Thierry Henry alifunga goli lake la nane kwa msimu huu wakati timu yake ya New York ilipotoka sare ya 3-3 na Portland jumapili iliyopita, na kumfanya kuongoza kwa ufungaji katika ligi ya Marekani sambamba na London Donovan. Katika mechi hiyo Henry alilimwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kichogoni mchezaji wa Portland Moffat baada ya kutokea majibizano baina ya wawili hao.
Kwa kile kilichoonekana kuwa ni utani wachezaji hao walipatana laki ni muamuzi wa mechi hiyo alionekana akijadiliana na mshika kibendera na aliporudi uwanjani akampatia Henry kadi nyekundu na kumpa Moffat kadi ya njano, kitendo hicho kiliwapandisha jazba wachezaji wa New York na walionekena kumzonga mwamuzi lakini Henry kwa upande wake alipeana mikono na wachezaji wa Portland na mwisho alimpa mwamuzi mkono na kutoka nje. Kitendo hicho cha mwamuzi kumpa Henry kadi kilikemewa vikali na uongozi wa New York na katika mtandao wa New York malalamiko yalimshutumu mwamuzi kwa kuchezesha vibaya mechi hiyo,ambapo uongozi ulilalamikia timu ya Portland kwa kucheza faulo nyingi na mwamuzi aliwapendelea,uongozi wa New York ulikiambia chama cha soka Marekani kutowaendekeza waamuzi kama hao kuchezesha mechi kwani wanadidimiza soka la Marekani.
No comments:
Post a Comment