Monday, September 10, 2012

SIMU YA MKONONI NI HATARI KWA MAISHA YAKO,TAFADHALI ITUMIE KISTAARABU

Fun & Info @ Keralites.net
Hawa wanapata kahawa jioni lakini maongezi hakuna kila mtu bizee na kisimu chake


Fun & Info @ Keralites.net
Wapo Dinner lakini kila mtu kwenye simu jamani kunaniii simuni?

Fun & Info @ Keralites.net
Wamekaa wanamsubiri mgeni hotelini lakini hakuna stori ni simu tuu..khaaa!!!??

Fun & Info @ Keralites.net
Wamekutana chakula cha usiku"Dinner" mhhh biiizee na simu no stori hapa

Fun & Info @ Keralites.net
Marafiki wapo Ufukweni "Beach" lakini hakuna stori, hakuna kucheza wala kuogelea ni simu tuuu..mweeee!!!

Fun & Info @ Keralites.net
Haya sasa mtu yupo uwanjani hafuatilii tena mechi ni simu tuuu bhaaaah!!

Fun & Info @ Keralites.net
Hawa ni wapenzi wametoana "OUT" badala ya kubadilishana mawazo kudumisha penzi lao
kazi ni moja simuuu heeee!!

Fun & Info @ Keralites.net
Misere na ndinga kitaani No stori ni simu tu kuchata kwa kwenda mbele kaazi kwelikweli

Fun & Info @ Keralites.net
Shughuli sasa hii hapa, Wanapoendesha magari ni simu tuuu vimeseji mwisho wa siku wanasababisha ajali...jamani mhhh ukistaajab ya Khalid Utayaona ya Firauni.

Fun & Info @ Keralites.net
Achana na waendesha magari shughuli pia imo kwa watembeaji kwa miguu na waendesha baiskeli, umeonaaa ni simu tuuu kudadadadekii utakoma mwenyewe ni kikumbo tu ukizubaazubaa!!

OBAMA ABEBWA JUU JUU NA MUUZA PIZZA


Rais Obama akiwa amenyanyuliwa juu na Scott Van Duzer

Mmiliki wa Mgahawa maarufu jijini Florida, Marekani Scott Van Duzer alitoa kali ya mwaka alipotembelewa na Rais Obama katika mgahawa wake na kumnyanyua juu kama ishara ya furaha aliyikuwa nayo kwa ujio wa Obama pale mgahawani.

Rais Obama akitumia usafiri wa basi katika ziara ya siku mbili jijini Florida ikiwa ni sehemu za kampeni za uchaguzi utakaofanyika mwezi Novemba, alitembelea Mgahawa maarufu jijini Florida unaotambulika vilivyo kwa kuuza Pizza baaab kubwa unaojulikana kama Big Apple Pizza & Pasta Restaurant unaomilikiwa na Scott Van Duzer.

"Scott, what's going on, man," alisikika rais Obama akisalimiana na Van Duzer mara tu ya kuingia mgahawani. "Let me tell you, you are like the biggest pizza shop owner I've ever seen."  Obama aliendelea kumwaagia misifa Van Duzer ambae alimpigia kura rais Obama mwaka 2008 na ameahidi kumpigia tena kura mwezi Novemba.


Woooowww jamani rahaaa sio rahaaaa...Van Duzer akimkumbatia President Obama na kumnyanyua juu juu katika mgahawa anaoumiliki wa Big Apple Pizza & Pasta Restaurant jijini Florida,Marekani.

RICH MAVOKO- Marry ME


MAKAMO WA RAIS AHUKUMIWA KIFO

TariQ Al Hashemi
 
Mahakama nchini Iraq imepitisha hukumu ya kifo kwa makamu wa rais, Tariq al-Hashemi, baada ya kumkuta na hatia kwa kuongoza makundi ya kuuwa watu, yaliyowalenga Washia na askari wa usalama.
Makamo wa rais, wa madhehebu ya Sunni, hakuweko mahakamani wakati wa hukumu hiyo kwani alishaikimbia Iraq awali mwaka huu, akiwa sasa anaishi Uturuki.

Kesi hiyo imezusha msukosuko wa kisiasa katika serikali ya Iraq, iliyogawa madaraka kati ya Wa-Sunni, wa-Shia na WaKurd.

Bwana al-Hashemi amemshutumu Waziri Mkuu Nuri al-Maliki ambaye ni M-Shia, kuwa anawasaka wapinzani wake wa kisiasa wa madhehebu ya Sunni, lakini serikali inasisitiza kuwa kesi hiyo inafuata misingi ya sheria tu.


Hukumu hii ya mahakama imekuja huku watu wasiopungua 45 wakiwa wameuawa katika mfululizo wa mashambulizi 24 nchini Iraq. Siku ya Jumapili mashambulizi kadhaa yalishuhudiwa katika maeneo ya Tuz Khurmatu, Baquba, Basra na Samarra.

Wanajeshi 11 waliuawa kaskazini mwa Baghdad, huku katika mji wa Amara watu 14 wakiuawa na wengine 60 kujeruhiwa katika mashambulio mawili ya mabomu ya kutegwa katika gari.

Maafisa polisi saba pia waliuawa kwa bomu katika mji wa kaskazini wa Kirkuk, wakati wanajeshi kumi nao wakiuawa katika kambi ya jeshi ya Dujail kaskazini mwa Baghdad. Na katika eneo la Nasiriya kusini kulitokea mlipuko wa bomu nje ya ubalozi wa Ufaransa ulioua mtu mmoja huku serikali ya Ufaransa ikilaani shambulio hilo.

Hashimu alikuwa ni mwanasiasa wa juu sana aliyeheshimika kutoka dhehemu la Sunni katika serikali yenye Wa-Shia wengi hadi alipofunguliwa mashitaka mwezi December mwaka 2011 wakati alipotoroka nchini humo.

Wanasiasa wengine wa Ki-Sunni walimkataa waziri mkuu wa Ki-Shia Nouri al-Maliki aliyetoa amri ya kukamatwa kwa Bwana Hashemi, wakimuita kama dikteta na kumshutumu kwa kuendeleza chokochoko zinazoweza kuiingiza nchi hiyo katika vita vya kikabila kwa mara nyingine.

Waandishi wa habari wanasema muungano wa serikali kati ya Wa-Sunni, Wa-Shia na wale wa makabila mengine inaonkena kuwa hatarini tokea wakati huo.

Wapiganaji wa Ki-Sunni wanaohusishwa na kundi la kigaidi la al-Qaeda wamekuwa wakishutumiwa kwa vurugu za hivi karibuni nchini Iraq.

Friday, September 7, 2012

NYAAAUUUU...SIMBA YARARURIWA NA SOFAPAKA


Akuffor wa Simba akijaribu kufunga bila mafanikio

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba S.C wamejikuta wakipelekeshwa puta na kupata kipigo cha fedheha cha mabao 3-0 kutoka kwa Sofapaka inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya katika mechi yao ya kimataifa ya kirafiki kwenye dimba kuu la Taifa jijini Dar es Salaam leo.
Sofapaka walipata bao la kuongoza katika dakika ya 18 kwa njia ya penati baada ya beki mpya wa kimataifa wa Simba, raia wa Mali
Komalbil Keita kufanya madhambi  ndani ya eneo la boksi na mshambualiaji wa zamani wa Yanga, John Baraza akatupia mpira wavuni kwa shuti kali lililomshinda kipa Juma Kaseja.

Safu ya mabeki wa Simba iliendelea kuwapa hofu mashabiki wa klabu yao baada ya Pascal Ochieng na keita kujichanganya na kuwapa wageni bao la pili katika dakika ya 57 kupitia tena kwa Baraza.


Kikosi cha Simba kinachonolewa na Mserbia Milovan Cirkovic kiliwasononesha mashabiki wao waliofika  kuwashangilia baada ya mabeki wake kuruhusu bao la tatu katika dakika ya 66 kwa shuti la Joseph Nyaga aliyemalizia vyema kazi nzuri iliyofanywa na mchezaji wa zamani wa klabu ya Azam, Osborne Monday.

Safu ya kiungo iliyotarajiwa kuwa 'kali' ya Salim Kinje na Mwinyi Kazimoto ilishindwa kuonyesha makali mbele ya Sofapaka, kama ilivyokuwa kwa viungo-washambuliaji Haruna Moshi 'Boban', Mrisho Ngassa aliyetua kwa kishindo katika timu hiyo akitokea Azam na mshambuliaji wao Christopher Edward aliyeibuka kinara wa kupachika mabao katika michuano iliyomalizika hivi karibuni ya Ligi ya Super8 na kuisaidia Simba B kutwaa ubingwa.

Awali, katika dakika ya 35, Simba walipata pigo baada ya Straika wao tegemeo kwa sasa, Mghana Akuffor kuumia vibaya baada ya kuchezewa faulo na Antony Kimani.


Alianguka uwanjani na kushindwa kupumua kwa muda, lakini alipozinduka alitaka kuendelea kucheza kabla daktari wa Simba, Cosmas Kapinga kumkataza na hivyo kutolewa uwanjani.


Kipigo cha leo kimemuacha kocha Milovan katika wakati mgumu wa kukiboresha kikosi chake kwani zimebaki siku chache kabla ya kushuka dimbani kuvaana na Azam wiki ijayo katika mechi ya kuwania Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Kabla ya kuivaa Sofapaka leo, Milovan aliahidi soka safi na kusema kwamba mechi hiyo ndio kipimo chao kabla ya kucheza dhidi ya Azam kwani wameshajifua vya kutosha, hasa walipokuwa katika kambi yao jijini Arusha.


Licha ya ubutu wa safu yao ya ushambuliaji, rekodi ya mabeki wa Simba pia haionyeshi kuwa wako 'ngangari' vya kutosha tangu aondoke Kevin Yondan aliyejiunga na Yanga, kwani penati waliyoruhusu leo dhidi ya Sofapaka ni ya pili katika mechi zao nne za kirafiki za hivi karibuni.


Penati nyingine ilishasababishwa na Pascal Ochieng. Mabeki hao vilevile wana rekodi ya kujifunga mara mbili katika mechi hizo nne za kujipima nguvu, mabeki hao ni mabeki Juma Nyosso na Keita.




Mshambuliaji wa Simba Akuffor akitolewa baada ya kuumia

Christopher Edward wa Simba akijaribu kumhadaa mlinzi wa Sofapaka Antony Kimani aliemuumiza Akuffor

Rekodi katika mechi hizo zinaonyesha kuwa beki Ochieng aliyeondoka AFC Leopards ya Kenya kutokana na kukosa namba katika kikosi cha kwanza, alisababisha penalti moja wakati Keita ambaye ametua kutoka Mali, amejifunga goli moja na kusababisha penati moja huku Nyosso naye akijifunga moja katika mechi hizo nne ambazo Simba waliwafunga JKT Oljoro 2-1, wakawabwaga Mathare United 2-1 pia na kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Sony Sugar ya Kenya.

Akuffor ndiye ambaye ameonekana kuwa mchezaji 'jembe' baada ya kufunga katika mechi zote tatu za kwanza kabla ya jana kuumia.

VIKOSI
Simba: Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Amir Maftah, Pascal Ochieng, Komalbil Keita, Mwinyi Kazimoto, Salim Kinje, Haruna Moshi ‘Boban’, Edward Christopher, Daniel Auffor na Mrisho Ngassa.

Sofapaka: Duncan Ochieng, Antony Kimani, James Situma, Edgar Ochieng, George Owino, Collins Okoti, Osborne Monday, Humphrey Mieno, Kago Danson, Joseph Nyaga na John Baraza.

Monday, September 3, 2012

ROBIN VAN PERSIE APIGA "HAT TRICK"

Robin Van Persie Robin Van Persie of Manchester United celebrates the winning goal during the Barclays Premier League match between Southampton and Manchestrer United at St Mary's Stadium on September 2, 2012 in Southampton, England.
Van Persie
 
Robin van Persie amegeuka kuwa kipenzi cha mashabiki wa klabu yake mpya kwa kuiokoa Man.United alipofunga matatu mwenyewe kumuondolea maradhi ya moyo Sir Alex Ferguson kunako mechi yake ya 1,000th akiiongoza Manchester United kama meneja.

Mdachi huyo alitanguliza la kichwa kutokana na kona iliyochongwa na Nani katika mda wa ziada kuokoa jahazi.

Southampton ilipata bao la kuongoza kupitia Rickie Lambert kabla ya Morgan Schneiderlin kupata la pili pia la kichwa katikati ya magoli ya Van Persie ya kusawazisha.

Uhodari wa Van Persie uliwekwa kwenya mizani alipokosa mkwaju wa peneti mnamo dakika 88 wakati United ikidorora 2-1.

Kwa menejawa Southampton Nigel Adkins dakika za majeruhi zilikua kama mwaka wenye machungu kutokana na jinsi vijana wake walivyoweza kuidhibiti United na mabao ya haraka haraka mawili bila shaka yalimuumiza.

Kwa mashabiki wa United, matokeo haya ni sehemu ya malipo ya kitita cha milioni 24 za pauni za Uingereza zilizomleta United kutoka Arsenal.
Robin Van Persie Robin Van Persie of Manchester United scores the winning goal during the Barclays Premier League match between Southampton and Manchestrer United at St Mary's Stadium on September 2, 2012 in Southampton, England.
Van Persie akitupia goli la kwanza
Robin Van Persie Robin Van Persie of Manchester United scores his second goal during the Barclays Premier League match between Southampton and Manchestrer United at St Mary's Stadium on September 2, 2012 in Southampton, England.
Van Persie akitupia goli la pili
Robin Van Persie Robin Van Persie of Manchester United celebrates the winning goal during the Barclays Premier League match between Southampton and Manchestrer United at St Mary's Stadium on September 2, 2012 in Southampton, England.
Van Persie akishangilia bao
Robin Van Persie Robin Van Persie of Manchester United scores the winning goal during the Barclays Premier League match between Southampton and Manchestrer United at St Mary's Stadium on September 2, 2012 in Southampton, England.
Mpira uliopigwa na Van Persie ukitinga wavuni kuandika goli la tatu "Hat Trick" na la mwisho la Man United
Southampton vs Man United

ARSENAL YAANZA LIGI YAIDUNGUA LIVERPOOL 2 KAVU


Kocha wa Arsenal Arsene Wenger akizungumza na waandishi wa habari baada ya mechi.

Arsenal imepata ushindi wake wa kwanza katika ligi ya Premier ya nchini Uingereza msimu huu baada ya kuidungua Liverpool 2-0 nyumbani kwao.
Hii ndio mara ya kwanza kabisa kwa Liverpool kuanza msimu kwa kichapo cha mabao 2-0 katika uwanja wao katika kipindi cha miaka 50,Magoli yote mawili ya Arsenal yalitupia kambani na wachezaji wapya Santi Cazorla na Lukas Podolski .

Mshambuliaji wa Ujerumani Podolski ndiye alikuwa wa kwanza kuipatia Arsenal bao katika dakika ya 31. Na katika dakika ya 68 Cazorla alipeleka kilio na kubadili ubao wa matangazo kuwa 2-0.
pod_2326586c.jpg
Podolski akitupia goli la kwanza

Podolsi akishangilia goli

Magoli hayo pia ndio yalikuwa ya kwanza kwa Arsenal tangu msimu huu uanze kwani katika mechi zao mbili za awali walitoka sare ya 0-0 na wapinzani wao.

Kufuatia ushindi huo Kocha wa Arsenal alisema kuwa uimara wa vijana wake unaongezeka katika kila mechi na kuwa amefurahishwa na matokeo ya timu yake.

Baada ya kucheza mechi tatu, Liverpool ambayo iko nchini ya mkufunzi mpya Brendan Rodgers ina pointi moja peke yake.

Hii inaweza kufananishwa na matokeo mabaya ya timu hiyo katika msimu wa mwaka 1962-63 chini ya Bill Shankly.

Katika mechi hii washambulizi Luis Suarez na Fabio Borini hawakuwa na kubwa uwanjani.

Nae mchezaji mpya wa kiungo Nuri Sahin wa Liverpool pia hakuonyesha makeke yake uwanjani.

Santiago Carzola akishangilia baada ya kutupia goli la pili


Golikipa wa Arsenal Manone akishangilia ushindi


Patashika Steven Gerrard na Abou Diaby

Liverpool 0-2 Arsenal