Tuesday, July 10, 2012

Wimbo wa leo BOB JUNIOR-Nichum

MPAMBANO WA SOKA WABUNGE WA SIMBA NA YANGA KATIKA PICHA


Timu za wabunge wa Simba na Yanga wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya mpambano

Waamuzi wa mpambano huo wakipiga picha ya pamoja na manahodha wa timu zote mbili

Wabunge wa Simba katika Dua kabla ya mtanange kuanza


Wabunge wa Yanga nao wakipiga dua kabla ya mtanange kurindima

Mashabiki wakiwahi mpambano

Mtanange umeanza


Mwamuzi wa mtanange huo Athuman Kazi akifuatilia kwa karibu kuhakikisha haki inatendeka


Mh Zitto Kabwe wa Simba akitoa pasi murua kama Iniesta vile!


Mbunge wa Simba akitiririka na kabumbu















Katibu uenezi wa CCM Nape Nnauye akifuatilia mpambano wa Wabunge wa Simba na wale wa Yanga katika dimba kuu la Taifa jijini Dar es salaam


Benchi la ufundi la Wabunge wa Simba wakifuatilia mpambano


Benchi la ufundi la Wabunge wa Yanga wakiongozwa na kocha mkuu mpya wa Yanga


Mbunge wa Yanga akiwa hoi bin taaban


Mbunge wa Yanga akijaribu kuihadaa ngome ya wabunge wa Simba


Hali tete mlinda mlango wa wabunge wa Yanga baada ya kichapo kwa njia ya matuta 3-2


Wera weraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!! wabunge wa Simba hatimae waliwachapa wa Yanga katika matuta baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 0-0




Nani kama Simbaaaa woyooooo woyooooooooo


Hakunagaa zaidi ya Simba hakunagaa, hakunaaa hakunaaaa hakunaaaaaaaaaa!!!


Weraaaaa tupishe tupiteeee, tupisheeeee tupishe tupiteeeeeeee..Wabunge wa Simba wakiongozwa na Mh Zitto Kabwe na William Ngeleja kuserebuka baada ya kuwaangushia kisago wenzao wa Yanga kwa mikwaju ya penati 3-2
Mpambano Wabunge SIMBA Vs YANGA

Katika mtanange huo baada ya dakika 90 na kipyenga cha mwamuzi Athumani kazi kupulizwa matokeo yalikuwa ni 0-0. Mpambano huo wa kufurahisha na kusisimua uliopigwa katika dimba kuu la Taifa jijini Dar es salaam ikiwa ni katika mchezo wa hisani kukusanya pesa kuchangia ujenzi wa mabweni kwa shule za sekondari nchini!

shukrani za pekee kwa waandaaji wa tamasha hilo ambalo pia liliwakutanisha wasanii wa Bongo flava na Bongo Movie hali kadhalika mpambano wa Masumbwi kati ya wasanii maarufu nchini na wenye kutengeneza vichwa vya habari katika redio na magazeti mbalimbali hapa nchini, ni Wema Sepetu na Jaquiline Wolper ambapo katika mpambano mpambano huo uliodumu kwa raundi mbili matokeo yalikuwa ni droo hakukuwa na mshindi.

KEITA AONDOKA BARCELONA NA "NDOO"14 HUKU TITO AKIMRITHI PEP GUARDIOLA


Seydou Keita

kiungo wa Mali Seydou Keita amekihama klabu ya Barcelona baada ya kukipiga kwa miaka minne.
Katika muda huo wa miaka minne, Keita aliisaidia Barcelona kuzoa jumla ya vikombe 14.
Wakati wakithibitisha kuondoka kwa mwamba huyo, Barca walimshukuru Seydou Keita kwa juhudi zake za kuiletea klabu hiyo ya Uhispania mafanikio na vile vile wakamtakia kila lakheri anakokwenda.

Keita na Sanchez wakiwa wamebeba kombe wakikipiga Barcelona

Kwa wakati huu kuna fununu kwamba mchezaji huyo wa Mali huenda anahamia klabu moja ya Uchina, Dalian Aerbin
Ikiwa hatiamae ataishia China basi Keita hatakuwa mchezaji wa kwanza kutoka bara la Afrika kufanya hivyo.
Majuzi nahodha wa timu ya Ivory Coast Didier Drogba aliwafuata Frederic Kanoute na Yakubu Aiyegbeni wa Nigeria kujiunga na timu za ligi kuu ya China.
Keita, mwenye umri wa 32, alijiunga na Barcelona mwaka 2008 kutoka Sevilla akiwa ni mchezaji wa kwanza kabisa ambaye Pep Guardiola alimsajili mara tu alipokwaa uongozi wa Barca.
Kabla ya hapo mchezaji huyo alikuwa Olympic Marseille, Lorient na Lens zote za Ufaransa na ndio baadaye akahima Seville ya Uhispania.
Keita amehama baada ya Guardiola kuondoka kama Meneja wa Barcelona na mahali pake kuchukuliwa na aliyekuwa naibu wake Tito Vilanova

Tito Vilanova kocha alierithi mikoba ya Pep Guardiola


Tito Vilanova akiwa na Pep Guardiola

Monday, July 9, 2012

RATIBA KOMBE LA KAGAME 2012


KAGAME CUP 2012 FIXTURE
1-Sat. 14th July 1 APR vs WAU SALAAM Uwanja wa Taifa 2pm

2-YANGA vs ATLETICO Uwanja wa Taifa 4pm

3-Sun. 15th July 3 AZAM vs MAFUNZO Chamazi 4pm

4-Mon. 16th July 4 VITA CLUB vs PORTS Uwanja wa Taifa 2pm

5-SIMBA vs URA Uwanja wa Taifa 4pm

6-Tue. 17th July 6 ATLETICO vs APR Uwanja wa Taifa 2pm

7-WAU SALAAM vs YANGA Uwanja wa Taifa 4pm

8-Wed. 18th July 8 VITA CLUB vs URA Uwanja wa Taifa 2pm

9-PORTS vs SIMBA Uwanja wa Taifa 4pm

10-Thu. 19th July 10 ATLETICO vs WAU SALAAM Uwanja wa Taifa 2pm

11-MAFUNZO vs TUSKER Uwanja wa Taifa 4pm

12-Fri. 20th July 12 PORTS vs URA Uwanja wa Taifa 2pm

13-YANGA vs APR Uwanja wa Taifa 4pm

14-Sat. 21st July 14 AZAM vs TUSKER Uwanja wa Taifa 2pm

15-SIMBA vs VITA CLUB Uwanja wa Taifa 4pm

16-Sun. 22nd July REST DAY


QUARTER FINALS

Mon. 23rd July 16 B2 vs C2
17 A1 vs C3

Tue. 24th July 18 C1 vs A2
19 B1 vs A3

Wed. 25th July REST DAY
SEMI FINALS

Thu. 26th July 20 Winner 16 vs Winner 17

Thu. 26th July 21 Winner 18 vs Winner 19

Fri. 27th July REST DAY

FINALS AND 3rd PLACE PLAY OFFS
Sat. 28th July 22 Loser 20 vs Loser 21
23 Winner 20 vs Winner 21

DIVA AFUNGUKA ANAETAKA KUMUOA AWE NA MILIONI 500 TASLIMU


Loveness Love "Diva"

Mtangazaji maarufu wa radio moja ya jijini Diva Loveness Love,Clouds Fm amefunguka na kusema kuwa anaetaka kumtoa katika geti la Mzee Malinzi ambaye ni baba yake pale msasani basi kidume huyo atahitajika kuwa na Milioni 500 Taslimu.
Mtangazaji huyo wa kipindi cha ala za roho cha Clouds FM kinachoanza saa nne za usiku alikuwa akifanya mazungumzo na mtangazaji mwenzake Adam Mchomvu katika kipindi cha XXL mida ya saa 9:30 mchana Diva alifunguka kwa kujiamini kuwa mwanaume anaetaka kumuoa ni lazima awe na milioni 500 taslimu,ndipo atamng'oa kwa Mzee Malinzi, katika mazungumzo hayo Diva alisisitiza na alipoulizwa kama hatotokea akaema basi...tungoje mimi na wewe hatujui yetu macho na masikio. Dunia hii.

Diva katika possssssssssssss

LIL WAYNE AHUDHURIA NDOA YA MAMA YAKE MZAZI

Lil-Wayne-and-Birdman-at-Ms-Citas-wedding
Lil Wayne na Birdman wakiwa kanisani wakati mama yake Lil wayne akifunga ndoa

LIl-Wayne-and-son-at-ms-Cita-and-Avery-wedding
Lil Wayne a.k.a Lil Wiz akiwa na kidume chake Sarah kanisani

Lil-Waynes-Daughter-Reginae
Binti yake Lil Wiz aitwae Reginae akiwa na mtoto wa kiume wa Birdman katika shughuli hiyo ya kukata na mundu

10
Padri akimfungisha ndoa mama yake Lil Wayne na baba yake mpya.

Birdman-at-Jacita-and-Averys-wedding
Birdman akimuongoza mama yake Lil Wayne Ms Jacinta

Lil-Wayne-gushing-over-his-mother
9 (1)
Lil Wayne akiwa na mama yake aitwae Jacinta katika ndoa ya Ms Jacinta na Avery

5 (1)
Binti yake Lil Wayne Reginae akiwaongoza wenzake kwenda kusimamia harusi ya bibi yake

Lil-Waynes-sons-by-Sarah-and-Nivea
Vijidume vya Lil Wayne,Sarah na Nivea vikitinga kanisani kusimamia harusi ya bibi yao

12
Burudani kabambe iliporomoshwa kanisani utaaaaaaaaaaaaaamu

Thursday, July 5, 2012

HASHEEM THABEET AULA OKC KUVUNA DOLA 880,000


Hasheem akifanya majamboooozz!!!

Nyota wa kikapu Mtanzania Hasheem Thabeet ameula baada ya kupata dili murua la kuhamia timu ya mpira wa Kikapu ya Oklahoma City Thunder (OKC) akitokea Portland Trail blazers ambapo kabla ya Portland alitokea Memphis Zote za nchini Marekani.
Habari zinasema Hasheem amesaini mkataba wa 'nyundo' mbili na anatarajiwa kuvuna umatemate wa kiasi cha dola za kimarekani 880,000 kwa mwaka a.k.a Nyundo.
Haya sasa vijana waliopo katika mchezo wa kikapu fuateni nyayo hizo.





Basketball sio lelemama lazima uwe umeshiba








Hasheem akiwa na rais wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea Ikulu jijini Dar es salaam

Menu time!!!!