Saturday, June 18, 2011

PICHA YA LEO

WACHEZAJI GHALI NA WANAOLIPWA ZAIDI 2011.

Unaweza kuwaita kuwa ndio wachezaji ghali na matajiri,vilevile ukawaita ndio wachezaji bora zaidi duniani. Kwa hivi sasa wachezaji ghali zaidi ni kama ifuatavyo;

1} CHRISTIAN RONALDO, Huyu ndiye mchezaji ghali zaidi aliyegharimu uhamisho wa paundi za uingereza milioni 80, kutoka Man U kwenda Real Madrid. Huu ndio uhamisho ghali zaidi kuwahi kutokea katika soka ambao mpaka sasa bado ni gumzo.

2} RICARDO KAKA, Huyu anasadikika kuwa ndiye mchezaji bora na mwenye kasi aliyewahi kutokea katika ulimwengu wa soka. Ambapo aliigharimu Real Madrid kitita cha Paundi za uingereza milioni 56 kumng'oa katika kikosi cha AC Milan ya Italy. Pamoja na kuwa na kipaji na ujuzi, Kaka hakuweza kuonesha makeke yake akiwa Real kutokana na kuwa majeruhi mara kwa mara lakini hamna shaka anaweza kurudi katika kiwango chake pale atakaporejea katika hali yake.
3} ZLATAN IBRAHIMOVIC, Huyu alikuwa ni mmoja kati ya wachezaji bora duniani,na alikuwa katika kiwango cha hali ya juu katika kipindi cha mwaka 2007-2008 katika msimu wa ligi ya Italy. Alinyakuliwa na Barcelona kwa kitita cha paundi za uingereza milioni 60.7 kutoka Inter Milan ya Italy.

4} FERNANDO TORRES, Huyu ni mmoja kati ya wachezaji bora katika ligi ya Uingereza ambapo mwaka 2007-2008 alishika nafasi ya pili kama mchezaji bora wa ligi kuu Uingereza namba moja akiwa ni Christian Ronaldo. Torres alinyakuliwa na Chelsea ya Uingereza kwa kitita cha paundi za Uingereza milioni 50 kutoka Liverpool pia ya Uingereza. Pamoja na kutokufanya vizuri akiwa Chelsea Torres bado ananafasi ya kufanya vizuri akiwa na Chelsea katika msimu ujao wa ligi.
5} ZINEDINE ZIDANE, Huyu ni mmoja kati ya wachezaji wenye ujuzi "skillfull" duniani, amliichezea Ufaransa mara mbili katika kombe la dunia na kuiwezesha Ufaransa kutinga fainali mwaka 2006.

6} LUIS FIGO, Huyu alikuwa ni ni mchezaji mzuri sana na inaaminika katika kipindi chake alikuwa mchezaji bora duniani ambapo aliigharimu Barcelona kumng'oa kutoka Real Madrid kwa paundi za Uingereza milioni 37.

7} HERNAN CRESPO, Crespo alikuwa ni mchezaji wa hali ya juu kipindi Figo yupo kwenye chati,na inaaminika Crespo ni kati ya wachezaji bora duniani ambapo alinunuliwa kwa paundu za Uingereza milioni 35.5 na timu ya Lazio ya Italy akitokea Parma pia ya Italy.

8} ANDY CAROLL, Huyu alipata uhamisho sio siku nyingi sana ni 2011 kutoka Newcastle kwenda Liverpool zote za Uingereza kwa kitita cha paundi za Uingereza milioni 35.
9} DAVID VILLA, Huyu hivi sasa ndio yupo katika kiwango chake,alipata kiatu cha dhahabu na akiwa ni miongoni wa wafungaji bora katika fainali z kombe la dunia 2010 akiichezea Uhispania. Alinyakuliwa na Barcelona Uhispania kwa kitita cha paundi za Uingereza milioni 34.2 akitokea Valencia pia ya Uhispania. Villa anategemewa kufanya mazuri zaidi kama atabaki Barcelona.
10} GIANLUIGI BUFFON, Ukiongelea golokipa bora katika historia ya soka....Buffon anasadikika kuwa golikipa bora zaidi duniani baada ya Oliver Kahn wa Ujerumani. Huwa haijalishi ni timu gani anachezea ana uwezo wa kupangua michomo ambayo huwafanya wachezaji wenzake warudi mchezoni, alisajiliwa na Juventus kwa paundi za Uingereza milioni 32.6 akitokea Parma zote za Italy. Buffon amemuoa mwanamitindo wa Czeck Seredova. 
 
 
 
 
 

Friday, June 17, 2011

NG'OMBE ALIYEKATA KAMBA AZUA KIZAAZAA MTAANI.

Ng'ombe aliyekuwa amefungwa katika nyumba moja nchini Sri lanka , haijulikani ni kwasababu alikuwa na njaa au alikuwa na hasira gani ghafla alikata kamba na kuanza kukimbia mitaani na kusababisha taharuki kwa wapita njia kama inavyoonekana pichani. Haikuweza kufahamika mara moja kama baada ya tukio hilo huyo ng'ombe alikamatwa vipi na je kuna mtu aliyejeruhiwa au kuuwawa.

VITU 10 KWA MWANAMKE VINAVYOMPENDEZA MWANAUME.

Katika historia ya mwanadamu tunaelezwa kuwa mungu baada ya kuumba kila kitu duniani aliamua na kuumba mtu wa kuvitawala vitu hivyo,ndipo akamuumba Adam na baadaye akaona sio vyema Adamu awe peke yake akaamua kumuumba mwenza wake ndipo akamuumba Hawa. Hivyo Adam akiwa ni jinsia ya kiume na Hawa ni jinsia ya kike ,akawaambia wautawale na kuujaza ulimwengu.Wataujazaje ulimwengu? ni kupitia kujamiiana na hatimae wazae watoto nao waje wazaane na kuujaza ulimwengu.
Kutokana na hilo Duniani watuy tumekuwa tukipendana na kila mmoja na vigezo vyake binafsi katika kupenda lakini leo nina vitu ambavyo wanaume wengi huvipenda kwa mwanamke,kama ifuatavyo;

1} UZURI WA ASILI, hivi unajua kama wanawake Marekani wanatumia dola 200 za marekani kwa ajili ya vipodozi? lakini mwisho wa siku wanaume wamekuwa na mapenzi na wanawake wenye uzuri wa asili,wanapenda ngozi safi na ya asili. wengi wanasema wanapenda kumuona mwanamke katika muonekano uleule muda wote iwe anatoka kulala, au kuoga na hata akiwa kazini sura yake na muonekano unakuwa ni wa asili.

2} MUONEKANO WA TUMBO, Wanaume wengi hupenda tumbo la mwanamke ambalo lipo katika mkao mzuri linaonekana kuendana na mwili wa mwanamke."Napenda tumbo lake" anasema Derke mwenye miaka 30, "Ni la duara" aliendelea, napenda anavyolimaintain na ni laini.

3} UCHANGAMFU, Wanaume wengi wanapenda wanawake wachangamfu,wenye matendo ya kuwafurahisha wanapokuwa wawili,ubunifu wa mambo fulanifulani humfanya mwanaume kuvutiwa na mpenzi wake wawapo wawili ikiwa ni pamoja na wakati wa tendo la ndoa au wanapokuwa wanapunga upepo au wamepumzika. "mke wangu anaimba nje ya key kabisa"anasema Ivan,miaka 38. "anapoimba bafuni,inapendeza ingawa sauti inatisha lakini haiachi kunichekesha"aliendelea kusema juu ya mpenzi wake. Vilevile kucheza wakati mnaposikiliza muziki ni njia mojawapo ambacho mwanaume atapenda amuone mpenzi wake akijaribu kufanya hivyo sio lazima awe anajua sana.

4} NYWELE, Muonekano wa nywele huwavutia sana wanaume,pale ambapo mwanamke anatunza nywele zake na kuwa na muonekano mzuri iwe ni za asili au zilizowekwa dawa au za bandia ili mradi ziendane na jinsi alivyo ambapo zitamfanya apendeze. "Mke wangu ana nywele ndefu sana akiingia bafuni inamchukua masaa mawili kila siku kwa ajili ya nywele tu,ni kitu kizuri" anasema Steve miaka 30.

5} KOPE, "Napenda macho yake"anasema Trevor miaka 46. "wakati mwingine anaponiangalia nikimtazama macho na jinsi kope zilivyo huwa vinanifanya nitamani tuende kitandani moja kwa moja" aliongezea. "macho yake ni moja ya vitu vinavyonivutia kwake,yananifanya niwe na hisia za moja kwa moja kwake"alimalizia.
 "Mpenzi wake ana kope za ajabu,ningependa niwe na msichana kama yeye" alisema Vik miaka 26 rafiki yake Seth.

6} MIGUU, Miguu ya mwanamke haijalishi mnene, mwembamba,mfupi au mrefu ili mradi iwe na mwonekano mzuri, "Miguu yake ni laini,napenda vile inavosisimua na wakati anapovaa viatu virefu hakika hunitia wazimu" alisema James 26,alipomuongelea mpenzi wake Sarah.
 "mimi binafsi ni mzaifu nionapo miguu,hivyo anapoipitisha katikati yangu huwa siwezi kujizuia,nae anafahamu hilo" alisema David 43. "Napenda miguu ya mwanamke lakini sijui kwanini,miguu ya wanawake ni ya kifahari ambayo sisi hatuna,ninapenda kitu tofauti ndio maana kwanini napenda matiti kwasababu mimi sina" alisema Nate 32.

7} STAILI YAKO, Wanaume huvutiwa na vile mwanamke anavyojua kupangilia viwalo,jinsi ya kujua ni ni cha kuvaa na kwa wakati gani hakika huwavutia wanaume hasa pale mwanamke anapotoka bomba. Lazima ujue ukivaa nini inakufit na kukutoa chicha,pia ujue jinsi ya kupangilia vitu yaani kuanzia viatu,nguo,mikoba,hereni,bangili na hata cheni.

8} MANUKATO, "Sifahamu anawezaje,lakini muda wote ananukia vizuri" alisema Brent 29."Hata kama anatoka kuoga" alisema. "Napenda kumnusa maeneo haya",anasema Damien 35 huku akionesha sehemu za shingoni kwa mpenzi wake. Kuna wanaume wengine wanadiriki kusema huwa hawafikirii mwanamke atavaa nini zaidi ya kufikiria jinsi atakavyonukia.

9} KUSEMA UNACHOTAKA, Katika mapenzi kila mtu ana uhuru wa kusema ni nini anataka mpenzi wake amfanyie na kipi asifanye,ingawaje wanawake wengi hawalifahamu hili kwani imefikia wanachagua vitu vya kuomba na vingine kuona sio haki yao,mfano tendo la ndoa wanawake wengi husubiri mpaka mwanaume aanze kusema yeye kimya. pia wakati wa tendo miguno ya mwanamke na maelekezo ya wapi pa ku kita na wapi pa kupekecha mwanamke anaposema mwanaume hufurahia tendo na kumfanya kumpenda zaidi mwanamke.

10} KAZI YAKO, Mwanamke anaewajibika humvutia mwanaume. wanaume wengi wanasema wanapenda kuwaona wanawake wao wakiwa sehemu zao za kazi wakiwajibika." Anafanya kazi katika shule ya awali,napenda ninapomuona akifundisha na kucheza na watoto" anasema Garisson 42. "mke wangu ni Profesa wa masuala ya wanawake,napenda kumuona akifundisha wanawake wenzake kupata kazi na kupigania haki zao"anasema Samuel 49.

ASHUSHWA KWENYE NDEGE KWA KUVAA MLEGEZO.

Marman

Kijana mmoja nchini Marekani ajulikanae kama Marman mwenye umri wa miaka 20 pichani juu alijikuta akiingia katika masahibu ya kushushwa kwenye ndege baada ya kugundulika amevaa suruali huku ameishusha mpaka chini ya matako hapa chini maarufu kama "mlegezo au kata K" na kuacha nguo ya ndani ikionekana bila tabu, wakati Wamarekani wao wanaita "Baggy Pants" kwa kiswahili maana yake ni suruali bombo.
"Siku ya jumatano muda wa saa tatu asubuhi polisi wa San Francisco walipokea simu kuwa nje ya geti la shirika la ndege la marekani kuna mtu amevaa hovyohovyo" alisema Sgt Michael Rodriguez. Wafanyakazi wa uwanja wa ndege walimuona kabla Marman hajapanda ndege 488,walipomuona amevaa suruali chini ya matako lakini juu ya magoti walimtaka kupandisha suruali yake lakini Marman alikaidi amri hiyo na kuendelea na safari ya kuingia ndani ya ndege,ndipo wafanyakazi hao walipoamua kupiga simu polisi na polisi walipofika uwanjani hapo walimkuta Marman ameshaingia ndani ya ndege na amekaa raha mustarehe. Askari walipomuamuru kushuka aliwajibu itanichukua dakika 15 mpaka 20 kushuka ndipo askari walipomkamata kwa kosa hilo,na kuachiwa siku ya alhamisi kwa dhamana ya dola 11,000 za kimarekani.
Mama wa Marman alipohojiwa alisema mwanae alikuwa na hali mbaya kihisia kwani alitoka kuhudhuria mazishi ya rafiki yake ambaye ni mwanafunzi mwenzake siku ya jumanne baada ya kuuwawa. Lakini wamarekani wengi wamejitokeza kulalamikia swala hilo na kusema lina uhusiano na ubaguzi wa rangi kwani Marman alivaa jinsi ambayo ilikuwa haimkeri mtu moja kwa moja.

Thursday, June 16, 2011

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA.

Leo ni maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika, Siku hii barani Afrika inaadhimishwa huku kukiwa na changamoto nyingi zinazoikabili jamii nzima ya Afrika kuhusiana na malezi ya watoto. Watoto Afrika wanakabiliwa na changamoto za maisha duni ya jamii kubwa barani Afrika ambapo katika nchi nyingi za kiafrika inaaminika kuwa familia nyingi zinaishi maisha ya taabu ambapo matumizi ya familia kwa siku yanasadikika kuwa ni chini ya dola moja ya kimarekani. Kutokana na jamii kubwa kuwa na maisha ya hali ya chini inapelekea malezi ya watoto nayo kuwa duni,watoto wanakosa haki za msingi kutokana na familia zao ama wazazi kutokuwa na uwezo wa kuwatekelezea haki hizo ambazo ni pamoja na haki ya kusoma, chakula, malazi,michezo na haki nyinginezo.

Watoto wana haki ya kupata elimu.

Siku hadi siku wimbi la watoto wa mitaani limezidi kuongezeka kutokana na ukweli kuwa maisha yanazidi kupanda kadri siku zinavyozidi kwenda na familia nyingi kujikuta kusambaratika kutokana na kutokuwa na uwezo wa kukaa pamoja na kupata mahitaji ya kila siku.

Watoto wana haki ya kupata chakula bora.

Leo ikiwa ni siku ya mtoto wa Afrika hatuna budi kutafuta mbinu za kukabiliana na matatizo yanayowakabili watoto, tuangalie ni jinsi gani tunaweza kuboresha mazingira yao ya kusomea yaani shule, pia tuweze kuangalia jinsi gani tutawatoa watoto waliopo mitaani ambapo hapa Tanzania inasadikika watoto wa mitaani ni wengi sana hasa katika mikoa ya Dar es salaam, Dodoma,Mbeya,Singida na Kilimanjaro. Viwanja vya kuchezea watoto visimilikiwe na watu kwani kufanya hivyo ni kuwanyima haki yao ya msingi, Kwa pamoja tuwe na wito unapomuona mtoto a mwenzio basi umuone na kumthamini kama mtoto wako wa kumzaa hapo ndio tunaweza kuwalea na kuwatunza katika maadili yaliyo mazuri.
Watoto wana haki ya kucheza.

Watoto wana haki ya kulala mahala safi na salama.





BAMBO APATA AJALI YA PIKIPIKI AVUNJIKA MGUU.

Wasanii wakimuangalia Bambo kitandani kwa huzuni.

Dereva wa pikipiki iliyokodiwa na Bambo akiwa hoi hospitalini.

Msanii maarufu wa maigizo Dickson Makwaya a.k.a BAMBO leo alfajiri maeneo ya Kigogo amepata ajali mbaya ya pikipiki, baada ya pikipiki aliyokuwa ameikodisha kugongwa na daladala aina ya DCM na kusababisha Bambo kuvunjika mguu wa kulia sehemu ya paja huku ajali hiyo ikimuacha dereva wa pikipiki hiyo akiwa katika hali mbaya, wote wamelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu.