| 21:45 - 23:45 |
Spain
| The UEFA Champions League | Real Madrid vs Juventus |
Wednesday, May 13, 2015
WATCH LIIVEEEE REAL MADRID Vs JUVENTUS
HALI ILIVYO BURUNDI BAADA YA NKURUNZINZA KUPINDULIWA
Wananchi wakishangilia Baada ya Nkurunzinza kupinduliwa
Waandamanaji wakijimwayamwaya mitaani
Wananchi wakishangilia Burundi
Raia wakikumbatiana katika bustani la uhuru Bujumbura
Raia wakiwazoma maafisa wapolisi ambao awali walikuwa wakikabiliana nao
Tuesday, May 12, 2015
WATCH BAYERN MUNICH Vs BARCELONA LIVEEEE
| 21:45 - 23:45 |
Germany
| The UEFA Champions League | Bayern Munchen vs FC Barcelona |
BUNGE LA BAJETI KUANZA LEO, WASOMI WALIKOSOA
Saa za mjadala katika vikao zimeongezwa ili kuziba
pengo la siku 12 zinazopungua na kutoa fursa kwa wabunge kuchangia
bajeti za wizara na Bajeti Kuu ya Serikali ndani ya siku 44
ikilinganishwa na siku 56 zilizotumika kupitisha bajeti ya mwaka 2014/15
na miaka ya nyuma.
Kutokana na hali hiyo, wachambuzi wa bajeti,
wachumi na wanasiasa wamesema hawatarajii kuona jipya isipokuwa mipasho
inayolenga Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Serikali imepanga kukusanya na kutumia Sh22.4
trilioni katika mwaka wa fedha 2015/16 ikiwa ni nyongeza ya Sh2.6
trilioni ikilinganishwa na Bajeti ya mwaka 2014/15 ambayo ilikuwa Sh19.8
trilioni.
Kwa miaka iliyopita, baadhi ya wizara zenye
majukumu mengi zilikuwa zinatengewa siku mbili au tatu, lakini safari
hii hali itakuwa tofauti kwa kuwa zitajadiliwa kwa siku moja tu au mbili
kulingana na mjadala utakavyokuwa na mapumziko yatakuwa Jumapili pekee.
Mkurugenzi wa Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano
wa Kimataifa wa Bunge, Jossey Mwakasyuka alisema badala ya Bunge kuanza
saa 3.00 asubuhi hadi saa 7.00 mchana na baadaye saa 11 jioni hadi saa
1.45 usiku; sasa litaanza 3.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana na kuendelea
saa 10.00 jioni hadi saa 2.00 usiku.
“Ili kuendana na muda, tumeongeza saa kadhaa ili
kumaliza shughuli zote zilizopangwa. Siku za Jumamosi zitahesabika kama
siku za kazi kama kawaida.” alisema.
Alisema Bunge hilo litamalizika Juni 27 lakini
akaongeza: “Tumeacha siku tatu za dharura, kuanzia Juni 28 hadi 30 ili
kama kuna jambo lolote la muhimu litajitokeza Bunge linaweza kuendelea
kwa muda huo wa siku tatu.”
Alisema kutokana na mabadiliko ya uwasilishaji, ni
lazima bajeti iwe imesomwa kabla ya kuanza utekelezaji wa bajeti ya
mwaka unaofuata Julai Mosi.
“Inawezekana tukapata kiongozi wa kulihutubia
Bunge au katika upitishaji wa bajeti za wizara akidi isitimie na
kulazimika shughuli husika kuendelea siku inayofuata. Zamani Bunge la
Bajeti lilikuwa likianza Juni hadi Agosti, lakini kwa mabadiliko haya
sasa lazima limalizike Juni,” alisema.
Alisema bajeti zote za wizara hadi kufikia Juni 10
zitakuwa zimeshasomwa, Juni 11 itasomwa Bajeti Kuu ya Serikali na
kuanza kujadiliwa.
Alisema ratiba hiyo pia inaweza kuvurugika utakapoanza mfungo wa Ramadhani.
Friday, May 8, 2015
TASWIRA YA JIJI LA DAR NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA


Maeneo ya Jangwani jijini Dar
Gari limetumbukia kwenye daraja lililobomoka maeneo ya Mbezi Makondeni kwa Mahita

Mmoja ya wakazi walioathirika na mafuriko

Mtaa wa Azikiwe jijini Dar


.jpg)
Lori la kokoto likiwa limezama Mto Msimbazi jijini Dar
Thursday, May 7, 2015
LIGI KUU SPAIN YAPIGWA "STOP"
Wapenda soka ulimwenguni hususani wanaopenda kuangalia ligi kuu ya Uhispania wale mashabiki wa Barcelona na Real Madrid bila kusahau wazee wa mikeka wataimiss ligi hiyo baada ya kusimamishwa,Hatua hii inafuatia mtafaruku baina ya shirikisho la ligi kuu la Uhispania na serikali ya taifa kuhusiana na ugavi wa mapato ya haki miliki ya kupeperusha mechi.
Pande zote zimeshindwa kukubaliana kuhusu ugavi wa mapato ya matangazo ya mechi za ligi hiyo maarufu duniani.
Agizo hilo liitaanza kutekelezwa kuanzia tarehe 16 mei.
Maamuzi hayo yataathiri zaidi ya wachezaji laki sita (600,000) na mechi elfu thelathini (30,000).
Kufikia hizi sasa Barcelona inaongoza jedwali la La Liga,wakiwa na alama mbili pekee zaidi ya wapinzani wao wakuu Real Madrid huku zikiwa zimesalia mechi tatu tu msimu ukamilike.
Serikali kuu imepitisha mswada mpya ambao utasimamia ugavi wa fedha zinazotokana na hati miliki ya matangazo ya mechi hizo za la Liga.
Mswada huo unaungwa mkono na muungano wa wachezaji wa kulipwa LFP.
Mkataba uliopa sasa inaziruhusu vilabu viwili vikuu nchini humo yaani , Barcelona na Real Madrid kukubaliana kivyao kuhusu nani atapeperusha mechi zao.
Kuna madai kuwa timu hizo mbili zinatia kibindoni nusu ya mapato yanayotokana na mechi zao.
Shirikisho lenyewe limesema kuwa linafahamu hasara itakayotokea lakini halijafunga mlango wa majadiliano.
Wednesday, May 6, 2015
watch live BAYERN MUNICH Vs BARCELONA
| 21:45 - 23:45 |
Spain
| The UEFA Champions League | FC Barcelona vs Bayern Munchen |
Subscribe to:
Posts (Atom)