Mike Du Toit amepatikana na hatia ya kutaka kumuua Nelson Mandela mwaka 2002
Mike Du Toit akiwa mahakamani
Nelson Mandela
Mtu aliyepanga njama za kutaka kumuua rais wa kwanza mweusi wa
Afrika Kusini, Nelson Mandela amepatikana na hatia.
Mahakama ya Pretoria imemtia hatiani kiongozi wa kundi la -Boeremag linaloamini kuwa mtu mweupe ni bora kuliko mtu mweusi alipatikana na hatia ya kupanga kumuua Mandela mwaka 2002.
Bwana Mike du Toit ndiye aliyepanga milipuko tisa katika eneo la Soweto mjini Johannesburg mwaka 2002.
Kiongozi huyo wa kundi la ki-baguzi ni mtu wa kwanza kupatikana na hatia tangu utawala wa wengi uanze mwaka 1994 nchini Afrika kusini.
Wataalamu wa mambo wanasema kuwa bado kuna hali ya kutopendana kati ya watu wa rangi tofauti nchini Afrika kusini.
Hata hivyo kundi kama la Boeremag,inayomaanisha Nguvu za Makaburu miongoni mwa Makaburu ,halina ufuasi mkubwa.
Mahakama hiyo ya Pretoria imempata Du Toit, ambaye alikuwa msomi baada ya kusikiliza kesi hiyo kwa miaka tisa.
No comments:
Post a Comment