Timu ya soka ya Azam F.C ya jijini Dar es salaam imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Kagame baada ya kuitandika AS Vita ya DRC katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa katika dimba kuu la Taifa jijini Dar es salaam.
AS Vita ndio walikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za Azam kabla ya John Bocco"Boko haram" kutupia kwa kichwa baada ya krosi maridhawa ya Erasto Nyoni. Mtanange ulikuwa mkali na wakushambuliana kwa zamu na ndipo mchezaji machachari alieingia kipindi cha pili Mrisho Halfan Ngassa alipotupia kambani bao la pili katika dakika za majeruhi na kuipeleka Azam fainali ya michuano ya Kagame.
Sasa Azam ambayo iliwaondosha mabingwa wa soka Tanzania bara Simba S.C katika mchezo wa robo fainali kwa mabao 2-1, Inabidi isubiri mshindi wa nusu fainali nyingine ambayo inaendelea hivi sasa kati ya Yanga na APR ni dakika ya 8 hakuna timu iliyoliona lango la mwenzake.
No comments:
Post a Comment