Friday, September 16, 2011

Bayern Munich Plot Bargain £7m Raid For Malouda


Florente Malouda

Bayern Munich are planning a £7million raid for Chelsea midfielder Florent Malouda in January.
The 31-year-old has only one-year remaining on his current deal and will be free to talk to other clubs in the new year.
The France international has seen his chances of playing regular first-team football hinderered by the Blues signing Juan Mata from Valencia.
Bayern are interested in the winger and hope Chelsea want to cash in on Malouda rather than let him go for free next summer, according to German magazine Kicker.
He was linked with a move away from Stamford Bridge during the previous transfer window with AC Milan and Juventus also keen on his signature.
Chelsea are believed to want to reduce the average age of the squad as well as the wage bill, and Malouda may be a casualty of the new regime.
Nicolas Anelka, Dider Drogba and Paulo Ferreira are all on the lookout for new clubs, but the Blues may decide to offer new deals or keep them until the summer.

YANGA YAANZA LIGI


MABINGWA watetezi, Yanga jana walipata ushindi wao wa kwanza kwenye Ligi Kuu baada ya kuichapa African Lyon kwa mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Mashabiki wa Yanga waliokuwa na hamu ya kuona timu yao ikishinda mchezo huo walisubiri kwa dakika 35, mpaka mshambuliaji wa kimataifa wa zamani wa Zambia, Davies Mwape alipofunga bao la kuongoza, lakini Lyon walisawazisha bao hilo kupitia kwa Hamis Shengo kabla ya Rashid Gumbo wa Yanga aliyeingia akitokea benchi kufunga bao la ushindi katika dakika ya 63.

Kwa matokeo hayo Yanga imejinasua mkiani kwa kufikisha pointi sita katika michezo mitano na kurudisha faraja kwa mashabiki wao kabla ya mechi ya Jumapili dhidi ya Azam itakayofanyika kwenye Uwanja wa Taifa.

Pamoja na rekodi mbaya ya utovu wa nidhamu kwa timu za Ligi Kuu msimu huu jana mwamuzi Mathew Akrama wa Mwanza alichezesha mechi bila ya kuonyesha kadi kwa mchezaji yeyote.

Mchezo ulianza kwa kasi na katika dakika ya 4, Sino Agustino alifanikiwa kuunganisha vizuri krosi ya Seleman Kassim, lakini shuti lake liligonga mwamba na kurudi uwanjani.

Yanga ilijibu mapigo katika dakika ya 10 na 14 kupitia kwa Mwape aliyeshindwa kumalizia nafasi mbili baada ya kupigiwa pasi nzuri na Nurdin Bakari na Shamte.

Bao la kwanza la Yanga lilipatikana baada ya Pius Kisambale kupiga pasi ndefu kutoka katikati ya uwanja ambayo ilitua kwa Shamte Ally aliyemtengenezea nafasi Mwape ambaye aliusukuma mpira wavuni katika dakika ya 35 na kuamsha shangwe kwa wanajangwani.

Dakika tano baadaye, Kassim wa Lyon aliwatoka mabeki wa Yanga na kipa Berko na kupiga shuti golini, lakini Juma Seif alifanya kazi ya ziada kuwahi mpira huo na kuutoa nje.Ikiwa inaonekana timu hizo zitaenda mapumziko huku Yanga ikiongoza kwa bao moja, Hamis Shengo aliisawazishia Lyon kwa mpira wa adhabu alioupiga na kwenda moja kwa moja wavuni na kumwacha Berko asijue la kufanya.

Kabla ya kufungwa bao hilo katika dakika ya 42, beki wa Yanga, Bakari Mbegu alimchezea vibaya kiungo Kassim nje kidogo ya eneo la 18, faulo ambayo ilitoa nafasi kwa vijana wa Lyon kupata sare 1-1 hadi mapumziko.Kipindi cha pili Yanga ilianza kwa kasi na katika dakika ya 47, Pius Kisambale alikosa bao kwa shuti lake kupanguliwa na kipa Juma Abdul na kutoka nje.

Kocha Sam Timbe aliwapumzisha Shamte, Kigi Makasi na Juma Seif na kuwaingiza Kenneth Asamoah, Rashid Gumbo na Godfrey Bonny mabadiliko ambayo yaliisaidia Yanga.

Mabadiliko hayo yaliisaidia Yanga kwa sababu Gumbo aliyechukua nafasi ya Kigi aliipatia Yanga bao la pili katika dakika ya 63 kwa shuti la umbali wa mita 32, lililomshinda kipa wa Lyon, Abdul.Washambuliaji wa Lyon, Adam Kingwande na Agustino Sino watajilaumu wenyewe kwa kupoteza nafasi nyingi za kufunga katika mechi hiyo.

Katika mechi hiyo pia Gumbo alipiga shuti kali ambalo liligonga mwamba katika dakika ya 71 na kutoka vile vile Kenneth Asamoah alishindwa kumalizia pasi Kisambale akiwa ndani ya 18. Katika mechi hiyo kocha wa Lyon alifanya mabadiliko mapema, ambapo katika dakika ya 16 alimtoa Benedictor Jacob na kumwingiza Sammy Kessy pia baadaye alimtoa Kessy na kumwigiza Jacob Massawe.

Licha ya kuwapo ulinzi mkali kwenye uwanja wa Azam, wapo baadhi ya mashabiki waliruka ukuta ambao sio mrefu sana na kuingia uwanjani.Yanga: Yaw Berko, Shadrack Nsajigwa, Abuu Zuberi, Bakari Mbegu, Chacha Marwa, Juma Seif, Shamte Ally, Nurdin Bakari, Davis Mwape, Pius Kisambale na Kigi Makasi.
African Lyon: Juma Abdul, Aziz Sibo, Hamis Shengo, Shaban Aboma, Hamis Yusuph, Razaki Khalfan, Adam Kingwande, Seleman Kassim, Benedictor Jacob, Hood Mayanja na Agustino Sino.

Thursday, September 15, 2011

BEAUTIFUL AQUA TOWER OF CHICAGO

http://groups.yahoo.com/group/babes_in_blue/

http://groups.yahoo.com/group/babes_in_blue/

KWANINI VIONGOZI TANZANIA HAWAWAJIBIKI PINDI YANAPOTOKEA MAJANGA?

Nakwazika sana na matukio na shida zinazowakabili wananchi wa Tanzania bila ya viongozi wanaohusika kuwajibika ama kuwajibishwa..mfano hili swala la ajali ya meli kama ingekuwa limetokea nchi zenye viongozi wanaojua nini uongozi na wenye maadili katika utumishi wa umma lazima wahusika wangejiuzulu,

Tumeshaona mifano nchi nyingi viongozi wakijiuzulu pindi mambo yanapokwenda kombo katika idara ama vitengo vyao iwe wamesababisha wao ama wamesababisha watendaji wao likishatokea janga ni kujiuzulu tu hakuna mjadala..kwa masikitiko hali ni tofauti hapa Tanzania, madaraka yanatumiwa vibaya na waliopewa dhamana kwani wanajali zaidi maslahi yao kuliko Taifa lenye watu waliowachagua. Na hii inatokana na udhaifu wa kiongozi mkuu ambaye ni Raisi, yeye ndie mwenye kusimamia Taifa na viongozi wake lazima awe na msimamo katika kuhakikisha watendaji wake wanawajibika kwa mujibu wa kanuni na taratibu za nchi.

Sioni sababu ya Viongozi ambao wizara ama idara zao zina kashfa za mikataba mibovu,matumizi mabaya ya ofisi,maafa kutokana na uzembe wa watendaji wao,hali ya maisha kuwa ngumu kutokana na upandaji na ukosekanaji wa bidhaa muhimu katika taifa,wizi na ufujaji wa mali za umma na wengineo wengi kuendelea kubaki katika nyazifa zao.

Kwa staili hii ya viongozi wazembe kuendelea kuonekana kama miungu watu Daima taifa litaendelea kuwa masikini, kwani kutokana na ajali na vifo vya majanga ya kizembe vinapoteza watu ambao ni nguzo muhimu katika ujenzi wa Taifa, Kutokuwa na uwajibikaji katika idara nyeti zinadumaza huduma muhimu kwa wananchi na kufanya kuwa na maendeleo duni,hivyo kama wananchi hawana la kufanya taifa haliwezi kupata kipato.
Inauma na inakera sana kuona nchi inakosa mwelekeo kwasababu ya watu wachache, Jamani enyi viongozi hivi mliingia katika uongozi ili muwatumikie wananchi kweli?
Nilichogundua ni tofauti ya kuwa kiongozi hapa Tanzania na kuwa kiongozi nchi zingine, tofauti ni hii:
Nchi zilizoendelea mtu anagombea uongozi kwa hulka ya kuwa kiongozi ya kuwatumikia wananchi waliomchagua tofauti na viongozi wetu swala la kuwa kiongozi wameligeuza ajira, hapa ndio matatizo yalipo ndio maana kiongozi ukimwambia ajiuzulu ama awajibike inamuwia vigumu kwasababu hana mbele wala nyuma uongozi ndio kila kitu kwake.


Imefikia wakati sasa viongozi muone uongozi kuwa ni dhamana halisi ya kuwatumikia watu na sio ajira kama mlivyogeuza kwa hivi sasa, mkiwa na jinsi nyingine ya kuishi na mkauchukulia uongozi kuwa ni dhamana ya kuwatumikia wananchi lazima mtakuwa na maadili mema ya utumishi wa umma, pindi unapoonekana umeshindwa kuwajibika basi swala la kuachia ngazi halitokuwa gumu kwako kwani ilikuwa ni sehemu ya maisha yako na sio maisha yako.

Watanzania wenzangu kwa kulifahamu hili na mkagundua viongozi wetu wameufanya uongozi ndio njia yao ya kuishi hamtoshangaa kwanini wanafanyaufisadi na wamekuwa wagumu kuwajibika ama kuchukua maamuzi magumu. Uongozi sio ajira kama tunavyofikiria,mshahara unaopewa kiongozi ni malipo ya muda na busara zako unazozitumia katika kuwajibika kwa wanachi na Taifa kwa ujumla. Na sababu hizi za kuufanya uongozi kama ajira zinapelekea viongozi kutokuwajibika ipasavyo katika nyazifa zao kwakuwa muda mwingi wanapanga mipango ya kujipatia pesa ama kufanya kazi aile tu zenye kuwapatia pesa ama zenye 10% na kazi za mshahara huwa hazifanyiki kwa jinsi inavyotakiwa zifanyike.
Nitaendelea na mada hii........+255 684 887 525.

SIMBA IKO JUU KAMA "ROCKET" YAWACHEZESHA KWATA POLISI DODOMA


Ulimboka mwakingwe akijaribu kuska mpira bila mafanikio

MSHAMBULIAJI Gervais Kago aliisaidia timu yake ya Simba kuichapa Polisi Dodoma bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi.

Matokeo hayo yameifanya Simba kufikisha pointi 13 na kuendelea kubaki kileleni mwa ligi kuu wakifuatiwa na JKT Ruvu wenye pointi tisa, huku Yanga ikishikilia mkia ikiwa na pointi tatu.

Kocha wa Simba, Moses Basena alisema amefurahishwa na matokeo yaliyompa pointi tatu muhimu.

Mshambuliaji Kago alifunga bao lake la pili msimu huu kwa Simba katika dakika ya 25 akipokea pasi ya kifua kutoka kwa Felix Sunzu na kupiga shuti kali lililojaa wavuni.

Katika mechi hiyo Bryton Mponzi alipoteza nafasi ya kuisawazishia Polisi Dodoma baada ya kushindwa kuunganisha krosi ya Salmin Kiss Kiss huku kiungo wa Simba, Jerry Santo naye alijitahidi kufunga bao katika dakika ya 22 kwa kichwa, lakini beki wa Polisi alizuia mpira huo kwenye mstari wa goli.

Wakati Polisi Dodoma wakijitahidi kutafuta bao la kusawazisha Mponzi alipiga kichwa dhaifu kilichoishia mikononi mwa kipa Juma Kaseja, ambapo Simba walijibu mapigo katika dakika ya 43, baada ya Kago kujaribu kumtungua kipa wa Polisi Dodoma, Agathon Mkwandiko, lakini mpira huo ulitoka nje.


Uhuru Selemani wa Simba akichuana na beki wa Polisi Dodoma

Simba walirudi kipindi cha pili kwa kasi hasa katika dakika za 53, 56, ambapo Kago na Emmanuel Okwi walipoteza nafasi za kufunga wakiwa wao na kipa Mkwandiko kwa mashuti yao kutoka nje.

Mwamuzi Charles Mchau alitoa kadi za njano kwa Bantu admin wa Polisi Dodoma na Nassoro Said wa Simba kwa mchezo mbaya katika mechi hiyo.

Kocha wa Polisi Dodoma, John Kanakamfumu akizungumzia mechi hiyo alisema makosa ya mabeki wake katika kipindi cha kwanza ndiyo yaliyosababisha matokeo hayo.

"Nimegundua mapungufu kidogo, lakini tunakwenda kurekebisha kabla ya mchezo ujao," alisema Kanakamfumu.
Licha ya uwanja wa Azam kuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 5000, mashabiki walishindwa kuujaza uwanja huo na sababu mojawapo ikiwa ni ulanguzi mkubwa uliokuwa ukifanywa na wauza tiketi katika vituo mbalimbali.


Uhuru Selemani akikwepa daruga la mlinzi wa Polisi Dodoma

Hamasa kubwa ya mashabiki wa Simba waliotaka kuiangalia timu yao ikicheza kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi ilitumbukia nyongo kutokana walanguzi wa tiketi hizo.

Pamoja na TFF kutangaza tiketi ya kiwango cha chini kuwa shilingi 7,000 baadhi ya magari yalionekana yakiziuza tiketi hizo kati ya Sh 9,000 hadi 10,000.

Gari lililokuwa linauza tiketi Mbagala mwisho Toyota Hiace namba tunazo walitoa tiketi kwa watu waliokuwa wakiziuza eneo la Big Bon Mbagala kwa bei ya ulanguzi.

Huku gari hilo lilikuwa likizunguka mitaani na kusimama kwenye kituo cha mabasi yaendayo Mbande na Msongola na kuuza tiketi kwa bei kubwa kinyume na eneo walilotakiwa kusimama na kuuza tiketi.

Pia, nje ya eneo la TFF majira ya saa tano asubuhi watu wengi walikuwa wanauza tiketi za Sh 7000 kwa sh 10,000 wakati huo magari yalikuwa hayajaanza kuuza tiketi.


Brcelona,Arsenal,Man United zashindwa kutamba Chelsea,Real Madrid,Bayern zang'ara Ligi ya mabingwa Ulaya

Ligi ya mabingwa ulaya iliendelea tena wiki hii na kuona vigogo vikishindwa kutamba kwa kulazimishwa suluhu na timu pinzani. matokeo ya mechi hizo ni kama ifuatavyo.

13-9-2011

Barcelona        2-2     A.C Milan
F.C Porto         2-1    Shaktar Donetsk
B/ Dortmund   1-1    Arsenal
Olympiakos     0-1    Marseille
Chelsea           2-0    Leverkusen
Genk               0-0    Valencia
Opoel Nicosia 2-1    Zenit
 Plzen               1-1    Bate

14-9-2011

D/Zagret   0-1   R.Madrid
Ajax         0-0    Lyon
Benfica    1-1    Man United
Basel        2-1   Otelul Galat
Inter         0-1   Trabzosper
Lille         2-2   CSKA Moscow
Villareal  0-2   Bayern Munich
Man City 1-1   Napoli

                                              Matukio mechi Barcelona vs AC Milan



Matukio mechi ya Chelsea vs Leverkusen


Matukio mechi ya Borussia Dortmund vs Arsenal


Matukio mechi ya Man United vs Benfica


Matukio mechi ya D/Zagreb vs Real Madrid


Matukio mechi ya Villarel vs Bayern Munich


Matukio mechi ya Man City vs Napoli

Wednesday, September 14, 2011

TIMU YA SOKA LA WANAWAKE URUSI KUVAA BIKINI KATIKA MECHI ZAO

Timu moja ya soka la wanawake nchini Urusi wameafikiana katika jambo la kipumbavu kabisa kuwa ili kuongeza umaridadi na wepesi katika kulisakata kandanda wawe wanavaa nguo za ndani maarufu kama"bikini". Timu hiyo inajulikana kama F.C Rossiyanka imeafiki hilo ili kuiweka timu yao katika ramani ya soka ulimwenguni zifuatazo ni baadhi ya picha za timu hiyo katika mazoezi.