MIJI IMARA KIUCHUMI MAREKANI.
LITTLE ROCK,Arkansas.
Little Rock ni mji wenye utajiri mkubwa ikihusisha kuwa na Hospitali kubwa,Taasisi za matibabu na pia mji huu una idadi kubwa ya shule na vyuo vyenye kutoa elimu bora. mji una idadi ndogo ya watu wasio na ajira kwani ni 7.7% kiasi ambacho ni kidogo ukilinganisha na kiasi cha Taifa ambacho idadi ya wasio na ajira ni 9.7% . Chuo cha sayansi ya madawa cha Arkansas ndio kinatoa ajira kwa jamii kwa idadi kubwa na masaa ya kufanya kazi ni Dakika 17.6, mji huu una wakazi 189,515. ukiwa ni mji wa kwanza kwa utajiri, 29 kwa elimu, 22 kwa afya , 61 kwa usalama.
BILLING,Montana.
Mji huu una idadi ya wasio na ajira kwa 6%. una idadi ya watu wanaofikia 103,994. Ni mji wa 65 kwa kutoa elimu bora, wa 41 kwa huduma za afya ,59 kwa kuwa na usalama, ni namba 2 kwa uchumi mzuri. Utajiri wa mji huu unaletwa na hifadhi za Yellowstone,Grand Teton na Little Bighorn.Muda wa kufanya kazi ni dakika 15.
SIOUX FALLS,South Dakota.
Mji huu una mbuga na hifadhi ndani ya eneo la heka zipatazo 2913, Mji huu unaonekana kama ndio kituo cha utamaduni, Na ni mji wenye idadi ndogo ya uhalifu,msongamano mdogo wa magari na idadi ndogo ya uchafuzi wa mazingira huku ukiwa na uwiano wa 13/1 ya wanafunzi na kuufanya kuwa mji bora kwa elimu. Idadi ya watu inafikia 154,997. Ni mji wa 60 kwa elimu bora, 3 kwa afya bora na huduma za afya, 45 kwa usalama, 3 kiuchumi.
SALT LAKE CITY,Utah.
Mji huu una idadi ya watu inayofikia 181,698. Masaa ya kufanya kazi ni dakika 20, ni mji wa 59 kwa kutoa elimu bora, 27 kwa huduma nzuri za afya, 75 kwa usalama, na wa 4 kwa uchumi. Uwapo Salt lake usafiri kufika popote pale kwa urahisi na uhakika ambapo kutoka mjini mpaka uwanja wa ndege ni dakika 10 tu na usafiri upo kila kona ya mji.
TULSA,Oklahoma.
Mji huu una idadi ya watu wapatao 385,635. Muda wa kufanya kazi ni dakika 17.8, Ni mji wa 5 kwa utajiri, 57 kwa usalama, 52 kwa huduma bora za afya, wastani wa walimu nawanafunzi ni 15/1.
No comments:
Post a Comment