hispania David De Gea, De Gea anaaminika kuwa ndiye golikipa kinda ghali zaidi duniani. Mashetani hao wekundu wamemnyakua golikipa huyo kwa kitita cha paundi za uingereza milioni 17 vyanzo vya habari vimeeleza.
WENGER AFUNGUKA KWA NASRI NA CLICHY.
Wenger awachimba mkwara Nasri, Clichy
- Jumatano, Mei, 25, 2011, 9:15
LONDON, Uingereza.
Meneja wa Arsenal mfaransa ARSENE Wenger amewakoromea nyota wake wanaogomea kusaini mikataba mipya, Samir Nasri na Gael Clichy kwamba hatokuwa na masihara katika hilo.
Nyota hao wamebakiza mwaka mmoja katika mikataba yao na kocha huyo wa Arsenal, Wenger anataka waamue mapema kuhusu kuongeza mikataba yao au waingizwe sokoni mwishoni mwa msimu huu.
“Tutamaliza tatizo hilo kwa haraka baada ya kumalizika kwa msimu,” alisema Wenger.
“Tunahitaji kufahamu mapema msimamo wao.”
Arsenal ilimpoteza kiungo Mathieu Flamini katika uhamisho huru mwaka 2008 baada ya kushindwa kuafikiana na nyota huyo wa Ufaransa.
Jambo hilo linamtisha Wenger na anadhani hali inaweza kujirudia.
Alisema: “Hatutaki yatokee kama yale yaliyokuwa kwa Flamini. Haturuhusu hilo kabisa. Tunataka kumaliza utata kabla ya msimu mpya kuanza.”
Meneja wa Arsenal mfaransa ARSENE Wenger amewakoromea nyota wake wanaogomea kusaini mikataba mipya, Samir Nasri na Gael Clichy kwamba hatokuwa na masihara katika hilo.
Nyota hao wamebakiza mwaka mmoja katika mikataba yao na kocha huyo wa Arsenal, Wenger anataka waamue mapema kuhusu kuongeza mikataba yao au waingizwe sokoni mwishoni mwa msimu huu.
“Tutamaliza tatizo hilo kwa haraka baada ya kumalizika kwa msimu,” alisema Wenger.
“Tunahitaji kufahamu mapema msimamo wao.”
Arsenal ilimpoteza kiungo Mathieu Flamini katika uhamisho huru mwaka 2008 baada ya kushindwa kuafikiana na nyota huyo wa Ufaransa.
Jambo hilo linamtisha Wenger na anadhani hali inaweza kujirudia.
Alisema: “Hatutaki yatokee kama yale yaliyokuwa kwa Flamini. Haturuhusu hilo kabisa. Tunataka kumaliza utata kabla ya msimu mpya kuanza.”
PIQUE AKUMBUKA MACHOZI MAN UNITED.
Pique akumbuka alivyomwaga chozi Man United
- Jumatano, Mei, 23, 2011, 9:10
BEKI wa Barcelona, Gerard Pique, akumbushia enzi zile alipokuwa Man United na kufunguka kwamba aliwahi kumwaga machozi wakati alipokuwa akikipiga Manchester United – lakini, Jumamosi hii Mhispania huyo atakutana na United katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, itakayofanyika kwenye dimba la Wembley, jijini London.
Gerlard PiqueAkiwa ndani ya jezi za Mashetani Wekundu hao wa Old Trafford, Pique anashukuru kwa sababu aliweza kutwaa mataji tisa na Kombe la Dunia.
Man United imebaki kuwa sehemu muhimu katika maisha yake ya soka, licha ya kwamba hakucheza mechi nyingi katika kikosi hicho cha Sir Alex Ferguson, na kudai kwamba yeye binafsi ana deni kubwa la kumshukuru Mskochi huyo.
“Nilikwenda England nikiwa na miaka 17 na mambo yalikuwa magumu sana,” alisema Pique.
“Nilizoea kuwa kiwanjani katika kila mechi, lakini kwa bahati mbaya siku nyingine za mechi mimi nilikuwa nikiachwa nyumbani.
“Iliniumiza sana, na niliona sikustahili yale. Lakini, wakati ule sikuwa sawa na nilipokuwa Manchester United.
“Nilijifunza jinsi ya kukabiliana na nyakati ngumu. Nilimpigia simu mama yangu mzazi na kumweleza yote baada ya kutokwa na machozi sana.”
Pique Jumamosi hii atakuwamo ndani ya dimba wakati Barca itakapokipiga na Man United katika fainali hiyo ya Mabingwa Ulaya katika dimba la Wimbley nchini Uingereza.
Tuesday, May 24, 2011
AMINI USIAMINI
Hapa duniani kuna viumbe wengi sana ambapo kila kiumbe kina tabia zake tofauti na viumbe wengine, ikiwa ni pamoja na uwezo wao wa kukabiliana na mazingira kulingana na hali ya hewa ya eneo husika pia viumbe hutofautiana katika uwezo wa kupambana na hali na katika kujitafutia ridhiki yaani hali ya kujiwezesha kuishi na hali kujiwezesha kuwa hai katika eneo husika.
Leo nitoe mfano Paka anaishi katika mazingira ambayo binaadamu anaishi lakini katika kuishi huko Paka amekuwa akiwadhuru baadhi ya viumbe ambavyo binaadamu anafuga kwa faida moja au zaidi.
Leo nitoe mfano Paka anaishi katika mazingira ambayo binaadamu anaishi lakini katika kuishi huko Paka amekuwa akiwadhuru baadhi ya viumbe ambavyo binaadamu anafuga kwa faida moja au zaidi.
| Kipa Mkenya asaini Simba miaka 2 | Send to a friend |
| Sunday, 22 May 2011 20:37 |
BAADA ya mazungumzo ya kina na uongozi wa klabu ya Simba, hatimaye kipa wa kimataifa wa Kenya, Willis Ochieng amesaini rasmi mkataba wa miaka miwili wa kuichezea timu hiyo.Ochieng ambaye awali alikuwa anacheza soka ya kulipwa katika klabu ya IFK Mariehamn ya Finland kabla ya kumalizika mkataba wake Novemba mwaka, jana alitua nchini Alhamisi ya wiki iliyopita kwa ajili ya kukamilisha taratibu za usajili ili aweze kuichezea Simba katika msimu ujao wa ligi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Akizungumza na Mwananchi jana akiwa njiani kurudi nchini Kenya, Ochieng alisema kuwa mpango wake wa kujiunga na Simba umekamilika na tayari amesaini mkataba wa miaka miwili."Nashukuru kilichonileta nimekamilisha, nimezungumza vizuri na watu wa Simba na nimesaini kucheza katika klabu yao kwa mkataba wa miaka miwili,"alisema Ochieng. Alisema,"Kimsingi nilipenda kucheza hapa kwa sababu mazingira ya kufanya kazi Kenya na Tanzania yanafanana na hata urafiki wa watu wake ni wa karibu sana hivyo ni dhahiri ninaweza kufanya vizuri na kuisaidia Simba kufikia malengo yake." Ochieng alisema anaelekea nyumbani kwao Kenya kwa ajili ya kuwaaga ndugu na jamaa na kwamba atarejea nchini baada ya wiki moja kujiunga rasmi na wenzake. "Nilikuja kwa ajili ya kuweka mambo sawa na hilo limemalizika, naelekea nyumbani kuaga ndugu na jamaa na nitarejea baada ya wiki moja kuanza kazi rasmi,"alisema Ochieng. Kipa huyo ameshazichezea klabu za Mumias Sugar ya nchini Kenya pamoja na Free State ya Afrika Kusini, alisema kuwa atalazimika kufanya juhudi zaidi ili aweze kupata nafasi ya kuwa kipa namba moja. "Mimi sijafanya mazungumzo ya kuja kuwa kipa namba moja hilo litatokana na juhudi nitalazimika kuzifanya na si rahisi kama watu wanavyoongeza, Simba ina makipa wazuri kama Juma Kaseja ni mmoja wao hivyo ni dhahiri ushindani utakuwepo,"alisema Ochieng.Wakati huo huo; Jessca Nangawe anaripoti kuwa mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi anatua leo akitokea nchini kwake Afrika Kusini alipokuwa akifanya majiribio na klabu ya Kaizer Chief |
TANZANIA KUJITANGAZA LIGI ZA ULAYA.
| Sh5bil kuitangaza Tanzania Ligi za Ulaya | Send to a friend |
| Monday, 23 May 2011 20:51 |
Rais wa Tanzania, Mh Jakaya Mrisho Kikwete. SERIKALI imejipanga kuitangaza sekta ya utalii hapa nchini kwa kupitia michezo na kwa sasa imeweka mkakati wa kutoa matangazo ya utalii katika viwanja vinane vya soka ulimwenguni vinavyotumiwa na timu za ligi kubwa duniani. Jumla ya sh5billioni zitatumika kwa zoezi hilo kuitangaza Tanzania katika ligi za England, EPL, Hispania, La Liga, Italia, Seria A, Ufaransa, Lique 1 na Ujerumani ya Bundesliga.Mbali na viwanja hivyo pia nafasi hiyo itatumika kutangana za Tanzania na utalii katika nchi za Ureno, Uholanzi pamoja na Uturuki. |
Subscribe to:
Posts (Atom)



