Tuesday, June 19, 2012
WAKATI TANZANIA INALIA NA MFUMUKO WA BEI, KABEJI MOJA CANADA INAUZWA DOLA 27
Je, unaweza kununua kabeji moja kwa dola 27 au kuku mmoja kwa dola 65, au maji ya lita kumi na mbili kwa dola 100? Hiyo bila shaka sio gharama ya mlo mmoja katika hoteli ya kifahari, lakini ndio bei ya vyakula muhimu katika maduka makubwa jimbo la Nunavut, kaskazini mwa Canada.
Wenyeji wa Iqaluit, mji mkuu wa jimbo hilo na wale wa Arctic Bay, Pond Inlet na Igloolik, pamoja na watu waliokerwa na bei hizo katika maeneo mengine nchini Canada, wamekuwa wakiandamana katika juhudi zao kuonyesha kero lao la bei ghali ya chakula katika maeneo ya vijijini.
Sasa kwa nini bei ya chakula ni ghali hivyo?
Nunavut ni mji ulio na ukubwa sawa na eneo zima la Magharibi mwa Uropa na eneo hilo limekalia sehemu kubwa Arctic iliyoko Canada lililo na watu 30,000.
Hali ya hewa ni mbaya na ukiwa unaishi maeneo ya kaskazini ina maana kuwa hakuna viwanda vya kilimo.
Vyakula vyote lazima vifikishwe katika eneo hilo kwa ndege kila siku kutoka sehemu zingine za nchi .
Kabla ya kuwasili kwa watu wa bara Uropa wenyeji wa sehemu hizo walitegemea uwindaji na uvuvi.
Lakini mabadiliko katika mfumo wa maisha una maana kuwa sasa watu wanategemea sana chakula kutoka nje na kwa muda mrefu watu wa maeneo hayo wanaweza tu kufikiwa kwa ndege.
"hatuna barabara zozote au njia za reli kutoka maeneo ya kusini kwa hivyo inabidi chakula kuletwa hapa kwa ndege kila siku," anasema Madeleine Redfern, meya wa mji mkuu wa, Iqaluit. "chakula muhimu kama maziwa na mkate huletwa hapa kila siku na wala sio sana katika sahemu zingine zilizo mbali kutoka hapa."
Michael McMullen, makamu wa rais wa kampuni ya North West ambayo ina maduka 32 katika maeneo ya vijijini nchini Canada, anasema kuwa kusafirisha chakula hadi kwenye maduka hayo, inagharimu mara kumi na moja zaidi kuliko maeneo ya Kusini. Anasema inagharimu doka 104.99 kufungisha maboksi ya chupa za maji ikizingatiwa gharama hiyo ni kabla ya kuzisafirisha.
"Usafirishaji pekee unatugharimu asilimia 13 ya gharama zote tunazotumia" alisema McMullane.
"Pia inatugharimu sana wakati tuzingatia mambo mengine kama umeme"
mboga ya kabeji
"Sio rahisi kusafirisha chakula, tunapata hasara kubwa zaidi wakati wa usafirishaji kulekea kaskazini kuliko maneo ya Kusini." aliongeza McMullen
Kulisha familia yangu.
Wakati bei ni nafuu kutuma chakula kinachoweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu kwa meli msimu huu nayo ina matatizo yake. "Kuna tatizo na uhifadhi wa vyakula hivyo" alisema bi Redfern. "tafakari tu kuleta hapa karatasi za kutumia vyooni yatakayotumika kwa mwaka mmoja kwa kwa watu wa hapa, ni pesa nyingi "
Leesee Papatsie, aliyeandaa maandamano hayo anayeishi eneo la Iqaluit, ana kazi nzuri lakini bado anatumia zaidi ya thuluthi moja ya mshahara wake kwa chakula, takriban dola 500- 600 kwa wiki.
"Chakula kina bei ghali sana" alisema mama huyo. " Mimi sijagutushwa na bei hiyo, angalau nimeishi katika mji mkubwa , katika miji midogo maisha huwa ghali"
Mshahara mdogo zaidi unaolipwa hapa Nunavut ni dola kumi na moja kwa saa, lakini kwa sababu ya bei ghali na mfumuko wa bei, ina maana kuwa pesa hizo ni kidogo sana kuweza kununua chochote kikubwa. Pia kuna ukosefu mkubwa wa ajira hapa inafika asilimia 16.
Afisaa mkuu wa umoja wa mataifa kuhusu haki ya chakula, Olivier De Schutter,hivi karibuni wakati wa ziara yake nchini Canada, alisema kuwa kati ya watu milioni mbili hadi milioni tatu nchini humo, hawawezi kumudu lishe wanayohitaji kuishi maisha mazuri yenye afya nzuri.
Alisema kuwa watu milioni moja na wengine 55,000 wa mji, wako katika hali mbaya.
Wenyeji wengi wa kusini mwa Canada wamekuwa wakiuliza ikiwa wenyeji huwinda na kutafuta chakula msituni ili kuweza kuepuka bei ghali ya chakula.
"Kuwinda na kutafuta chakula ni muhimu" alisema bi Redfern, lakini wakati mwingine inakuwa vigumu hata kupata chakula wakati wa shughuli ya uwindaji.
ITALIA YATINGA ROBO FAINALI EURO 2012 BALOTELLI ATUPIA
Balotelli akitupia kambani bao la pili na la ushindi
Cassano akiwa hewani na kupiga kichwa kilichazaa bao la kwanza la Italia
Italia ilipata ushindi dhidi ya timu ya Jamhuri ya Ireland ambayo tayari wachezaji wake walikuwa tayari wameshafungasha virago kuondoka kutoka mashindano ya Euro 2012, kwa kuwafunga magoli 2-0.
Jamhuri ya Ireland walianza mchezo huo wa Jumatatu usiku, wakithibitisha nia yao ya kujitahidi kupata ushindi, lakini Antonio Cassano, mchezaji wa Italia, ndiye aliyefanikiwa kuliona lango la Ireland akitupia kambani kwa kichwa kufuatia mpira wa kona iliyopigwa na Andrea Pirlo.
Hapa kazi tu!!! Thiago Motta wa Italia akichumpa hewani huku chini ni Kevin Doyle wa jamhuri ya Ireland
Iwapo Ireland ingelisawazisha, kama alivyokaribia kutupia kambani Keith Andrews
lakini kipa wa Italia Gianluigi Buffon alikuwa imara kuokoa mchomo wake, ingelimaanisha Italia,
katika kundi C, wangelijikuta wametupwa nje ya mashindano hayo ya Ulaya, hasa
kama Croatia ingelipata bao la kusawazisha dhidi ya Uhispania, mechi iliyochezwa
sambamba na hii, na iliyokwisha kwa ushindi wa Italia wa bao 1-0.
Andrews aliamrishwa na mwamuzi kuondoka uwanjani, baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya manjano, na Mario Balotelli akafanikiwa kutupia bao la pili na kuwatuliza mashabiki wa Italia.
Kutokana na Uhispania kuishinda Croatia, sasa itakutana na mshindi wa kundi D.
England ni miongoni mwa mataifa katika kundi hilo.
Kamba ya Balotelli
EURO 2012 JESUS AIPELEKA SPAIN ROBO FAINALI
Jesus Navas akitupia kambani goli la pekee na la ushindi
Jesus Navas alikuwa ni mkombozi wa timu ya Uhispania, pale alipotupia kambani dakika za lala salama dhidi ya Croatia, na kuiwezesha nchi yake kufuzu katika hatua ya robo fainali za mashindano ya Euro 2012.
Nakuja kwako Modric.........Andre Iniesta"fundi" akiwa amekusanya kijiji cha wa-croatia
Ilielekea kana kwamba mabingwa watetezi Uhispania walikuwa wakicheza mechi hiyo ya Jumatatu usiku kwa wasiwasi.
Hata hivyo Jesus, ambaye ni mchezaji wa Seville ya Uhispania, aliweza kupenyezewa pande maridadi na Andres Iniesta, na zikiwa zimesalia dakika mbili kabla ya mechi kumalizika, alifanikiwa kuipatia Uhispania bao, na kuwahuzunisha mashabiki wa Croatia.
Bao hilo moja lilihakikisha Uhispania inaongoza kundi la C.
Uhispania walicheza karata yao vyema, kwani kwa kumtoa Fernando Torres na mahala pake kuingia Jesus Navas, ni mchezaji huyo wa zamu aliyeweza kutupia kambani.
Sasa mabingwa watetezi wanasubiri kujua kama watakutana na England au Ufaransa katika timu nane ambazo zitasalia kucheza robo fainali.
Mhh ishakuwa sooo!!! shabiki wa Croatia akiwa amelowa baada ya chama lake kuchapwa na Spain
Iniesta akifanya udambwidambwi
Luka Modric akituliza ngozi mbele ya Xavi
Kichapo ni noma asikuambie mtu, mashabiki wa Croatia wakisononeka kwa machungu kufuatia kamba ya Jesus dakika za lala salama
Shabiki wa Croatia akimnyamazisha mwenzake alieangua kilio uwanjani baada ya kichapo cha bao 1 kwa 0 kutoka kwa Spain katika dimba la Gdansk Arena
Jikaze babaaa ndio mpira huoo
Wachezaji na mashabiki wa Croatia wakiwa katika majonzi mazito baada ya kushindwa kutinga robo fainali ya mashindano ya EURO 2012
Monday, June 18, 2012
HUYU NDIE STAR WA FILAMU ZA NGONO ALIEMTOA UDENDA BALOTELLI
Mario Balotelli na Holly Henderson
Mario Balotelli na Holly Henderson wakipata fegi katika maegesho ya magari jijini Manchester
Mchezaji mwenye matata na udambwidambwi mwingi Mario Balotelli akiwa na Holly Henderson ambaye ni mcheza filamu za ngono. Taarifa zilizopztikana mwishoni mwaka jana novemba zinasema Balotelli alikutana na Holly katika hoteli ya Manchester ambapo Holly alikuwa anapiga picha.
Imedokezwa kwamba wawili hao walikutana na kupeana mabusu ya nguvu katika eneo la maegesho ya magari kabla ya kusepa zao.
Wakati hayo yakitokea mchumba wa Balotelli alipokuwa Italia katika kazi za mitindo(Modelling)
Mario Balotelli na mchumba wake Rafaella Fico
Balotelli katika swaga za kapelo
Holly Henderson anaedaiwa kuwa na uhusiano wa siri na Mario Balotelli
Holly Henderson akiwa na mlinzi wake, sogea kipande kikutoe nnya
Holly Henderson akikatiza mitaani vidume mimacho balbu shingo feni
CHADEMA kama kawa
Holly anatafuta sehemu ya kuweka poss ufukweni
Holly anaweka sawa chakula ya watoto
Full Batraaaaaaaaaaa
BALOTELLI na swaga za body suit
UJERUMANI YATINGA ROBO FAINALI EURO 2012 YADUNGUA DENMARK
We kipara unaenda wapi? Mshambuliaji wa Denmark akichanja mbuga
Lars Bender alifunga bao la ushindi la Ujerumani siku ya Jumapili zikiwa zimesalia dakika 10 kabla ya kipenga cha mwisho, na kuiwezesha nchi yake kuwa miongoni mwa nchi nane ambazo zitashiriki katika michuano ya robo fainali.
Lars Bender akishangilia waya huku mlinda mlango wa Denmark akitambaa
Mechi nyingine ya kundi hilo la B ambayo ilichezwa wakati mmoja, kati ya Ureno na Uholanzi, Ureno walifuzu kwa ushindi kama huo wa magoli 2-1.
Bender, mwenye umri wa miaka 23, na ambaye ni mchezaji wa Bayer Leverkusen ya Ujerumani, aliizima ndoto ya Denmark ya mwaka 1992, walipowashinda Wajerumani katika fainali.
Mashabiki wa Ujerumani wakiwa wanakula bata huku wanafuatilia soka
Mashabiki wa Ujerumani wakishangilia baada ya chama lao kutinga robo fainali za EURO 2012
Ujerumani iliweza kuongoza katika mechi hiyo dakika ya 19 wakati Lukas Podolski alipofunga, lakini Michael Krohn-Dehli aliweza kuisawazishia Denmark dakika sita baadaye na kuipatia nchi yake matumaini ya kufika robo fainali.
Wachezaji wa Ujerumani hawakupendezwa na safari kutoka kituo chao cha nyumbani cha Gdansk, Poland, hadi Ukraine, lakini kutokana na ushindi wa Lviv, wameweza kufuzu kuingia robo fainali na watafurahia kuicheza mji ambao wameezeka kambi yao.
Kabla ya mechi ya Jumapili, mara ya mwisho Denmark ilipopambana na Ujerumani katika mashindano makubwa, ilikuwa ni fainali ya 1992, wakati Yugoslavia ilipopigwa marufuku kucheza, na hatimaye Denmark iliwashangaza wengi ilipoishinda Ujerumani katika fainali.
Timu ya Ujerumani ya mwaka huu ndio timu yenye vijana wenye umri mdogo zaidi katika mashindano ya mwaka huu, kwa jumla wachezaji wengi wakiwa na umri wa miaka 25 na siku 107.
Hii ni mara ya kwanza kwa Ujerumani kukamilisha mechi za makundi kwa rekodi safi mno ya asilimia 100.
GERMANY Vs DENMARK
EURO 2012 UHOLANZI DOROOOO YACHAPWA NA URENO
Christiano Ronaldo akitupia kambani bao la kwanza
Mabao mawili ya mshambuliaji Cristiano Ronaldo yaliiwezesha Ureno kuingia robo fainali ya michuano ya Euro 2012, kwa kuifunga Uholanzi, na pasipo shaka yoyote, kuwalazimisha kurudi nyumbani.
woyoooooooooooooooooooo!!!!!!!!!!
Kwa Uholanzi kuwa na matumaini yoyote kuendelea kusalia katika mashindano hayo, walilazimika kuifunga Ureno magoli 2-0, na bao la kwanza la mkwaju wa kupinda kutoka kwa Rafael van der Vaart liliwapa matumaini Uholanzi walipoweza kutangulia.
Lakini mchezo wa Uholanzi uliendelea kufifia, na Ronaldo alifanikiwa
kusawazisha, alipopigiwa mpira na mwenzake Joao Pereira.
Nani alimsaidia Ronaldo kufunga kwa mara ya pili, na Ureno ikavuka hatua ya makundi na kujiandikishia nafasi katika robo fainali.
Ureno sasa itacheza na Jamhuri ya Czech, inayoongoza kundi A.
Ronaldo akitoka uwanjani
Kwa Uholanzi, timu hiyo imeonyesha mchezo duni sana, kwa kushindwa katika mechi tatu za makundi, ilhali miaka miwili iliyopita, wao walimaliza katika nafasi ya pili katika fainali ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini.
Itawachukua muda Uholanzi kumsahau Ronaldo, mchezaji nyota wa Real Madrid ya Uhispania, ambaye aliifungia klabu hiyo magoli 60 msimu uliopita, na katika mechi dhidi ya Jumapili alicheza kwa kasi na kwa juhudi na kuwaacha Waholanzi wamezubaa.
PORTUGAL 2-1 NETHERLANDS
Subscribe to:
Posts (Atom)