Monday, December 3, 2012

TANZANIA STARS YATINGA NUSU FAINALI YAIBANJUA RWANDA

Robo fainali ya kwanza ya michuano ya Tusker kati ya Tanzania Stars na Rwanda umemalizika jijini Kampala katika dimba la Lupogo,na timu ya Tanzania Stars ikitinga nusu fainali kwa kuichapa Amavubi mabao mawili kwa bila. Shujaa wa leo ni Mwinyi Kazimoto alietengeneza pande la maana kipindi cha kwanza katika dakika ya 33 na Amri Kiemba kumalizia kwa kumchambua kipa wa Rwanda na kutupia kambani bao la kwanza.
Dakika ya 54 ilikuwa ni Mwinyi Kazimoto"Iniesta" aliepiga shuti kali lililomshinda kipa wa Rwanda na bila kupepesa njumu, bila kupepesa bukta John Bocco "Adebayor" akauwahi mpira na kuutupia kambani na kufanya mabao kuwa ni 2-0.
Wakati Tanzania inatinga nusu fainali ndugu zao Zanzibar muda huu wapo uwanjani wakipepetana na Burundi katika robo fainali ya pili katika dimba hilohilo la Lupogo jijini Kampala,Uganda.
KILIMANJARO STARS 2-0 Rwanda
Shughuli imemalizika jijini Kampala, Stars imetinga nusu fainali baada ya kuichapa Amavubi mabao mawili kwa bila. Shujaa wa leo ni Mwinyi Kazimoto alietengeneza pande la maana kipindi cha kwanza katika dakika ya 33 na Amri Kiemba kumalizia kwa kumchambua kipa. Dakika ya 54 ilikuwa ni Mwinyi Kazimoto aliepiga shuti kali lililomshinda kipa wa Rwanda na John Bocco "Adebayor" akauwahi mpira na kuutupia wavuni. Hongera Stars!
Wachezaji wa Tanzania wakishangilia goli lililofungwa na John Bocco(14)

ROBO FAINALI TUSKER TANZANIA,ZANZIBAR KUPENYA?

ROBO FAINALI YA MICHUANO YA TUSKER CHALLENGE CUP 2012 INAYOENDELEA UGANDA

Desemba 3, 2012

Tanzania Vs Rwanda Saa 8:00 mchana Lugogo

Zanzibar Vs Burundi Saa 10:00 jioni Lugogo

Desemba 4, 2012

Kenya Vs Malawi Saa 10:00 jioni Namboole

Uganda Vs Ethiopia Saa 1:00 usiku Namboole

Friday, November 30, 2012

MAZISHI YA SHARO MILIONEA


MAREHEMU HUSSEIN RAMADHANI MKIETI "SHARO MILIONEA"

Zifuatazo ni picha za matukio katika mazishi ya msanii mchekeshaji na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a SHARO MILIONEA yaliyofanyika nyumbani kwao Muheza,Tanga siku ya Jumatano 28/11/2012.


Sajuki na Mlela wakiwa msibani



Umati wa waombolezaji wakiwa msibani


Baadhi ya wasanii waliohudhuria msibani Belle 9,Shetta,Timbulo na Tundaman


Mama mzazi wa Sharo Milionea akilia kwa uchungu katika msiba wa mwanawe.


Mjomba wa Sharo Milionea akimwaga chozi


Wema Sepetu akiwa msibani


Miss Kinondoni 2 Husna akimwaga Chozi

WALIOTOA NASAHA

Steve Nyerere

Nape Nnauye

Mzee Majuto

Mwana FA akitoa salamu kwa niaba ya wasanii wa Bongo flava

Mwili wa marehemu Sharo Milionea ukianza safari kuelekea makaburini


Kila mtu alijitahidi kufanya awezavyo ili mradi ashuhudie mazishi


Nnauye akiwa eneo la makaburini

WALIOZIMIA









MAKABURINI

Mzee Majuto





GARI ALILOPATA NALO AJALI




Tuesday, November 27, 2012

R.I.P HUSSEIN RAMADHAN MKIETE "SHARO MILIONEA"

Msanii wa vichekesho na muziki wa kizazi kipya Hussein Ramadhan Mkiete a.k.a Sharo Milionea amefariki katika ajali ya gari iliyotokea kijiji cha Lusanga,Muheza mkoani Tanga Siku ya jumatatu ya tarehe 26/11/2012 majira ya saa mbili usiku.
Habari zilizothibitishwa na kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga Constatine Massawe. kifo cha Sharo Milionea kimesababishwa na ajali aliyoipata wakati gari yake aina ya Toyota Harrier ilipopasuka tairi na kugonga mti eneo la Maguzoni.
Mwili wa marehemu Sharo umehifadhiwa katika hospitali Teule Tanga kwa kusubiria taratibu za mazishi zitakazofanywa na ndugu wa marehemu, Mungu ailaze roho ya marehemu Hussein Ramadhan Mkiete a.k.a SHARO MILIONEA Mahala pema peponi,AMIN!


Marehemu Hussein Ramadhan Mkiete "SHARO MILIONEA" enzi za uhai wake.


Sharo Milionea akifanya shopping mwezi huu kabla ya kupata ajali iliyoondoa uhai wake.



VIDEO ZA NYIMBO ZA SHARO MILIONEA

Monday, November 26, 2012

MAN CITY, CHELSEA HAKUNA MBABE

Timu za soka za Chelsea na Man City ziliumana katika mwendelezo wa mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza katika uwanja wa Stamford Bridge.
Katika mpambano huo wa wababe hao kutoka suluhu na ikiwa mechi ya kwanza kwa kocha mpya wa Chelsea Rafael Benitez akichukua nafasi ya kocha kipenzi cha mashabiki wa Chelsea Roberto De Matteo.
Mashabiki wa Chelsea hawakufurahishwa na kitendo cha De Matteo kutimuliwa na wameonesha kwa kiasi kikubwa hawamkubali kabisa Rafael Benitez ambaye ameshindwa kuipa matumaini mema Liverpool alipokuwa kocha mkuu na sasa yupo Chelsea itakuwaje? ngoja tusubirie lakini mashabiki na mimi mwenyewe hatumkubali Benitez kama tunavyomkubali De Matteo.




Mashabiki wa Chelsea na ujumbe wa kumdhihaki Benitez na kumtukuza De Matteo


Benitez akiwa kibaruani lakini mashabiki hawamkubali hata kidogo

Roberto Mancini kocha wa Man City akitoa maelekezo katika mpambano huo


Huu Haaa!! Kazi Vicent Company na Torres


Tulia wewe bwana mdogo tuu!!! Torres akiwa chini ya ulinzi mkali


Ukijipendekeza nakupasua!!! Ramires akimtuliza Aguero


Aaaah mi nimeshachoka msiniseme sana bhanaa wanakaba kama nini!!

MPIGIE KURA MCHEZAJI UNAYETAKA ACHUKUE TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA 2012 YA BBC

Majina ya wachezaji watano wanaowania tuzo la BBC la mchezaji bora zaidi barani Afrika mwaka 2012 yamewekwa hadharani.

Bofya Yahya Toure.
Mcheza kiungo kutoka Ivory Coast, anayeichezea Manchester City ya Uingereza. Toure aliiongoza Manchestert City kushinda kombe la ligi kuu ya Premier ya England kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka 44 iliyopita.


Bofya Demba Ba
kwa sasa ni mmoja wa wachezaji nyota wa klabu ya Newcastle na kufikia sasa tayari amefunga jumla ya magoli 6 katika ligi kuu ya premier la England na anatarajiwa kujumuishwa kwenye kikosi cha Senegal kitakachocheza katika fainali ya kombe la mataifa bingwa barani Afrika.


Bofya Didier Drogba
Ni noadha wa timu ya taifa ya Ivory Coast, amewahi kuongoza Chelsea kushinda kombe la ligi kuu ya Premier ya England pamoja na kombe la klabu bingwa barani ulaya.


Bofya Christopher Katongo
Ni mchezaji wa timu ya taifa ya Zambia maarufu kama Chipolopolo na aliiongoza timu hiyo kushinda fainali ya kombe la mataifa bingwa barani Afrika


Bofya Younes Belhanda
Ni mchezaji mwenye umri wa miaka 22, na mmoja wa wachezaji waliotia fora na kuisaidia klabu ya Montepellier, kushinda kombe la ligi kuu kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya karne moja tangu klabu hiyo ilipobuniwa.

PIGA KURA HAPA
Bofya Ukitaka kupiga kura unaweza kufungua anwami hii ya mtandao na kumbuka maagiza yametolewa kwa lugha ya Kiingereza.