Thursday, June 16, 2011

BAMBO APATA AJALI YA PIKIPIKI AVUNJIKA MGUU.

Wasanii wakimuangalia Bambo kitandani kwa huzuni.

Dereva wa pikipiki iliyokodiwa na Bambo akiwa hoi hospitalini.

Msanii maarufu wa maigizo Dickson Makwaya a.k.a BAMBO leo alfajiri maeneo ya Kigogo amepata ajali mbaya ya pikipiki, baada ya pikipiki aliyokuwa ameikodisha kugongwa na daladala aina ya DCM na kusababisha Bambo kuvunjika mguu wa kulia sehemu ya paja huku ajali hiyo ikimuacha dereva wa pikipiki hiyo akiwa katika hali mbaya, wote wamelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu. 

Wednesday, June 15, 2011

UANGALIAJI WA TV HUUMIZA AFYA YAKO.

Wale wanaopenda kukaa na kuangalia Luninga(TV) muda wote ambao kwa kitaalamu tunawaita "Couch Potatoes" mpo katika hatari ya kupata madhara katika afya zenu kwa kutazama luninga kwa masaa mawili au zaidi ambapo utafiti umeonesha kuna hatari ya kupata Type 2 diabetes,Cardiovascular disease na vifo vya mapema kutokana na hayo madhara na inaripotiwa na jarida ya chama cha madawa cha Marekani (J.A.M.A).
Uangaliaji wa luninga unahusishwa na kutokuwa na mpangilio mzuri katika ulaji wa chakula, kuongezeka kwa uzito, athari za kisukari,magonjwa ya moyo na maisha mafupi. Utafiti umeonesha pia kutolala kwa usahihi pia kunasababishwa na uangaliaji wa luninga ambapo kwa kawaida mtu anatakiwa alale masaa saba mpaka nane. Kwa haya yote hatupaswi kulaumu luninga kwani sisi ndio tunaoiwasha na kushika remote na kukaa masaa yote kwenye kochi.Angalia tabia ya kuangalia luninga inavyoweza kuhatarisha afya yako:
1} TYPE 2 DIABETES; zaidi ya wamarekani milioni 26 wana kisukari kwa hili wana hatari kubwa ya kupata magonjwa ya moyo na kiharusi.Type 2 diabetes husababishwa na uzito kupita kiasi,maisha ya sedentary (sedentary lifestyle),mlo usiokamili, Ili kuepukana na hili punguza uzito na fanya mazoezi kwani kunasaidia insulin kufanya kazi ambayo ndio sababu kubwa ya kisukari.

2} CARDIOVASCULAR DISEASE (CVD). Hii inahusisha ugonjwa wa moyo,mapigo ya moyo kwenda mbio(high blood pressure),maumivu ya kifua,kiharusi na moyo kushindwa kufanya kazi. utafiti unaonesha madhara haya huwapata wanaoangalia TV kwa masaa 2 kwa siku, mwanga wa TV unaowaingia watoto unapunguza njia machoni mwao na siku za usoni wanaweza kupatwa na CVD.
Njia ya kujikinga ni kufanya mazoezi kwa nusu saa kwa siku tano au zaidi kwa wiki, kupima blood pressure na cholestrol mara kwa mara.

3}ALL CAUSE MORTALITY. Utafiti wa (J.A.M.A) umeonesha uangaliaji wa TV kwa masaa zaidi ya matatu kwa siku kunapelekea kuwa na mazoea na TV yaani "couch potato" Njia ya kuepuka hili ni ni kama zile za kujikinga na kisukari na CVD.

4}SLEEP DEPRIVATION. Kiafya tunahitaji masaa 7-8 ya kulala kila siku lakini watu wengi hawayapati ipasavyo, utafiti unaonesha uangaliaji wa TV karibu na kitanda ni wa kulaumu. Utafiti umeonesha kuwa mwanga wakati wa usiku ikiwamo wa TV una hatari ya kusababisha kansa ya maziwa kwa wanawake.
Njia ya kuepuka hili,zima TV kwa saa moja kabla ya kwenda kulala kwasababu mwanga wa  TV unaupa ubongo uwezo wa kufanya kazi na hivyo kukufanya iwe ngumu kupata usingizi kwa haraka.

5} NEARSIGHTEDNESS IN KIDS. Hii imeathiri watu zaidi ya bilioni 1.6 duniani kote,idadi ni kubwa zaidi katika nchi ambazo watoto wanaangalia TV na kucheza Computer game badala ya kucheza viwanjani yaani nje.Tokyo na Hongkong 30%-50% ya watoto ni myopic(nearsightedness) na 20% U.S.A. Utafiti wa mwaka 2009 umeonesha watoto wenye athari hii ni wale wanaotumia muda wa saa 4-5 kwa wiki katika TV.
Njia ya kujikinga, utumiaji wa saa 2 kwa siku nje hupunguza tatizo hili kwa watoto na tuwashauri kuangalia vitu vilivyo mbali ili kuimarisha uwezo wa macho kuona. michezo ya nje pia huimarisha uzito wa mtoto kulingana na afya yake. 
kwa maswali jiffjeff@yahoo.com    +255712184598

Tuesday, June 14, 2011

PICHA YA LEO

Upendo ni kitu muhimu sana katika maisha ya kiumbe chochote chini ya jua.

TOFAUTI YA PROFILE ZA WASICHANA/WANAWAKE NA WAVULANA/WANAUME KATIKA FACEBOOK

Mtandao wa kijamii wa Facebook maarufu kama FB umezidi kuchukua umaarufu siku hadi siku na katika hilo naweza kusema mtandao huu wa kijamii umeteka Dunia.
Katika mtandao huu watu hupata marafiki aidha kwa kujuana au kwa kujuana ki facebook facebook tu na kuombana urafiki kisha wanaendelea na mawasiliano. Kuna kitu kinaitwa Profile hapa ni pale ambapo habari binafsi za mwanachama hupatikana kama vile yeye ni nani,yupo wapi na anafanya shughuli gani vilevile unapata kuona picha zake ambazo amezihifadhi yeye.
Katika hizi PROFILE nimegundua kuwa za wasichana au wanawake zipo tofauti sana na za wale wa jinsia ya pili yaani wanaume, Tofauti hiyo ni hii;
Mwanamke akiandika kitu katika sehemu ya status kwa mfano; Najisikia vibaya......
Mwanaume nae aandike mfano; nimepata ajali nimeumia sana......
Sasa basi status ya mwanamke ina dakika moja tu tangu aandike, na mwanaume ina siku nne tokea aiandike lakini matokeo yatasomeka hivi;
Katika muda huo mfupi mwanamke atakuwa na likes 60, mwanaume atapata likes 1.
watakao comment kwa mwanamke watafikia 104 wakati mwanaume atapata comment 3.
Ukisoma walicho-comment kwa mwanamke kitasomeka hivi, Imekuwaje?
Sasa ninajiuliza mwanamke kaandika tu..najisikia vibaya lakini mwanaume kaandika kitu serious kwamba amepata ajali lakini duh..kila mtu anahitaji kuwasiliana na mwanamke,haya ndio yanayotokea katika mitandao mingi ya kijamii hasa FACEBOOK.

HAKUNA MBINU MBADALA KUKABILIANA NA GHASIA ZAIDI YA KUTUMIA SILAHA ZA MOTO?

Maandamano na migomo ni haki za msingi kwa mwananchi yeyote yule ili mradi maandamano hayo au mgomo huo ufuate kanuni na taratibu na vyote hivyo vifanyike pasipo kukiuka au kuvunja sheria na kanuni za nchi. Sasa basi bila kujali kuwa maandamano au mgomo umefuata taratibu au la, nijuavyo mimi maandamano au migomo huwa ni katika kutafuta haki ambayo kwa namna moja au nyingine imenyimwa au imenyang'anywa iwe kwa bahati mbaya au kwa makusudi na ili ipatikane lazima kuwe na shinikizo la amani yaani maandamano au mgomo.
Hali imekuwa mbaya sana pindi migomo au maandamano yanapotokea iwe kwa kufuata taratibu au kwa kutifuata taratibu,waandamanaji huwa hawana nia ya kudhuru zaidi ya kutaka kusikilizwa, lakini cha kushangaza jeshi letu la polisi limeonesha udhaifu kwani mara kwa mara hupenda kutumia silaha za moto katika kukabiliana na waandamanaji kitu ambacho si sahihi kwasababu waandamanaji huwa hawana silaha sasa iweje polisi watumie silaha kukabiliana nao? Hili linanipa wasiwasi kwamba jeshi letu la polisi limekosa ubunifu na halina ujuzi wowote wa kukabiliana na waandamanaji na wanaona suluhisho ni kurusha silaha za moto ambazop matokeo yake zimekuwa zikiua na kujeruhi wananchi ambao kwa namna moja au nyingine huwa hawana makosa.
Wakati mwingine huwa inanipa hisia mbaya na kufikiria kuwa hawa askari wetu pindi zinapotokea purukushani basi wao huona hapo ndio pa kuonesha utaalamu wao wa kufyatua risasi kwa hali halisi askari anaweza akaanza kazi mpaka akastaafu bila kufyatua risasi zaidi ya kwenye mafunzo.
Ushauri wangu kwa jeshi letu ambalo ndilo lenye dhamana ya kusimamia usalama wetu na mali zetu wajipange upya katika kukabiliana na migomo au maandamano pasipo kudhuru wananchi kwani hili linaleta chuki kati ya jeshi la polisi na wananchi, siamini kuwa hakuna njia nyingine ya kukabiliana na waandamanaji,swali la kujiuliza je waandamanaji wangekuwa wanaandamana na silaha za moto hali ingekuwaje?

Friday, June 10, 2011

PICHA YA LEO

Familia moja nchini Scotland kama inavyoonekana picha ambapo kila mtu katika familia hiyo anamiliki mnyama ampendae, tofauti kabisa na sehemu zingine tumezoea kuona watu wakimiliki vitu kama magari,baiskeli, pikipiki na vitu vingine...haya ukistaajabu ya Mussa utaona ya firauni.