Wednesday, January 23, 2013

KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA IVORY COAST YAIANGAMIZA TOGO

Mechi za awali za kombe la mataifa ya afrika zimemalizika jana huku kila timu ikiwa imeshacheza mchezo mmoja, Timu ya soka ya taifa ya Ivory Coast ikiwa imesheheni nyota "ma-father" wanaocheza soka la kulipwa kama Drogba,Yaya Toure,Kolo Toure,Didier Zokora"Maestro",Ya Konan,Solomon Kalou,Emmanuel Eboue na Gervinho iliweza kuiadabisha timu ya taifa ya Togo iliyokuwa ikiongozwa na Emmanuel Adebayor kwa bao 2-1 katika mchezo uliopigwa katika dimba la Royal Bakofeng na kushuhudiwa na watazamaji wapatao 2,000.

Ilikuwa katika dakika ya 7 tu ya mchezo pale Yaya Toure alipotupia kambani goli la kwanza kabla ya Jonathan Ayite kusawazisha katika dakika ya 45 sekunde chache kabla ya mapumziko. Timu zote zilirudi uwanjani na nguvu mpya kila moja ikitafuta ushindi lakini katika mchezo huo uliotawaliwa zaidi na nyota wa Ivory Coast na dakika 3 kabla mchezo kumalizika mshambuliaji "mchoyo" wa Arsenal Gervinho aliweza kuipatia Ivory Coast goli la pili na la ushindi. Mpaka mwisho Ivory Coast 2-1 Togo.

Yaya Toure akishangilia goli na wachezaji wenzake

Adebayor chini ya ulinzi mkali

Togo wakishangilia goli la kusawazisha


Drogba akionesha udambwidambwi..

Gervinho wa Ivory Coast akitiririka na gozi la ng'ombe


Gervinho akishangilia goli
Ivory coast 2-1 Togo

No comments:

Post a Comment