Mabingwa wa soka Tanzania bara, Simba s.c "wekundu wa msimbazi" wamepata ushindi wao wa kwanza nchini Oman baada ya kuiadabisha Ahli Sidab kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Oman ambako Simba wamepiga kambi kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania bara.
Viungo Kigi Makassy na Amri Kihemba walikuwa mashujaa kwa upande wa Simba baada ya kutupia kambani mabao katika kila kipindi cha mchezo huu.
Makassy alitupia kambani bao la kwanza dakika 21 kabla ya kutolewa nje baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Amri Kiemba ambaye aliingia na kutupia kambani bao la pili na la ushindi katika dakika ya 68.
Wakati huohuo, baada ya kumrudisha kundini beki Juma Nyosso wiki iliyopita, uongozi wa Simba sasa upo mbioni kumuuza beki Juma Nyoso nchini Oman.
Simba kwa sasa ipo kambini Oman na viongozi wake wapo kwenye mazungumzo na wakala Said Ally aliyeonyesha nia ya kumtafutia timu Nyoso.
Nimeshazungumza na Simba na kila kitu kinaenda sawa, tukifikia mwafaka nitaweka wazi ni timu gani atachezea na kiasi ambacho atauzwa, alisema wakala huyo.
Simba wiki iliyopita walimaliza tofauti zao na Nyoso aliyedaiwa kushuka kiwango na kumlazimisha kuchezea timu B, jambo lililopingwa vikali na beki huyo.
Juma Nyosso
No comments:
Post a Comment