Tuesday, December 3, 2013

YAYA TOURE MWANASOKA BORA WA BBC AFRIKA 2013


Yaya Toure katika uzi wa Man City
Yaya Toure ambaye ni raia wa Ivory Coast, na pia ni kiungo wa klabu ya Manchester City ya Uingereza, Toure alisugua benchi katika tuzo hizo kwa miaka minne mfululizo kwa kutokuwepo  katika orodha ya wachezaji wanaowania tuzo za mwanasoka bora wa mwaka wa BBC upande wa Afrika, Yaya Toure  aliwashinda Pierre-Emerick Aubameyang, Victor Moses, John Mikel Obi na Jonathan Pitroipa, na  kuibuka mshindi.
Toure kwasasa ana umri wa miaka 30.
Orodha fupi ya waliowania tuzo hiyo ilitayarishwa na wataalamu 44 wa soka kutoka kote barani Afrika, na wakizingatia hasa maarifa ya mchezaji, kiufundi, ushirikiano na wenzake katika timu, na kwa kucheza mchezo safi na wa uhakika kwa nidhamu ya hali ya juu. 

 
Yaya Toure katika uzi wa timu yake ya Taifa,Ivory Coast
 
Tazama udambwidambwi wa Yaya Toure

No comments:

Post a Comment