Monday, May 7, 2012

SIMBA YAIRARUA YANGA 5-0, OKWI AINYANYASA BEKI YA YANGA,LOYD NCHUNGA ATOKA ATIMUA MBIO BAADA YA BAO LA TANO, MASHABIKI 3 WAZIMIA UWANJANI


Kioo cha matangazo cha uwanja mkuu wa Taifa kilivyokuwa kikisomeka katika dakika za majeruhi

Lloyd Nchunga jana alishindwa kuvumilia na kuamua kukimbia uwanjani baada ya timu yake kutandikwa bao la nne, wakati Yanga ilipopokea kipigo cha Paka mwizi cha mabao 5-0 kutoka kwa wapinzani wao, Simba.
Mwenyekiti huyo ambaye hivi karibuni alijikuta katika wakati mgumu, baada ya wazee wa klabu yake kutaka kuichukua timu mikononi mwake, alishuhudia mvua ya mabao kutoka kwa mabingwa, Simba, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar na kuzidi kuwa katika hali ngumu zaidi.
Katika mchezo huo, Simba walianza kupata bao dakika ya kwanza tu ya mchezo kupitia kwa Emmanuel Okwi aliyeunganisha vizuri pasi ya Felix Sunzu baada ya Nurdin Bakari kupoteza mpira karibu na lango la Yanga.

Nimewanyongaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa


Mchezaji aliyei-cost Yanga kuliko mchezaji mwingine yeyote Shadrack Nsajigwa


wa Yanga Papic jukwaani akiAliyekuwa kocha mkuu shuhudia timu hiyo ikinyanyaswa na Simba

Baada ya bao hilo, Yanga walifanya mashambulizi kadhaa katika dakika ya tisa na 11 huku shuti moja lililopigwa na Athuman Idd ‘Chuji’ likigonga mwamba na kurejea dimbani kabla Hamis Kiiza kupiga tena na safari hii mlinda mlango Juma Kaseja akiucheza mpira na baadaye kuokolewa na mabeki wake.

Okwi akishangilia baada ya kuitengeneza Yanga goli la kwanza

Kipindi cha kwanza kiliisha kwa Simba kuendelea kuongoza kwa bao 1-0 lakini kipindi cha pili ndicho kilichopeleka simanzi kubwa Jangwani baada ya kushuhudia kipa Said Mohammed aliyechukua nafasi ya Yaw Berko, akiokota mipira minne langoni mwake.
Aibu ya Yanga ilianzia dakika ya 53, baada ya Felix Sunzu, kupiga penalti kwa ufundi akiandika bao la pili. Penalti hiyo ilitokana na Okwi kuchezewa faulo katika eneo la hatari.
Dakika ya 62, Okwi alifanya tena kazi ya ziada, alipomtoka beki mkongwe, Shadrack Nsajigwa na kufunga bao safi lililowaacha wachezaji wa Yanga wakiwa wameshika viuno kwa huzuni.

Huku Jangwani wakiendelea kujiuliza, Simba walipata penalti nyingine katika dakika ya 66 baada ya Okwi kufanyiwa faulo tena ndani ya eneo la hatari na kipa, Mohammed. Juma Kaseja ndiye aliyepiga penalti hiyo na kuiandikia Simba bao la nne.


Nahodha wa Simba Juma Kaseja Juma akikabidhiwa kombe la ligi kuu ya Tanzania bara

Wachezaji wa Simba wakishangilia na kombe lao

Katika hali ya kushangaza, Simba walipata penalti ya tatu dakika ya 71 iliyotokana na beki, Athuman Idd ‘Chuji’ kumfanyia faulo Okwi ndani ya eneo la hatari. Patrick Mafisango alipiga penalti hiyo na kufikisha bao lake la 11 kwenye Ligi Kuu ya Bara msimu huu.
Katika tukio la kusikitisha, mashabiki wawili wa Yanga walizimia na kubebwa na watu wa Msalaba Mwekundu, baada ya Mafisango kufunga bao la tano huku Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Fred Felix Minziro, akigoma kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu mchezo huo.
Naye Kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic, amesema baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa, kwa sasa wanachokiangalia ni kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza Yanga ilifanikiwa kuichapa Simba bao 1-0.

Katika matokeo mengine, licha ya Villa Squad kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mlandizi, Pwani, ilijikuta ikishuka daraja na kuungana na Polisi Dodoma pamoja na Moro United.

Umati uliohudhuria kichapo cha Yanga

Kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, JKT Oljoro ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi, wakati huko Mkwakwani, Tanga, Toto ilipata kipigo kama hicho kutoka kwa Coastal Union na kunusurika kushuka daraja kutokana na kuwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa licha ya kuwa na pointi 26 sawa na Villa.
Mtibwa Sugar iliendeleza ubabe wake kwa kuifunga Moro United bao 1-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Azam ikiishinda Kagera mabao 2-1, Chamazi, Dar na African Lyon ikiibamiza JKT Ruvu mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro

e

Sunday, May 6, 2012

CHELSEA BINGWA FA


Ramires akitupia bao la kwanza

Chelsea wamechukua ubingwa wa Kombe la FA Cup kwa mara ya saba, kufuatia magoli kutoka kwa Ramires na Didier Drogba dhidi ya Liverpool.

Ramires alifunga kufuatia kosa la Jay Spearing, kabla ya Didier Drogba kufanikiwa kumkwepa Martin Skrtel na kuandikisha bao la pili.


Drogba akishangilia baada ya kutia kambani bao la pili

Liverpool walionyesha mchezo duni hadi Andy Carroll alipofunga bao moja baada ya John Terry kukosa kuimarisha ngome ya Chelsea kikamilifu, na mabao kuwa ni magoli 2-1.


Patashika katika fainali hiyo

Kulikuwa na ubishi kwa muda uwanjani baada ya Carroll kudhani alikuwa amefunga bao la kusawazisha kwa kichwa, na Petr Cech kuutema mpira huo, ambao kwanza uligonga mwamba na kuanguka mbele ya msitari.

Wachezaji na mashabiki wa Liverpool wote walidhani mpira ulikuwa umevuka msitari.
Binafsi kwangu mimi lile lilikuwa goli safi kabisa lakini mbeleko katika soka imoooo!

Wachezaji wa Chelsea wakishangilia na kombe la FA


Drogba na Kalou wakiwa wameposs na kombe la FA


Kocha aliepata mafanikio ya muda mfupi na Chelsea Robert De Matteo

Thursday, May 3, 2012

BURUDANI TIME (18+)

PAPISS DEMBA CISSE ATUPIA KAMBANI GOLI LA MSIMU WAKATI NEWCASTLE IKIIADHIBU CHELSEA

Goli la msimu la Demba Cisse dhidi ya CHELSEA

Timu ya soka ya Newcastle United jana waliwaadhiri wababe walioingia fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya timu ya Chelsea katika mtanange wa ligi kuu ya Uingereza kwa kuigaragaza kwa magoli 2-0 katika dimba lao la nyumbani hapa naizungumzia Stamford bridge.

 Papiss Cisse Chelsea
Papiss Demba Cisse akiachia mkwaju ulioelekea moja kwa moja kwenye nyavu za Chelsea zikimuacha golikipa Peter Cech akiwa ananing'inia bila mafanikio

Katika mechi hiyo Demba Cisse alitupia kambani mara mbili ambapo dakika ya 19 alimtesa vilivyo Peter Cech wa Chelsea na dakika za nyongeza akatupia la pili na kukamilisha shughuli iliyokuwa na pilipili nyingi kwa upande wa Chelsea wakati Newcastle wakiifurahia kwa ndimu iliyokolea.

Wednesday, May 2, 2012

FULHAM YAVUNJA MWIKO KWA LIVERPOOL YAICHAPA 1-0


Beki wa Liverpool Skrtel akiutazama mpira uliomgonga ukielekea wavuni

Bao la kujifunga la Martin Skrtel lilileta masikitiko mengi usiku wa Jumanne wakati walipoikaribisha Fulham katika uwanja wa Anfield, na kuwasaidia wageni kuandikisha historia, ikiwa ni mara yao ya kwanza kupata ushindi katika uwanja huo.

Lakini inaelekea meneja wa Liverpool, Kenny Dalglish, hakuwa na wasiwasi mno, kwani tangu mwanzo aliichezesha timu dhaifu, wachezaji wake mahiri akiwapumzisha na anakusudia kuwatumia kikamilifu katika pambano la fainali la Kombe la FA mwishoni mwa wiki.

Liverpool walipata nafasi za kusawazisha, lakini Mark Schwarzer hakuwa mbunifu katika kumalizia na kuelekeza mikwaju vyema.


Mshikemshike katika mechi hiyo

Fulham pia walishindwa kujiongezea mabao, kwani Kerim Frei aligonga mwamba, na kipa wa Liverpool Doni pia aliweza kuiokoa timu yake kutoka kwa makombora zaidi ya Pavel Pogrebnyak na Clint Demsey.

Matokeo hayo yanamaanisha Fulham sasa ina pointi 49, sawa na Liverpool.


Ngoma nzito Climp Dempsey na Martin Kelly

Liverpool imo katika nafasi ya nane, na msimu huu imeshinda mechi tano tu, kati ya 18, na sasa wameachwa nyuma kwa pointi tatu na Everton, ambao pia usiku wa Jumanne walikamilisha mechi yao kwa sare ya 1-1 dhidi ya Stoke City.


Dunny Murphy akimkwatua Albert Riera wa Liverpool

Bila shaka mechi hii itakumbukwa na mashabiki wengi wa Liverpool, na ambao watajiuliza timu yao imejiandaa vipi katika kupambana na Chelsea katika fainali ya Kombe la FA, Jumamosi, tarehe 5 Mei.

MATOKEO KIDATO CHA SITA 2012