Tuesday, September 11, 2012

RATIBA YA MECHI ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2014

RATIBA KIMATAIFA


KWA SAA ZA AFRIKA MASHARIKI (EA, GMT+3)

Tuesday 11 September 2012
New Zealand v Solomon Islands Auckland 010:35
Japan v Iraq Saitama 13:34
Uzbekistan v South Korea Tashkent 16:00
Lebanon v Iran Beirut 17:00
Jordan v Australia Amman 18:00
Czech Republic v Finland Teplice 19:00
United Arab Emirates v Kuwait Abu Dhabi 19:00
Cyprus v Iceland Larnaca 20:00
Israel v Russia Ramat Gan 20:00
Romania v Andorra Bucharest 20:30
Georgia v Spain Tbilisi 20:30
Bulgaria v Armenia Sofia 21:00
Turkey v Estonia Istanbul 21:00
Norway v Slovenia Oslo 21:00
Gabon v Saudi Arabia 21:00
Bosnia-Herzegovina v Latvia Zenica 21:15
Slovakia v Liechtenstein Bratislava 21:15
Austria v Germany Vienna 21:30
San Marino v Montenegro Serravalle 21:30
Serbia v Wales Novi Sad 21:30
Hungary v Netherlands Budapest 21:30
Sweden v Kazakhstan Malmo 21:30
Switzerland v Albania Lucerne 21:30
Republic of Ireland v Oman London 21:30
South Africa v Mozambique Mbombela Stadium 21:30
Italy v Malta Modena 21:45
Northern Ireland v Luxembourg Belfast 21:45
Belgium v Croatia Brussels 21:45
Poland v Moldova Wroclaw 21:45
Greece v Lithuania Piraeus 21:45
France v Belarus Saint-Denis 22:00
England v Ukraine Wembley 22:00
Scotland v Macedonia Glasgow 22:00
Chile v Colombia Santiago De Chile 22:30
Portugal v Azerbaijan Braga 23:00
Uruguay v Ecuador Montevideo 24:30

Wednesday 12 September 2012
Paraguay v Venezuela Asuncion 01:25
Peru v Argentina Lima 03:25
Tahiti v New Caledonia Papeete 08:00

SOMALIA YAPATA RAIS

Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud
 
Bunge la Somalia limemchagua Hassan Sheikh Mohamud kuwa Rais mpya wa nchi hiyo.

Hassan ameshinda kinyang'anyiro hicho kutoka wagombea 22 walioshiriki uchaguzi huo, akiwemo Rais anayeondoka Shariff Sheikh Ahmed na waziri mkuu Abdiweli Mohamed Ali.
Hassan Sheikh Mohamud alishinda kufuatia duru ya tatu ya upigaji kura, ambapo alikuwa anachuana na Rais anayeondoka Shariff Sheikh Ahmed.

Katika raundi ya kwanza Sheikh Ahmed alikuwa amepata ushindi mwembamba wa kura 64 dhidi ya 60 alizopata Sheikh Mohamud.

Kwa jumla wabunge 271 walipiga kura.

Katika duru ya mwisho wabunge wengi waliowaunga mkono wagombea waliochujwa walimuunga mkono Sheikh Mohamud , akapata kura 190 dhidi ya 70 alizopata Rais anayeondoka.

Hii ni mara ya kwanza kwa uchaguzi wa Rais kufanyika katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, tangu kuondolewa kwa serikali ya kijeshi mwaka 1991.

SIMBA USO KWA MACHO NA AZAM TAIFA LEO HII



Leo ndio leo wakati Mrisho Ngassa wa Simba anatarajia kuwa kiini cha utamu wa mchezo wa soka, pale atakaipoikabili kwa mara ya kwanza timu yake ya zamani, Azam FC katika mechi ya Ngao ya Jamii, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Mrisho Ngassa

Simba, mabingwa wa soka Bara walimsajili Ngassa kutoka kwa washindi hao wa pili wa Ligi Kuu Azam. Kabla ya kutua Simba, Ngassa alikuwa akiwaniwa na Yanga ya Dar es Salaam.

Mbali na Ngassa, mwingine ambaye leo huenda akawa kivutio, ni Ramadhan Chombo 'Redondo' atakayekuwa na timu yake mpya Simba.

Redondo ambaye usajili wake ulizua utata, alisajiliwa na Simba kutoka Azam FC, ambao nao awali walimsajili kutoka kwa Wekundu hao wa Msimbazi.

Pambano la timu hizo ni ishara ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu mwishoni mwa wiki hii, kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Ramadhan Chombo "Redondo"

REKODIKwa mwaka huu pekee, Simba na Azam zimekutana mara tano katika mechi za mashindano mbalimbali. Hazijawahi kutoka sare, huku Simba ikishinda michezo mitatu na Azam miwili.

Mechi ya karibuni ni ile ya nusu fainali ya michuano ya Super8, ambapo Simba iliyochezesha kikosi 'B' dhidi ya kikosi kamili cha Azam, ilishinda mabao 2-1.

"Majembe"
Kwa kiasi kikubwa Simba itakuwa na mwonekano tofauti kwa vile ina sura kadhaa mpya kutoka ndani na nje ya nchi.

Miongoni mwa nyota wapya mbali na Redondo na Ngassa kwenye jeshi la Simba leo, wengine ni mshambuliaji wake mpya kutoka Ghana, Daniel Akufo na beki raia wa Mali Komanbill Keita na Mkenya, Pascal Ochieng.

Nayo Azam kama ilivyo kwa wenzao wa Simba, inatarajiwa kuwa na mabadiliko kidogo hasa hasa katika mpangilio wa kikosi na hii ikitokana na kutokuwapo kwa Ngassa na Redondo.

Mfumo:
Wakati Simba itakuwa na kocha mwenye uzoefu na timu hiyo Milovan Cirkovic, Azam itaongozwa na kocha wake mpya Boris Bunjak aliyeukwaa ubosi, baada ya kutimuliwa Mwingereza Stewart Hall.

Timu zote zinatumia mfumo mmoja wa 4-4-2 na hata aina ya soka lao pia linafanana, likipingwa pasi nyingi fupifupi.

Wakizungumzia pambano baina yao, makocha wa timu hizo wakiwa katika hali ya kujiamini walijinasibu kila moja kufanya kweli na kuibuka na ushindi.

"Itakuwa mechi ngumu, lakini ni wakati wa sisi kulipa kisasi baada ya wao kutufunga Kombe la Kagame. Tupo vizuri kiakili na kisaikolojia," alisema Cirkovic.

Naye Bunjak alisema, "Ili ushinde unahitaji maandalizi, na kwa upande wetu tumejiandaa kikamilifu kuhakikisha tunashinda mechi hiyo na kutuongezea morali katika ligi."

Kwa upande mwingine, wachezaji wa kuchungwa zaidi leo ni pamoja na mshambuliaji nyota wa Simba Mganda Emmanue Okwi, kama itakavyokuwa kwa mpachika mabao hatari wa Azam John Boko 'Adebayor'.


Rekodi kamili Simba/ Azam mwaka 2012.

Mapinduzi Cup: Azam 2-0 Simba
Ligi Kuu: Simba 2-0 Azam
Urafiki Cup: Simba 3 -1 Azam (pen)
Kagame Cup: Azam 3- 1 Simba
Super 8: Simba 2- 1 Azam.

Monday, September 10, 2012

SIMU YA MKONONI NI HATARI KWA MAISHA YAKO,TAFADHALI ITUMIE KISTAARABU

Fun & Info @ Keralites.net
Hawa wanapata kahawa jioni lakini maongezi hakuna kila mtu bizee na kisimu chake


Fun & Info @ Keralites.net
Wapo Dinner lakini kila mtu kwenye simu jamani kunaniii simuni?

Fun & Info @ Keralites.net
Wamekaa wanamsubiri mgeni hotelini lakini hakuna stori ni simu tuu..khaaa!!!??

Fun & Info @ Keralites.net
Wamekutana chakula cha usiku"Dinner" mhhh biiizee na simu no stori hapa

Fun & Info @ Keralites.net
Marafiki wapo Ufukweni "Beach" lakini hakuna stori, hakuna kucheza wala kuogelea ni simu tuuu..mweeee!!!

Fun & Info @ Keralites.net
Haya sasa mtu yupo uwanjani hafuatilii tena mechi ni simu tuuu bhaaaah!!

Fun & Info @ Keralites.net
Hawa ni wapenzi wametoana "OUT" badala ya kubadilishana mawazo kudumisha penzi lao
kazi ni moja simuuu heeee!!

Fun & Info @ Keralites.net
Misere na ndinga kitaani No stori ni simu tu kuchata kwa kwenda mbele kaazi kwelikweli

Fun & Info @ Keralites.net
Shughuli sasa hii hapa, Wanapoendesha magari ni simu tuuu vimeseji mwisho wa siku wanasababisha ajali...jamani mhhh ukistaajab ya Khalid Utayaona ya Firauni.

Fun & Info @ Keralites.net
Achana na waendesha magari shughuli pia imo kwa watembeaji kwa miguu na waendesha baiskeli, umeonaaa ni simu tuuu kudadadadekii utakoma mwenyewe ni kikumbo tu ukizubaazubaa!!

OBAMA ABEBWA JUU JUU NA MUUZA PIZZA


Rais Obama akiwa amenyanyuliwa juu na Scott Van Duzer

Mmiliki wa Mgahawa maarufu jijini Florida, Marekani Scott Van Duzer alitoa kali ya mwaka alipotembelewa na Rais Obama katika mgahawa wake na kumnyanyua juu kama ishara ya furaha aliyikuwa nayo kwa ujio wa Obama pale mgahawani.

Rais Obama akitumia usafiri wa basi katika ziara ya siku mbili jijini Florida ikiwa ni sehemu za kampeni za uchaguzi utakaofanyika mwezi Novemba, alitembelea Mgahawa maarufu jijini Florida unaotambulika vilivyo kwa kuuza Pizza baaab kubwa unaojulikana kama Big Apple Pizza & Pasta Restaurant unaomilikiwa na Scott Van Duzer.

"Scott, what's going on, man," alisikika rais Obama akisalimiana na Van Duzer mara tu ya kuingia mgahawani. "Let me tell you, you are like the biggest pizza shop owner I've ever seen."  Obama aliendelea kumwaagia misifa Van Duzer ambae alimpigia kura rais Obama mwaka 2008 na ameahidi kumpigia tena kura mwezi Novemba.


Woooowww jamani rahaaa sio rahaaaa...Van Duzer akimkumbatia President Obama na kumnyanyua juu juu katika mgahawa anaoumiliki wa Big Apple Pizza & Pasta Restaurant jijini Florida,Marekani.

RICH MAVOKO- Marry ME


MAKAMO WA RAIS AHUKUMIWA KIFO

TariQ Al Hashemi
 
Mahakama nchini Iraq imepitisha hukumu ya kifo kwa makamu wa rais, Tariq al-Hashemi, baada ya kumkuta na hatia kwa kuongoza makundi ya kuuwa watu, yaliyowalenga Washia na askari wa usalama.
Makamo wa rais, wa madhehebu ya Sunni, hakuweko mahakamani wakati wa hukumu hiyo kwani alishaikimbia Iraq awali mwaka huu, akiwa sasa anaishi Uturuki.

Kesi hiyo imezusha msukosuko wa kisiasa katika serikali ya Iraq, iliyogawa madaraka kati ya Wa-Sunni, wa-Shia na WaKurd.

Bwana al-Hashemi amemshutumu Waziri Mkuu Nuri al-Maliki ambaye ni M-Shia, kuwa anawasaka wapinzani wake wa kisiasa wa madhehebu ya Sunni, lakini serikali inasisitiza kuwa kesi hiyo inafuata misingi ya sheria tu.


Hukumu hii ya mahakama imekuja huku watu wasiopungua 45 wakiwa wameuawa katika mfululizo wa mashambulizi 24 nchini Iraq. Siku ya Jumapili mashambulizi kadhaa yalishuhudiwa katika maeneo ya Tuz Khurmatu, Baquba, Basra na Samarra.

Wanajeshi 11 waliuawa kaskazini mwa Baghdad, huku katika mji wa Amara watu 14 wakiuawa na wengine 60 kujeruhiwa katika mashambulio mawili ya mabomu ya kutegwa katika gari.

Maafisa polisi saba pia waliuawa kwa bomu katika mji wa kaskazini wa Kirkuk, wakati wanajeshi kumi nao wakiuawa katika kambi ya jeshi ya Dujail kaskazini mwa Baghdad. Na katika eneo la Nasiriya kusini kulitokea mlipuko wa bomu nje ya ubalozi wa Ufaransa ulioua mtu mmoja huku serikali ya Ufaransa ikilaani shambulio hilo.

Hashimu alikuwa ni mwanasiasa wa juu sana aliyeheshimika kutoka dhehemu la Sunni katika serikali yenye Wa-Shia wengi hadi alipofunguliwa mashitaka mwezi December mwaka 2011 wakati alipotoroka nchini humo.

Wanasiasa wengine wa Ki-Sunni walimkataa waziri mkuu wa Ki-Shia Nouri al-Maliki aliyetoa amri ya kukamatwa kwa Bwana Hashemi, wakimuita kama dikteta na kumshutumu kwa kuendeleza chokochoko zinazoweza kuiingiza nchi hiyo katika vita vya kikabila kwa mara nyingine.

Waandishi wa habari wanasema muungano wa serikali kati ya Wa-Sunni, Wa-Shia na wale wa makabila mengine inaonkena kuwa hatarini tokea wakati huo.

Wapiganaji wa Ki-Sunni wanaohusishwa na kundi la kigaidi la al-Qaeda wamekuwa wakishutumiwa kwa vurugu za hivi karibuni nchini Iraq.