Wednesday, July 18, 2012

SHOW YA LEKA DUTIGITE UWANJA WA LAKE TANGANYIKA KIGOMA POTEZA MBAYAA


Umati wa watu waliohudhuria Show ya Leka Dutigike iliyofanyika katika uwanja wa Lake Tanganyika,Kigoma na kushirikisha wasanii wote ambao ni wazaliwa ama wenye asili ya Kigoma. Wakiongozwa na wabunge Vijana Mh Zitto Kabwe,Halima Mdee,Ester Bulaya na Joshua Nassari.

Wasanii wanaounda kundi hilo la wasanii wa Mkoa wa Kigoma ni Chege,Mwasiti,Banana Zorro,Peter Msechu,Diamond,Linex,Fid Q,Baba Levo,Makomando,Abdu Kiba,Ommy Dimpoz,Recho na wengineo wengi.

Wasanii wanaounda kundi la Kigoma All Stars


Mh Zitto Kabwe akizungumza na wananchi waliohudhuria uwanja wa Lake Tanganyika




Mh Halima Mdee (mbele), Ester Bulaya(katikati) na Joshua Nassari wakiserebuka



Wabunge wakiserebuka


Fid Q akifanya makamuzi


Mwasiti nae akitoa burudani

HAPPY BIRTHDAY NELSON MANDELA "MADIBA"


Nelson Rolihlahla Mandela ametimiza miaka 94. Alizaliwa 18 Julai 1918. Aliwahi kuwa Rais wa Afrika ya Kusini na alishika wadhifa huo tangu mwaka 1994 mpaka 1999. Nakutakia maisha mema mzee Madiba Afrika bado inahitaji busara zako!

Mzee wa Afrika Nelson Mandela akiwa amebeba kombe la dunia pale Afrika ya Kusini ilipokuwa mwenyeji wa kombe hilo mwaka 2010 na Uhispania kuibuka bingwa wa Dunia katika ardhi ya Afrika.


Nelson Mandela enzi za kupigania uhuru

Tuesday, July 17, 2012

MAAJABU YA MSIKITI SHEIKH ZAYED NI MSIKITI MZURI KULIKO YOTE DUNIANI


Msikiti wa Sheikh Zayed Uliopo Falme za Kiarabu (U.A.E) ni msikiti mkubwa kuliko yote katika falme za kiarabu na ni msikiti wa Nane kwa ukubwa duniani. Na inasadikika kuwa ndio msikiti mzuri kuliko yote Duniani, msikiti huu ulijengwa katika kumbukumbu za kumuenzi marehemu Sheikh Zayed Bin Sultan Al Nahyan ambaye alikuwa sheikh maarufu katika falme za kiarabu na ndie mwaanzilishi wa Falme za kiarabu

Ifuatayo ni historia fupi ya Msikiti wa Sheikh Zayed,

Only freshly fallen snow can reflect the light with more intensity. Like a mirage the building soars above the shimmering Abu Dhabi heat.

The 82 domes and 1,096 rooms are not an optical illusion, but belong to a mesmerizing mosque of superlatives on the edge of this city in the Gulf, a house of worship that seems to beckon visitors from afar.

To the faithful, this glorious building is known as the Sheikh Zayed Mosque, although its full title is Sheikh Zayed bin Sultan Al Nahyan, since it was named after the founder of the United Arab Emirates. He was the man who initiated this masterpiece in marble, the very whiteness of which is a symbol of peace to Muslims.

The blindingly white façade reminds onlookers of the Taj Mahal in India and the ethereal magnificence of the mosque is emphasized by the use of translucent stone from the finest quarries in Italy, Greece, India and China.

A total of 115,119 square metres of the stone was used for the four minarets and the outer facade alone. The Emirates' founding father ordered the same material for his burial place close by, a modest mausoleum where he was buried aged 86 on November 2, 2004, three years before the vast house of prayer was officially inaugurated.

When he laid the foundation stone in 1996, Sheikh Zayed marked the start of the construction of the largest mosque in the UAE and the third most sizeable in the Islamic world. The muezzin summons worshippers to a complex spread over 22,412 square metres. It can accommodate a total of 30,000 people, 23,000 of them within the cavernous main prayer hall which is also made of marble.

Only the best is good enough for a mosque of such enormous proportions. The building contains the world's largest hand-woven Persian carpet. A small army of 1,200 weavers toiled for 18 months to complete this floor covering, using up 38 tonnes of wool in the process. They used 2.2 billion knots in its creation and the carpet covers an area of 5,625 square metres.

















Tuesday, July 10, 2012

Wimbo wa leo BOB JUNIOR-Nichum

MPAMBANO WA SOKA WABUNGE WA SIMBA NA YANGA KATIKA PICHA


Timu za wabunge wa Simba na Yanga wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya mpambano

Waamuzi wa mpambano huo wakipiga picha ya pamoja na manahodha wa timu zote mbili

Wabunge wa Simba katika Dua kabla ya mtanange kuanza


Wabunge wa Yanga nao wakipiga dua kabla ya mtanange kurindima

Mashabiki wakiwahi mpambano

Mtanange umeanza


Mwamuzi wa mtanange huo Athuman Kazi akifuatilia kwa karibu kuhakikisha haki inatendeka


Mh Zitto Kabwe wa Simba akitoa pasi murua kama Iniesta vile!


Mbunge wa Simba akitiririka na kabumbu















Katibu uenezi wa CCM Nape Nnauye akifuatilia mpambano wa Wabunge wa Simba na wale wa Yanga katika dimba kuu la Taifa jijini Dar es salaam


Benchi la ufundi la Wabunge wa Simba wakifuatilia mpambano


Benchi la ufundi la Wabunge wa Yanga wakiongozwa na kocha mkuu mpya wa Yanga


Mbunge wa Yanga akiwa hoi bin taaban


Mbunge wa Yanga akijaribu kuihadaa ngome ya wabunge wa Simba


Hali tete mlinda mlango wa wabunge wa Yanga baada ya kichapo kwa njia ya matuta 3-2


Wera weraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!! wabunge wa Simba hatimae waliwachapa wa Yanga katika matuta baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 0-0




Nani kama Simbaaaa woyooooo woyooooooooo


Hakunagaa zaidi ya Simba hakunagaa, hakunaaa hakunaaaa hakunaaaaaaaaaa!!!


Weraaaaa tupishe tupiteeee, tupisheeeee tupishe tupiteeeeeeee..Wabunge wa Simba wakiongozwa na Mh Zitto Kabwe na William Ngeleja kuserebuka baada ya kuwaangushia kisago wenzao wa Yanga kwa mikwaju ya penati 3-2
Mpambano Wabunge SIMBA Vs YANGA

Katika mtanange huo baada ya dakika 90 na kipyenga cha mwamuzi Athumani kazi kupulizwa matokeo yalikuwa ni 0-0. Mpambano huo wa kufurahisha na kusisimua uliopigwa katika dimba kuu la Taifa jijini Dar es salaam ikiwa ni katika mchezo wa hisani kukusanya pesa kuchangia ujenzi wa mabweni kwa shule za sekondari nchini!

shukrani za pekee kwa waandaaji wa tamasha hilo ambalo pia liliwakutanisha wasanii wa Bongo flava na Bongo Movie hali kadhalika mpambano wa Masumbwi kati ya wasanii maarufu nchini na wenye kutengeneza vichwa vya habari katika redio na magazeti mbalimbali hapa nchini, ni Wema Sepetu na Jaquiline Wolper ambapo katika mpambano mpambano huo uliodumu kwa raundi mbili matokeo yalikuwa ni droo hakukuwa na mshindi.

KEITA AONDOKA BARCELONA NA "NDOO"14 HUKU TITO AKIMRITHI PEP GUARDIOLA


Seydou Keita

kiungo wa Mali Seydou Keita amekihama klabu ya Barcelona baada ya kukipiga kwa miaka minne.
Katika muda huo wa miaka minne, Keita aliisaidia Barcelona kuzoa jumla ya vikombe 14.
Wakati wakithibitisha kuondoka kwa mwamba huyo, Barca walimshukuru Seydou Keita kwa juhudi zake za kuiletea klabu hiyo ya Uhispania mafanikio na vile vile wakamtakia kila lakheri anakokwenda.

Keita na Sanchez wakiwa wamebeba kombe wakikipiga Barcelona

Kwa wakati huu kuna fununu kwamba mchezaji huyo wa Mali huenda anahamia klabu moja ya Uchina, Dalian Aerbin
Ikiwa hatiamae ataishia China basi Keita hatakuwa mchezaji wa kwanza kutoka bara la Afrika kufanya hivyo.
Majuzi nahodha wa timu ya Ivory Coast Didier Drogba aliwafuata Frederic Kanoute na Yakubu Aiyegbeni wa Nigeria kujiunga na timu za ligi kuu ya China.
Keita, mwenye umri wa 32, alijiunga na Barcelona mwaka 2008 kutoka Sevilla akiwa ni mchezaji wa kwanza kabisa ambaye Pep Guardiola alimsajili mara tu alipokwaa uongozi wa Barca.
Kabla ya hapo mchezaji huyo alikuwa Olympic Marseille, Lorient na Lens zote za Ufaransa na ndio baadaye akahima Seville ya Uhispania.
Keita amehama baada ya Guardiola kuondoka kama Meneja wa Barcelona na mahali pake kuchukuliwa na aliyekuwa naibu wake Tito Vilanova

Tito Vilanova kocha alierithi mikoba ya Pep Guardiola


Tito Vilanova akiwa na Pep Guardiola