Wednesday, July 25, 2012

WANAOONGOZA KWA KUTIKISA NYAVU KATIKA MICHUANO YA KAGAME 2012


Etikiama Taddy, Mshambuliaji wa AS Vita anaongoza mpaka sasa kwa kutikisa nyavu katika michuano ya Kagame ana mabao 6

ORODHA KAMILI YA WALIOTIKISA NYAVU MPAKA SASA

Taddy Etikiama (AS Vita)       6

Said Bahanuzi (Yanga SC)    5

Hamisi Kiiza (Yanga SC)       4

John Bocco (Azam FC)         4

Suleiman Ndikumana (APR) 3

Abdallah Juma (Simba SC)   2

Leonel St Preus (APR)         2           
 
Didier Kavumbagu (Atletico) 2

Feni Ali (URA)                       2

Robert Ssentongo (URA)      2

MRISHO NGASSA ANATAKA KURUDI YANGA, AIFANYIA AZAM MGOMO BARIDI


Mrisho Ngassa akiwa katika Benchi la Azam katika mechi ya robo fainali kombe la Kagame kati ya Azam na Simba

KOCHA wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall amesema hamtumii Mrisho Khalfan Ngassa kwa sasa, kwa sababu haonyeshi dalili za kutaka kucheza.

“Hana jitihada zozote, hajitumi, hana hamu ya kucheza, siwezi kumchezesha,”alisema Stewart mapema tu, kabla ya mechi ya Robo Fainali dhidi ya Simba SC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Pamoja na kucheza bila Ngassa, Azam imeshinda 3-1 na kuingia Nusu Fainali, ambako itamenyana na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Kuna tetesi kwamba, Ngassa yupo kwenye mgomo baridi kushinikiza uhamisho wa kurejea Yanga, lakini habari ambazo  zimepatikana kutoka ndani ya Azam, zinasema kwamba, klabu hiyo itaendelea kuishi naye hivyo hivyo ‘kimakunyanzi’ hadi amalize mkataba wake msimu ujao.

KOMBE LA KAGAME, MNYAMA ALAMBA LAMBALAMBA YENYE SUMU KALI UWANJA WA TAIFA


Wachezaji wa Azam wakishangilia bao lililotupiwa na John Bocco "Adebayor/Boko Haramu" aliekaa chini.

Vilabu vya Azam na Vita vimefanikiwa kuingia nusu fainali ya michuano ya soka ya Cecafa.

John Bocco alikuwa shujaa pale timu yake ya Azam ya Tanzania, ilipofanikiwa kuingia nusu fainali ya mashindano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati baada ya kuwafunga mabingwa wa Tanzania, Simba, mabao 3-1.

Katika mechi hiyo ya robo fainali iliyochezwa Jumanne mjini Dar es Salaam, Bocco alitupiamo kambanio mabao yote dakika ya 17, 46 na 73, wakati bao la kufutia machozi la Simba likitupiwa na Shomari Kapombe dakika ya 53.

Timu hiyo sasa itapambana na Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwenye nusu fainali itakayochezwa Alhamisi.

Vita Club walifuzu baada ya kushinda kwa mambao 2-1 dhidi ya Atletico ya Burundi kwenye mechi nyingine iliyochezwa Jumanne. Mabao ya Vita yalifungwa na Taddy Etekiama na Basilua Makola wakati bao la Atletico lilifungwa na Pierre Kwizera.

Matokeo hayo yamekuwa ya kushangaza hasa ikizingatiwa kuwa Simba ni timu kongwe ambayo imeshinda kombe hili la ukanda mara sita.

Nayo Azam, iliyoanzishwa mwaka 2007, haya ni mashindano yao ya kwanza kimataifa tangu timu ianzishwe na ilipata tiketi ya kushiriki baada ya kumaliza ligi msimu uliopita ikiwa nafasi ya pili.

Mafanikio ya Azam yanakuja baada ya kusajili wachezaji kutoka Ivory Coast na Kenya na kumwajiri kocha kutoka Uingereza.

Mechi zote za nusu fainali zitachezwa Alhamisi kufuatia kuondoshwa Simba kwenye mashindano.

Timu nyingine zitakazokutana kwenye hatua hiyo ni bingwa mtetezi Yanga ya Tanzania na APR ya Rwanda.

Fainali itachezwa Jumamosi na bingwa atapewa zawadi ya dola 30,000 na mshindi wa pili 20,000, na atakayemaliza katika nafasi ya tatu ataondoka na kitita cha dola 10,000.

Katika mchezo wa huo, kikosi cha Azam kilikuwa; Deo Munishi, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Michael Balou/Ramadhan Chombo, Kipre Herman Tcheche/George Odhiambo ‘Blackberry’, Salum Abubakar, John Bocco, Ibrahim Mwaipopo na Khamis Mcha ‘Vialli’/Jabir Aziz.

Simba SC; Juma Kaseja, Haruna Shamte, Shomary Kapombe, Lino Masombo, Juma Nyosso, Mussa Mudde, Uhuru Suleiman/Kiggi Makassy, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Jonas Mkude/Amri Kiemba.

Mrisho Ngassa akiwa ubaoni


Kocha wa Simba Milovan Cirkovic akiwa amelowana kwa kichapo.


Kocha wa Yanga Tom Saintfiet ,Felix Minziro naMfaume athumani wakifuatilia mtanange kati ya Simba na Azam


Benchi la Simba haliamini kilichotokea katika mechi yao dhidi ya Azam

Mashabiki wa Azam F.C


Mashabiki wa Simba S.C


John Bocco "Boko Haramu" akijaribu kuiponyoka ngome ya Simba


Felix Sunzu akiwa amerudi nyuma kusaidia kuokoa jahazi wakati mpira wa kona ukielekezwa lango la Simba


Kipre Cheche wa Azam akitiririka kuelekea kumsalimu Juma Kaseja


John Bocco "Boko Haram" akishangilia bao la pili


John Bocco 'Boko Haram" na Abubakar Saalum 'Sure Boy' wakishangilia kwa mtindo wa aina yake.

Nazi hii ilivunjwa na kamati ya ufundi ya Simba S.C lakini haikufua dafu!


Kikosi cha Simba




Kikosi Cha Azam F.C

Tuesday, July 24, 2012

ROBO FAINALI KAGAME CUP,HATUMWI MTOTO SOKONI SIMBA Vs AZAM


'Mwali" wa Kagame ambapo imefikia hatua ya robo fainali

Mabingwa wa Soka nchini, Simba na mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC leo zina fursa kupalilia kampeni ya kuongeza mataji kwenye makabati yao zitakapokutana katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya Kombe la Kagame kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Mbali na mechi hiyo inayotarajia kuwa na ushindani mkubwa, pia kutakuwa na mchezo mwingine wa robo fainali utakaozikitanisha Atletico ya Burundi dhidi ya Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mchezowa Simba na Azam ni kama fainali kwani zimekuwa zikikamiana kila zinapokutana, ambapo mara ya mwisho zilikutana fainali ya Kombe la Urafiki na Simba kushindwa kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya 2-2.
Lakini kabla ya hapo, Simba ilinyukwa mabao 2-0 kwenye michuano ya Kombe la Mpinduzi, kabla ya Wekundu hao wa Msimbazi kulipa kisasi kwa ushindi wa mabao 2-0 katika mechi ya marudiano ya Ligi Kuu.
Mechi ya leo inazikutanisha kwa mara ya nne, ambapo zitakutana tena katika mchezo wa Ngao ya Jamii mwishoni mwa mwezi ujao kama ishara ya mwanzo wa msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.
Azam inashiriki michuano ya Kombe la Kagame kwa mara ya kwanza na imepania kutaka kuweka rekodi ya kutwaa taji lingine baada ya lile la Mapinduzi.
Kocha Stewart Hall anajivunia kikosi chake kilichokuwa Kundi C la michuano hiyo pamoja na Mafunzo na Tusker ya Kenya.
Atamtegemea zaidi kipa mpya, Deogratius Munishi 'Dida'  ndiye atakayesimama langoni, huku Waziri Salum akirejea uwanjani kucheza beki wa kushoto na mchezaji bora nchini, Aggrey Morris atasimama katikati akishirikiana na Joseph Owino na Erasto Nyoni akicheza beki wa kulia.
Viungo watatu watakuwa ni Kipre Bolou, Salum Abubakar na Ramadhan Chombo Redondo, wakati mfungaji bora wa klabu John Bocco atasimama katika ushambuliaji akishirikiana na Kipre Tchetche na Mrisho Ngasa.
Kwa upande wa Simba ambayo makali yake katika safu ya ushambuliaji bado hayajaonekana tangu kuondoka kwa Emmanuel Okwi, itaendelea kumtegemea Felix Sunzu kupachika mabao.
Kocha Circovic Milovan, amekiri wazi kukosekana Okwi na kufariki kwa Patrick Mafisango, kumeacha pengo kubwa kwenye kikosi chake.
Simba ilianza vibaya michuano hiyo kwa kunyukwa 2-0 na URA ya Uganda kalba ya kuichapa Ports ya Djibouti mabao 3-1 na kulazimishwa sare ya 1-1 na Vita Club ya Kongo.
Majeruhi Shomari Kapombe na Amir Maftah wanampa presha Milovan na itabidi atumie muungano wa Haruna Shamte na Kiggi Makasi na nafasi ya Okwi akiiziba Abdallah Juma ambaye ni kinda aliyemfunika Felix Sunzu kutokana na kutumia vema nafasi hiyo.
"Kukosekana kwa ubunifu baada ya Okwi kuondoka ni ngumu kwetu, lakini Juma Abdallah anajitahidi kucheza vizuri ingawa bado haijaimudu vizuri.
"Nahitaji harakati mshambuliaji mmoja muhimu, nina uhakika wa asilimia 75 Okwi hawezi kurudi tena Simba," alisema Milovan.
Mechi nyingine itanayotarajia kuwa kali itazikutanisha Atletico na Vita Club ambazo zimeonyesha uwezo na kucheza kwa ufundi tangu kuanza kwa michuano hii.
Atletico imetinga robo fainali bila ya nyavu zake kutikiswa baada ya kuinyuka Yanga mabao 2-0 na kisha kwenda sare ya bila kufungana na APR, kabla ya kuinyuka Wau Salaam ya Sudan ya Kusini mabao 5-0 huku Vita ambayo inashiriki michuano hii kama wageni waalikwa walianza harakati zao kwa kuinyuka Ports ya Djibouti mabao 7-0 na kujikuta ikinyukwa mabao 3-1 na URA ya Uganda na kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Simba mwishoni mwa  wiki.

Friday, July 20, 2012

DENNIS RODMAN AKUTANA NA BABA YAKE PHILANDER RODMAN BAADA YA NYUNDO 42


Dennis Rodman

Mchezaji wa zamani na maarufu wa muda wote wa mchezo wa Mpira wa Kikapu(Basketball) Dennis Rodman hatimae amekutana na baba yake mzazi aitwae Philander Rodman baada ya baba huyo kumuacha mama yake Dennis miaka 48 iliyopita.

Dennis Rodman aliewahi kuzichezea timu za Pistons,Spurs,Bulls,Lakers na Mavericks hakuonana na baba yake kwa miaka 42 na hivi karibuni kukubali kukutana na baba yake huko Manila nchini Phillipines wakati wa mechi za Basketball.

Philander Rodman Jr ni baba wa watoto 29 kwa mama 16 alisema alipatwa na mshangao na furaha pale mwanae alipokubali kukutana nae huko Manila jumatano ya tarehe 19 july 2012, baada ya jaribio lake kushindikana mwaka 2006 siku ya michezo kama hiyo huko Manila,Phillipines.

Dennis Rodman akielezea kwa hisia na uchungu kuwa alikuwa na wakati mgumu katika maisha yake kwa kulelewa na mama tu na kukosa mfano wa kufuata kutoka kwa mzazi wa kiume(baba) ndani ya nyumba, 

Philander Rodman Jr (Baba mzazi wa Dennis Rodman)

Yafuatayo ni maneno ya Rodman akielezea hisia zake;
 "I never really knew my father, Philander Rodman. He was in the Air Force in New Jersey, where I was born, and when I was three we packed up and came back to Dallas where my mother is from. We did this when my father stopped coming home.
My father isn't part of my life. I haven't seen him in more than thirty years, so what is there to miss? I just look at it like this: Some man brought me into this world. That doesn't mean I have a father; I don't. I could say, 'This is my father. This is my dad,' but that doesn't sound right to me. I grew up with my mother and two younger sisters, Debra and Kim. There wasn't a male role model in my life until I got to college and started getting my [act] together."

Baba nae alikuwa na haya ya kusema;
''I've been trying to meet him for years. And then last night, boom, I met him. I was really, really happy and very surprised,'' he told The Associated Press.
''I really, really felt good,'' he said. ''It's the beginning of something new.''


Baba na Mwana walipokutana baada ya miaka a.k.a Nyundo 42

Mzee ulinitosa au?.........

Rodman akisaini vitabu vya kumbukumbu kwa mashabiki wake huko Manila nchini Phillipines ambako ndiko alipokutana na baba yake 19 july.


Rodman enzi zake akikipiga na Pistons


Rodman enzi zake akikipiga na Chicago Bulls



Hapa akikipiga na Spurs


Hapa akikipiga L.A Lakers



Enzi akikipiga na Dallas Mavericks


Rodman katika swaga na mbabe wa mieleka maarufu Hulk Hogan..na alama za Freemasons


Haya ..Hii alama inasemekana ni ya Freemasons!

Thursday, July 19, 2012

USAFIRI MPYA KUKABILI FOLENI MIJINI

Katika kupambana na tatizo la usafiri na pia kukabiliana na foleni zisizokwisha maeneo ya mijini hatimae kumeibuka usafiri wa aina yake ambao unajulikana kama "Burger" Aina hii ya usafiri haitofautiani sana na ile ya Mshikaki lakini hii inabeba watu wengi zaidi kwa kutumia chombo kilekile cha usafiri....haya sasa wakazi wa pale Dar es salaam usafiri huu utawafaa sanaa!!

WATANZANIA WAENDELEA KUPOTEZA MAISHA KWA AJALI ZA MELI, HII TENA


WATU 60 wanahofiwa kufa maji na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya boti iliyokuwa imebeba abiria wanaokadiriwa kufikia 250 ikitokea Dar es Salaam kwenda Unguja, Zanzibar kuzama baharini.Hii ni ajali ya pili mbaya kutokea katika kipindi cha miezi 10 tangu ilipotokea nyingine ya Meli ya Mv Spice Islander ambayo inakadiriwa kuwa watu wapatao 200 walifariki dunia.Boti hiyo iliyoondoka jana Dar es Salaam majira ya saa 6:00 mchana na kutarajiwa kufika Bandari ya Malindi, Zanzibar saa 9:30 jioni, ilizama eneo la Pungume karibu kilomita 48 kutoka Bandari ya Zanzibar.
Inaelezwa kuwa, ilianza kuzama saa 7:30 mchana kutokana na kupigwa na mawimbi mazito ya bahari.

Hata hivyo, Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu wa Zanzibar, Hamad Masoud Hamad alithibitisha vifo vya watu 12 hadi vilivyoripotiwa ilipotimu saa 12:30 jioni jana wakati kazi ya uokoaji ikiwa inaendelea.

Baadaye saa 1:00 Ofisa Habari na Mawasiliano wa Wizara hiyo, Nafisa Madai aliwaambia waandishi wa habari kuwa idadi hiyo ilikuwa imeongezeka hadi kufikia 24 na majeruhi walikuwa 145.Madai alisema wakati boti hiyo inaondoka Dar es Salaam, ilikuwa na abiria 250 wakiwamo watoto 31 na wafanyakazi tisa.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Said Shaaban akizungumzia ajali ya boti hiyo ya Mv Skad, inayomilikiwa na Kampuni ya Meli Seagull alisema: “Vikosi vya uokoaji tayari vinaelekea katika eneo hilo ili kusaidia majeruhi na kufuatilia yaliyotokea.”

Maofisa kadhaa wa Serikali wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi walifika Bandari ya Malindi na Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Zanzibar, Hamad Masoud Hamad aliongoza msafara wa viongozi wengine kwenda katika eneo la tukio.

Awali, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alisema kuwa, hadi alipopata taarifa, watu waliokuwa wamefariki dunia ni saba na 124 ndiyo waliokuwa wameokolewa. Alisema meli hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 300 na waliosafiri siku ya tukio hawazidi 250.

Awali, taarifa zilieleza kuwa watu 10 waliokolewa na maiti zaidi ya 60 zimenasa katika boti hiyo na kuvifanya vikosi vya uokoaji vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi na KMKM kupata wakati mgumu kwenye zoezi la uokoaji.Kazi ya kuokoa maisha ya watu waliozama kwenye boti hiyo na kuopoa maiti ilifanywa kwa kutumia boti nne zikiwamo za Serikali na zile zinazomilikiwa na Kampuni ya Azam Marine.

Hata hivyo, ilielezwa kwamba boti za polisi zilichelewa kwenda katika eneo la tukio kutokana na kukosekana kwa mafuta.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kufika bandarini, Balozi Seif aliwataka wananchi kutulia na kusubiri wakiwa nyumbani wakati Serikali ikifanya juhudi za uokoaji.

Shughuli nyingi za usafiri zilivurugika kutokana na tukio hilo na Meli ya Mv Sea Bus ililazimika kufuta safari zake kupisha kazi hiyo ya uokoaji.
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imesema inafuatilia tukio hilo kwa karibu ili kubaini chanzo.
Ofisa Uhusiano wa Sumatra, David Mziray alisema jana muda mfupi baada ya ajali hiyo kuwa, wanawasiliana na Kituo cha Utafutaji na Uokoaji Majini (MRCC), ili kupata taarifa kamili kabla ya kuujulisha umma.


Baadhi ya abiria wakisubiri uokozi


Waokoaji wakiwa katika boti ya Kilimanjaro wakiopoa maiti ya mzungu


Muokoaji akiwa na maiti



Meli ya MV Skagit ikiwa imezama katika bahari ya Chumbe


Abiria akichomolewa baharini na kikosi cha uokoaji




Jopo la madaktari likitoa huduma ya kwanza kwa majeruhi wa ajali ya meli katika bahari ya Chumbi


Umati wa wananchi wakiwa katika bandari ya Malindi wakifuatilia tukio la ajali ya meli ya Mv Seagull(Skagit)







"Najuuuuta kuifahamu Tanzania".....Inaelekea ndivyo mzungu huyu anavyofikiria


Boti ya KMKM ikiwa katika uokozi


Maiti ikitolewa baharini


Majeruhi akiwa amebebwa tayari kwa kupatiwa huduma ya kwanza