Wednesday, February 29, 2012

Taifa Stars Vs Msumbiji

















Kikosi cha stars mazoezini juzi

KOCHA Taifa Stars, Jan Poulsen na kiungo Nizar Khalfan wamewataka Watanzania kuondoa wasiwasi kwa kuahidi kufanya vizuri kwenye mchezo wa leo dhidi ya Msumbiji.
Kauli hizo za Poulsen na Khalfan zinatokana na baadhi ya mashabiki wa Stars kukata tamaa na timu hiyo kwa kutokuwa na matokeo mazuri kwenye michezo yake ya kimataifa hivi karibuni pamoja na kutofurahishwa na uteuzi wa wachezaji wa kikosi hicho.
Wakizungumza na Mwananchi jana mara baada ya mazoezi ya timu hiyo, Poulsen alisema ana imani wachezaji wake watapata matokeo mazuri kesho kama wataungwa mkono na mashabiki wote.
"Watanzania wote kwa sasa wanapaswa kuwa kitu kimoja na kuendelea kutuunga mkono ili kuhakikisha tunaibuka na ushindi katika mchezo huo muhimu.
"Siwezi kuwalazimisha kuondoa hofu, lakini ningependa kuwaambia kuwa nina matuini makubwa vijana wangu kufanya vizuri kwenye mechi hiyo. Wachezaji wameonyesha uchungu na timu ya taifa," alisema Poulsen.
Alisema maneno mengi yanayosemwa na baadhi ya mashabiki kutokana na kutomwita Mbwana Samataa katika kikosi cha Stars, hayajengi isipokuwa jambo la msingi ni kuijitokeza kwa wingi na kuishangilia timu kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akiunga mkono kauli za kocha wake kiungo Khalfan alisisitiza kuwa Taifa Stars ina nafasi kubwa ya kuifunga Msumbuji.
Nizar aliyetemwa dakika za mwisho na klabu yake ya Philadephia Union ya Marekani alisema: "Nafikiri tuna kila sababu ya kushinda mchezo wa kesho, kila atakayepata nafasi yakucheza ajitume na kujitoa kwa ajili ya Taifa lake."
Alisema timu ya Zambia haikuwa na wachezaji wakutisha sana kwenye fainali ya Kombe la Mataifa Afrika zilizomalizika Gabon na Equatorial Guinea isipokuwa nyota wake walikuwa na moyo wakujitoa na kujituma zaidi.
"Naamini tukiweza kufuata hayo kutoka kwa ndugu zetu Zambia tutashinda mchezo huo tena kwa kishindo," alisisitiza.

Alisema tangu alipotua nchini Jumapili jioni amefurahishwa na morali aliyowakuta na wachezaji wa kikosi hicho na kusema ni dalili nzuri ya ushindi kwa Stars.
"Ni dalili nzuri kwetu kumwona kila mmoja wetu morali yake ikiwa juu, tunaomba mashabiki watupe sapoti ya kutosha ili tuweze kufanya yale ambayo yamekusudiwa na wengi," aliongeza.
Alisema anaamini kama watashinda mechi hiyo ya kwanza ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa Afrika 2013 watajiweka katika mazingira mazuri yakusonga mbele.
Katika hatua nyingine, alisema hafahamu sababu za Poulsen kumwacha Samatta.
"Sababu atakuwa nazo mwenyewe, siwezi kuingilia maamuzi yake, naamini Samata bado ana nafasi kubwa kwenye timu ya taifa," alisema Nizar.

Hii ni mara ya tano kwa Tanzania na Msumbiji kucheza kati ya hizo Mambaz imeshinda mechi mbili na kutoka sare mbili.
Watanzania wengi wanakumbukumbu ya bao la Tiko Tiko lililowanyima kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2008 nchini Ghana.

Monday, February 27, 2012

Liverpool mabingwa Carling Cup baada ya ukame wa miaka 6

Cup of joy: Gerrard lifts lifts the Carling Cup trophy as Liverpool celebrate
Liverpool wakishangilia ubingwa wa Carling

Ilikuwa fainali ya kukata na shoka iliyochezwa kwa muda wa dakika 120 baada ya kukosa mbabe ndani ya dakika 90 na hatimaye mshindi alipatikana kutokana na mikwaju ya penati.

Bright start: Cardiff's Joe Mason casually rolled his side into the lead in the first half
Joe Mason akitia "kambani" goli la kuongoza dhidi ya Liverpool

Comeback: After plenty of near misses, Liverpool hit back through Martin Skrtel
Martin Skrtel akiisawazishia Liverpool dakika ya 60

Ni miaka sita tangu kuwe na ukame wa vikombe kwa Liverpool na sasa wamekinyaka cha Carling. Mpambano ulianza kwa kasi na Cardiff ndio walikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za Liverpool goli likifungwa na Joe Mason, lakini Liverpool walijibu mapigo na kujipatia goli la kusawazisha kwa bao lililofungwa na Skrtel dakika ya 60.

Liverpool vs Cardiff

Hadi dakika 90 za kawaida zinamalizika timu hizo zilitoshana nguvu na mwamuzi wa mpambano huo  kulazimika kuongeza dakika nyingine 30.

Super sub: Kuyt scored within five minutes of coming on
Dirk Kuyt muuaji wa goli la pili

Katika kipindi cha pili cha dakika za nyongeza Mshambuliaji wa Liverpool Dirk Kuyt, alieingia kuchukua nafasi Andy Carrol alitia kambani na kuipatia Liverpool goli la pili katika dakika ya 108.
Vijana wa Cardiff hawakukata tamaa na zilipotimia dakika 118 mchezaji Ben Turner wa Cardiff alizima ndoto za Liverpool kuibuka mabingwa ndani ya dakika 120 baada ya kutupia kambani baada ya kizaazaa kutokana na kona iliyoelekezwa langoni mwa Liverpool.
Dramatic scenes: Ben Turner took the game to penalties
Ben Turner akitia kambani baada ya kizaazaa kutokea langoni mwa Liverpool kutokana na Kona
Atmospheric: Liverpool fans held a protest inside the ground against the launch of the Sun on Sunday
Mashabiki wa Liverpool

Baada ya dakika 120 kukamilika ndipo changamoto ya mikwaju ya penati ilipofikia ambapo Liverpool walifanikiwa kufunga penati 3 zilizotiwa nyavuni na Dirk Kuyt, Glen Johnson na Downing. Waliokosa ni Steven Gerrard na Charli Adam.

Timu ya Cardiff walifanikiwa kutia nyavuni penati mbili zilizopigwa na Don Cowie na Wittingham, na wachezaji waliokosa penati ni Kenny Miller, Rudy Gestede na Anthony Gerrard.
Magic moment: Liverpool's players rush to celebrate their win
Wachezaji wa Liverpool wakishangilia ubingwa baada ya binamu yake Steven Gerrald,Anthony Gerrald kukosa penati ya mwisho ya Cardiff.

Arsenal nomaaaa,yaibanjua Spurs 5-2


Thomas Rosicky akishangilia "kamba" ya tatu dhidi ya Spurs

Matokeo ya mwisho katika mechi kati ya Arsenal na Tottenham Hotspurs yalisomeka 5-2, Magoli ya Arsena yakifungwa na Sagna, Van Persie, Rosicky, Walcott*2. huku Saha na Adebayor wakiipatia Spurs mawili ya kufutia machozi. Mechi hiyo ilipigwa katika dimba la Emirates ambapo mashabiki wa Arsenal walishuhudia timu yao ikitoka nyuma kwa magoli mawili na kupata ushindi wa kishindo dhidi ya Spurs.

Robin Van Persie,Walcott na Chamberlain wakishangilia goli la nne

MUGABE ATIMIZA "NYUNDO" 88

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe

Sherehe za kuadhimisha Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kutimiza umri wa miaka 88, zimefanywa katika mji wa Mutare, mashariki mwa nchi, na maelfu ya watu wamehudhuria.
Matawi ya chama cha ZANU PF cha Rais Mugabe, yalichanga kugharimia sherehe hizo ambazo piya zilikuwa na mashindano ya warembo na mechi ya mpira.
Aliwaambia wafuasi wake kwamba wale wanaopinga msimamo wake dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na ndoa kati yao, wapotelee mbali.
Bwana Mugabe alikanusha kuwa ni mgonjwa, na mapema juma hili alisema yeye kakazana kama kigongo na anaweza kuongoza nchi..
Umri wake pamoja na taarifa kuwa Rais Mugabe anauguwa saratani ya kibofu, imezusha wito mwengine kuwa Zanu PF inafaa kubadilisha uongozi.
Lakini chama chake kimemuunga mkono agombee tena urais mwaka huu.

Friday, February 24, 2012

MAN UNITED CHUPUCHUPU EUROPA

Manchester United iliponea chupuchupu kufungwa na Ajax ya Uholanzi katika uwanja wa nyumbani wa Old Trafford.
Javier Hernandez
Chicharito akitupia kambani bao la kufutia machozi wakati Man U ilipofungwa na Ajax licha ya kufuzu kuendelea kucheza Europa

Bao la Toby Alderweireld liliwalazimu kukubali kushindwa katika mechi hiyo ya Europa iliyochezwa Alhamisi jioni.
Licha ya hofu iliyosababishwa na Ajax, Man United ilifuzu kuwa miongoni mwa vilabu 16 ambavyo vitaendelea kucheza katika ligi hiyo ya Europa.
Sasa Man U inatazamiwa kukutana na Athletic Bilbao ya Uhispania
Lakini kutokana na wingi wa mabao, Man U ilifuzu kwa jumla ya magoli 3-2.
Ajax awali ilikuwa imeangamizwa kwa bao la awali la Javier Hernandez, baada ya kugongewa mpira vyema na Dimitar Berbatov.
Ingawa Man U wako njiani kuelekea kwa fainali Bucharest, ambako fainali itafanyika, kushindwa kwa timu hiyo kuliondoa matazamio mengi ya mashabiki, baada ya meneja wa muda wa timu ya England, Stuart Pearce, kuwachagua wachezaji sita kutoka Old Trafford, na ambao ni miongoni mwa wachezaji 25 watakaopambana na Uholanzi, Jumatano ijayo, katika mechi ya kirafiki.


Pearce alikuwepo uwanjani kutizama namna wachezaji wanne, kati ya hao sita, wakicheza; Tom Cleverley, Chris Smalling, Ashley Young na Phil Jones.
Licha ya kwamba Man U ilikuwa imeishinda Ajax, mabingwa mara nne barani Ulaya, walipokutana katika mechi yao ya awali, meneja Sir Alex Ferguson hakutaka utani katika mechi ya Alhamisi.

Man City kiboko,Inter Milan na Bayern Munich "Ndembendembe"


                       Man city 4-0 Porto

MABINGWA watetezi wa Europa Ligi, Porto wamevuliwa ubingwa huo baada ya kuchakazwa 4-0 na Manchester City na kuondolewa kwa jumla ya mabao 6-1 na vinara hao wa Ligi Kuu ya England juzi Jumatano.

Walifungwa 2-1 nyumbani hivyo timu hiyo ya Ureno ikawa na matumaini ya kurekebisha makosa ili iweze kusonga mbele kwa hatua ya 16 bora, lakini walipata pigo sekunde ya 19 kwenye Uwanja wa Etihad kwa bao la kuongoza la City lililofungwa na Sergio Aguero.

Katika usiku huo ambao kocha Roberto Mancini alisema mshambuliaji wake mtukutu Carlos Tevez amerejea baada ya kuwa nje kwa wiki kadhaa kufutia uamuzi wake wa kuomba radhi kwa kitendo cha kugomea kucheza, Aguero alionyesha kiwango cha juu na kuthibitisha kuwa City ina washambuliaji makini hata asipokuwepo Tevez.

Alitegeneza bao kwa mshambuliaji Edin Dzeko aliyeingia baada ya dakika ya 76 wakati City ilipoisambaratisha Porto.Pia bao la David Silva na David Pizarro yalikamilisha kalamu ya timu hiyo ya Mancini na kujikatia tiketi ya kufuzu kwa hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Porto walimaliza pungufu mchezo huo baada ya Rolando kuonyeshwa kadi ya njano ya pili kwa kumfokea mwamuzi akipiga bao alilolifunga Dzeko.

MARSEILLE, Inter Milan wamehadhibiwa kwa mbinu zao mbovu wakati Andre Ayew alipofunga kwa kichwa bao pekee na kuipa Olympique Marseille ushindi 1-0 kwenye mchezo huo wa kwanza wa Ligi ya Mabingw hatua ya 16 bora.

Ayew alifunga bao hilo akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Mathieu Valbuena katika dakika tatu za nyongeza na kuwaacha wachezaji wa Inter wakitikisa vichwa wasiamini kilichotokea.

Kocha wa Inter, Claudio Ranieri alimweka benchi mshambuliaji wa Argentina, Diego Milito, pamoja na kuwa huyo ndiye mchezaji pekee aliyeifungia timu hiyo katika michezo saba iliyopita, ukiwe ule aliofunga mabao nne walipotoka sare ya 4-4 na Palermo katika Serie A wiki tatu zilizopita.

Wesley Sneijder na Mauro Zarate hawakuwa kwenye kiwango kizuri dhidi ya Marseille, lakini Milito hakuingizwa na Ranieri alipotumia wachezaji wawili wa akiba kati ya watatu huku Giampaolo Pazzini pia alibaki benchi.

“Milito alikuwa na mafua wiki hii. Sikutaka kuhatarisha afya yake,” alisema Ranieri.Ranieri anaonekana anataka kujipanga kwa ajili ya mchezo wa marudiano utaofanyika nyumbani kwao San Siro hapo Machi 13.

BASEL, Timu ya Basel imepiga hatua moja kubwa katika Ligi ya Mabingwa baada ya kuidungua Bayern Munich kwa bao 1-0 na kujiweka vizuri kwenye harakati zake za kufuzu kwa robo fainali.

Mshambuliaji Valentin Stocker aliyeingia akitokea benchi alifunga bao hilo la ushindi kwa mabingwa hao wa Uswisi dakika ya 86 kwa shuti lililompita tobo kipa wa Bayern, Manuel Neuer.

Bayern walikosa mara mbili kwenye mchezo huo wakati mashuti ya Aleksandar Dragovic na Alexander Frei yalipogonga mwamba na kutoka, timu hiyo ya Uswisi ambayo mfumo wake wa kushambulia kwa kushtukiza ndio uliowamaliza Manchester United kwenye hatua ya makundi.

Hilo ni pigo jingine kwa Bayern ambao wamekuwa kwenye kiwango cha chini kwenye Bundesliga wakiwa nyuma kwa pointi nne kwa vinara Borussia Dortmund

STARS D.R.C HAKUNA MBABE

Timu ya mpira wa miguu ya Tanzania (TAIFA Stars) imeshindwa kutumia uwanja wake wa nyumbani kwa kukubali kulazimishwa suluhu na DR Congo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa ulitoa nafasi kwa makocha wa timu zote kuangalia ubora wa vikosi vyao kabla ya kucheza mechi zao za kuwania kufuzu kushiriki Kombe la Mataifa ya Afrika 2013.

Taifa Stars itawakaribisha Msumbiji kwenye uwanja huo Jumatano ijayo katika kampeni yake ya kusaka tiketi ya kwenda Afrika Kusini.

Stars ilianza mchezo huo kwa taratibu na kuwaruhusu DR Congo kufanikiwa kufika langoni kwa Taifa Stars mara mbili ndani ya dakika 5, kupitia kona ya Mutombo na mpira wa adhabu wa Kasusula Kilisho uliogonga mwamba na kutoka baada ya Tresor Mputu kufanyiwa faulo na Stephano Mwasika.

Katika mechi hiyo nahodha Shadrack Nsajigwa nusura amchape makofi mshambuliaji Hussein Javu baada ya kupiga shuti hafifu akiwa yeye na kipa Bolongo kwenye mchezo huo ulioshudiwa na mashabiki wachache wa Tanzania, pia kulikuwa na kikundi cha mashabiki kutoka DR Congo.

Stars walijitahidi kutawala mchezo huo, lakini Congo inayoundwa na nyota wengi wa TP Mazembe walionekana kumiliki vizuri zaidi sehemu ya kiungo, ila washambuliaji wake walikosa umakini kwenye umaliziaji.

Katika dakika ya 22 kipa Juma Kaseja alifanya kazi kubwa ya kumzuia Deo Kanda asifunge baada ya mshambuliaji huyo kuwatoka mabeki wa Stars na kupiga shuti la pembeni vilevile dakika ya 24 Mwasika aliushika mpira katika harakati za kuokoa na mwamuzi Israel Mujuni aliamuru faulo iliyopigwa na Kasusula na kutoka nje.

Ngome ya Stars ikiwa chini ya Agrey Morris, Juma Nyoso, Nsajigwa na Mwasika katika kipindi cha kwanza ilikuwa imara na kucheza vizuri ili kuhakikisha wanawazuia vilivyo washambuliaji wa Wakongo.

Mshambuliaji Mrisho Ngasa alifanya juhudi binafsi katika dakika ya 32, ambapo alipiga shuti la mbali la mita 35, lakini shuti hilo lilipaa juu kidogo ya goli la DR Congo.

Pia John Boko alijitahidi kufunga baada ya kutuliza mpira vizuri na kupiga shuti kali akiwa nje ya 18 katika dakika ya 45, ambapo shuti lake lilipaa sentimita chache kwenye lango la Congo.

Mwanzoni mwa kipindi cha pili kocha wa DR Congo, Claude Le Roy alimpumzisha kipa Bolongo na kumwingiza Kidiaba Muteba wakati Jan Poulsen aliwatoa Ngasa, Kaseja, Javu na Nsajigwa na kuwaingiza Mwadini Mwadini, Said Nasoro, Uhuru Selemani na Nsa Job.

Dakika ya 56, kipa Mwadini alithibisha ubora wake kwa kuokoa kwa ufundi mkubwa mpira wa kichwa uliopigwa na Kayiba, ambapo Stars ilijibu mapigo dakika moja baadaye baada ya Boko kujirusha vizuri kujaribu kufunga kwa kichwa krosi iliyopigwa na Abdi Kassim.

Kocha Poulsen alifanya mabadiliko mengine katika dakika ya 58 kwa kuwatoa Mwinyi Kazimoto, Kassim na kuwaingiza Jonas Mkude na Abubakar Salum 'Sure Boy' nao Congo waliwatoa Mputu na kumwingiza Amomo Ngoy.

Pamoja na makocha wote kufanya mabadiliko hayakuweza kuwasaidia kwani hadi filimbi ya mwisho inapulizwa na mwamuzi Mujuni matokeo yakulikuwa suluhu.