On Saturday evening, Mena Suvari put a sexy spin on the little black dress when she showed up at the Motion Picture & Television Fund gala in a barely-there Maria Lucia Hohan cocktail frock
Thursday, June 21, 2012
MREMBO WA SIKU
On Saturday evening, Mena Suvari put a sexy spin on the little black dress when she showed up at the Motion Picture & Television Fund gala in a barely-there Maria Lucia Hohan cocktail frock
WALIOONGOZA KWA KUTUPIA KAMBANI KATIKA HATUA YA MAKUNDI EURO 2012
1-(3) Alan Dzagoev wa Urusi ameshatupia kambani mara mpaka kumalizika kwa hatua ya makundi, amekwishapoteza matumaini ya kunyakua daruga la dhahabu kwani Urusi haikufanikiwa kufuzu katika hatua ya robo fainali katika kundi A.
2-(3) Mario Gomez wa Ujerumani amekwisha kutupia kambani mara tatu na ana matumaini makubwa ya kuibuka kidedea kwa kutupia kambani katika michuano ya EURO 2012 baada ya Ujerumani kufuzu katika hatua ya robo fainali baada ya kuibuka namba moja katika kundi B ikijikusanyia pointi zote 9 ikifuatiwa na Ureno iliyomaliza kwa pointi 6.
3-(2) Andriy Shevchenko nahodha wa Ukraine ambao ndio wenyeji wenza wa michuano ya EURO 2012 ametupia kambani mara 2 na kwa bahati mbaya wenyeji hao wametupwa nje ya michuano hiyo baada ya kumaliza katika nafasi ya 3 katika kundi D, Uingereza na Ufaransa zikipenya kwa hatua ya robo fainali.
4-(2) Christian Ronaldo wa Ureno amekwisha tupia mara 2 na ana matumaini makubwa ya kuwa kinara wa mabao katika mashindano hayo baada ya Ureno kufuzu robo fainali baada ya kushika nafasi ya pili katika kundi B nyuma ya Ujerumani.
5-(2) Fernando Torres wa Uhispania ametupia mara 2 na anaweza kuendelea kutupia baada ya timu yake ya Uhispania kufuzu kwa hatua ya robo fainali baada ya kuongoza kundi C.
6-(2) Francesc Fabregas wa Uhispania amekwishatupia kambani mara 2 matumaini ya kuendelea kutupia yanabaki baada ya timu yake kutinga katika hatua ya robo fainali ikiongoza kundi C na sasa atachuana na mhispania mwenzake Fernando Torres katika mbio za kuvaa daluga la dhahabu.
7-(2) Mario Mandzukic wa Croatia ametupia mara 2 na ndio mwisho baada ya Croatia kushindwa kuvuka hatua ya makundi kuelekea robo fainali za michuano ya EURO 2012 ikimaliza katika nafasi ya 3 kundi C
8-(2) Michael Krohn-Dehli wa Denmark ametupia kambani mara 2 na matumaini ya kuvaa daluga la dhahabu yaliyeyuka pale Denmark waliposhindwa kufuzu kwa hatua ya robo fainali baada ya kushika nafasi ya 3 kundi B
9-(2) Nicklas Bendtner wa Denmark ametupia mara 2 na ndio amemaliza hapo baada ya Denmark kuburuzwa nje ya michuano hiyo katika kundi B
10-(2) Olof Mellberg wa Sweden nae amefanikiwa kutupia kambani mara 2 na kutokana na ukweli kwamba Sweden haijafuzu kwa hatua za robo fainali matumaini yake ya kunyakua kiatu cha dhahabu yamezikwa rasmi.
11-(2) Petr Jiracek wa Jamhuri ya Czech ametupia mara mbili na itambidi asubiri miaka minne ijayo ili aendelee kuwania ufungaji bora kwasababu Timu yake imeshindwa kufuzu kwa hatua ya robo fainali za EURO 2012.
12-(2) Vaclav Pilar wa Jamhuri ya Czech nae ametupia kambani mara 2 lakini kutokana na timu yake kushindwa kufuzu kwa hatua ya robo fainali sasa matumaini yake ya kutwaa daluga la dhahabu yameishia hapo.
13-(2) Zlatan Ibrahimovic mshambuliaji wa Sweden ametupia kambani mara 2 na ki ukweli kabisa kama Sweden ingesonga katika hatua ya robo fainali basi huenda angetupia mara nyingi zaidi kutokana na uwezo alionao, lakini sasa ndio basi tena Sweden wameshatupwa nje baada ya kushika mkia katika kundi D.
RATIBA YA MECHI ROBO FAINALI EURO 2012
Uefa Euro 2012 | FIXTURES
| Thursday 21 June 2012 |
| 25 | Czech Republic | v | Portugal |
| Friday 22 June 2012 |
| 26 | Germany | v | Greece | Arena Gdansk |
| Saturday 23 June 2012 |
| 27 | Spain | v | France | Donbass Arena |
| Sunday 24 June 2012 |
| 28 | England | v | Italy | NSC Olimpiyskiy |
| Wednesday 27 June 2012 |
| 29 | Winner Q/F 1 | v | Winner Q/F 3 | Donbass Arena |
| Thursday 28 June 2012 |
| 30 | Winner Q/F 2 | v | Winner Q/F 4 | Warsaw National Stadium |
| Sunday 01 July 2012 FINAL |
| 31 | Winner SF1 | v | Winner SF2 | Olympic Stadium |
FAHAMU ZILIZOINGIA ROBO FAINALI EURO 2012 BAADA YA HATUA YA MAKUNDI
Uefa Euro 2012 | LOGS
Group A
| Pos | Team | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
| 1 | Czech Republic | 3 | 2 | 0 | 1 | 4 | 5 | -1 | 6 |
| 2 | Greece | 3 | 1 | 1 | 1 | 3 | 3 | 0 | 4 |
| 3 | Russia | 3 | 1 | 1 | 1 | 5 | 3 | 2 | 4 |
| 4 | Poland | 3 | 0 | 2 | 1 | 2 | 3 | -1 | 2 |
Group B
| Pos | Team | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
| 1 | Germany | 3 | 3 | 0 | 0 | 5 | 2 | 3 | 9 |
| 2 | Portugal | 3 | 2 | 0 | 1 | 5 | 4 | 1 | 6 |
| 3 | Denmark | 3 | 1 | 0 | 2 | 4 | 5 | -1 | 3 |
| 4 | Netherlands | 3 | 0 | 0 | 3 | 2 | 5 | -3 | 0 |
Group C
| Pos | Team | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
| 1 | Spain | 3 | 2 | 1 | 0 | 6 | 1 | 5 | 7 |
| 2 | Italy | 3 | 1 | 2 | 0 | 4 | 2 | 2 | 5 |
| 3 | Croatia | 3 | 1 | 1 | 1 | 4 | 3 | 1 | 4 |
| 4 | Ireland | 3 | 0 | 0 | 3 | 1 | 9 | -8 | 0 |
Group D
| Pos | Team | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
| 1 | England | 3 | 2 | 1 | 0 | 5 | 3 | 2 | 7 |
| 2 | France | 3 | 1 | 1 | 1 | 3 | 3 | 0 | 4 |
| 3 | Ukraine | 3 | 1 | 0 | 2 | 2 | 4 | -2 | 3 |
| 4 | Sweden | 3 | 1 | 0 | 2 | 5 | 5 | 0 | 3 |
RUNGU LA UEFA LAIANGUKIA ENGLAND KUFUATIA VURUGU ZA MASHABIKI EURO 2012
Mashabiki wa soka wa Uingereza wakilipuka kwa mayowe ya ushindi
Chama cha soka cha England, FA, kimelimwa faini ya Euro 5,000 (sawa na pauni 4000), kutokana na utovu wa nidhamu wa mashabiki wake ambao Ijumaa iliyopita walijaribu kuuvamia uwanja baada ya England kuichabanga Sweden.
Faini hiyo ni kufuatia mashabiki kujaribu kuingia uwanjani baada ya England kuiangushia kipigo Sweden cha 3-2 katika mechi ya kundi D mjini Kiev.
Chama cha FA kimeamua hakitakata rufaa kuhusiana na faini hiyo, na kwa kuwa UEFA haijaitoza FA pesa nyingi, inaashiria kwamba shirikisho hilo la soka ya Ulaya linalichukua tukio hilo kama jambo dogo.
"Tunakubali hatua iliyochukuliwa, na tunalifikiria tukio hili kama jambo ambalo limetatuliwa," taarifa ya FA ilielezea.
Baada ya magoli ya England yaliyotiwa wavuni na Theo Walcott na Danny Welbeck, mashabiki kati ya 20 hadi 30 walivikaribia vizuizi uwanjani, na kutaka kuingia ndani ya uwanja wa Olympic, lakini walifanikiwa kuifikia sehemu ya riadha tu.
Chama cha FA, kikijitetea, kiliweza kutoa ushahidi thabiti wa video mbele ya UEFA na kuonyesha kwamba “uvamizi” huo ulikuwa ni jambo ambalo lilitokea ghafula, na wala mashabiki hao hawakuwa wamepanga kutekeleza kitendo hicho.
Tukio hilo lilichukuliwa kama jambo dogo, na hata afisa wa UEFA katika mechi hiyo hakulitaja katika ripoti yake kuhusiana na mechi.
Chama cha FA pia kimethibitisha kwamba hakuna mashabiki wa England waliokamatwa aidha nchini Poland au Ukraine katika mashindano ya mwaka huu.
Wednesday, June 20, 2012
EURO 2012 ROONEY AWAFUNGASHIA VIRAGO WENYEJI
Rooney akichanja mbuga
Rooney akitupia kambani kwa kichwa goli pekee la Uingereza
Wayne Rooney alirejea dimbani akiwa shujaa wa timu ya England usiku wa Jumanne, baada ya kutokuwepo kwa muda kufuatia adhabu ya UEFA, na bao lake moja dhidi ya Ukraine liliiwezesha timu yake kukwea kileleni katika kundi D.
Kocha wa Uingereza Roy Hodgson akimpongeza Rooney kwa kazi nzuri
Vile vile bao hilo linamaanisha England imeweza kuiepuka Uhispania katika robo fainali, na sasa itacheza dhidi ya Italia.
Rooney, akiwa karibu sana na kipa wa Ukraine, Andriy Pyatov, aliweza kufunga kwa kichwa, mpira uliokuwa wa majaro ya juu kwa juu kutoka kwa nahodha Steven Gerrard.
Licha ya England kuibuka washindi, Ukraine walifanya juhudi kubwa na kupata nafasi nyingi zaidi za kusawazisha, lakini yote hayo hayakufua dafu.
Ukraine walistahili kupata bao wakati mkwaju wa Marko Devic ilikuwa wazi umevuka mstari, lakini kufuatia juhudi za John Terry katika kuondosha mpira huo, pengine mwamuzi alishawishika kwamba kweli mpira haukuvuka msitari.
Ushindi wa Sweden wa magoli 2-0 dhidi ya Ufaransa ulihakikisha kwamba England wanafuzu kuingia robo fainali kama timu iliyoongoza katika kundi D.
Mlinzi wa Uingereza Lescott akichuana vikali na Shevchenko wa Ukraine
Mtifuano kati ya Kacheridi na Welbeck
Tulia weweee, daruga kali la Oleg Husev limemuangukia Ashley Cole
Ukraine 0-1 England
UFARANSA YACHAPWA NA SWEDEN LAKINI YATINGA ROBO FAINALI EURO 2012 USO KWA USO NA SPAIN
Mlinda mlango wa Ufaransa Hugo Lloris akichupa bila mafanikio
Bao lililotupiwa kammbani kwa ustadi na Zlatan Ibrahimovic limeisaidia Sweden kuichapa Ufaransa magoli 2-0 katika mechi ya kundi D usiku wa Jumanne, na kuhakikisha wameisukuma Ufaransa katika nafasi ya pili katika kundi, na pia kuilazimisha kukutana na mabingwa watetezi Uhispania katika mechi ya robo fainali ya Euro 2012.
Wachezaji wa Sweden Wakishangilia ushindi baada ya kuiangushia kichapo Ufaransa
Ufaransa walizidiwa katika mechi hiyo, na Ola Toivonen al-manusra aipatie Sweden bao la kwanza baada ya kuachia nduki iliyogonga sehemu ya nje ya mwamba wa goli.
Hatimaye Ibrahimovic alipata bao kupitia nduki kali kutoka umbali wa yadi 15, baada ya kupenyezewa pande maridadi na Sebastian Larsson.
Olivier Giroud alitupia kwa kichwa na kuiwezesha Sweden kupata bao lao la pili.
Kichapo cha Ufaransa kina maanisha hatua yao ya kucheza pasipo kushindwa katika msururu wa mechi 23 zilizopita tangu waliposhindwa wakiwa nyumbani na Belarus mwezi Septemba mwaka 2010 imesitishwa.
wachezaji wa Ufaransa hawaamini kilichotokea
Adil Rami,Mathieu Debuchy,Phillipe Mexes na Alou Diarra wameloa kwa kichapo
Huo ndio muda mrefu zaidi ulioandikishwa timu kucheza pasipo kushindwa kwa upande wa mechi za kimataifa.
Ufaransa wameshindwa baada ya mechi 24 za kimataifa, na kocha Laurent Blant sio tu atakuwa na wasiwasi katika kupambana na mabingwa wa Ulaya na wa dunia pia, bali pia kuhusiana na timu yake kucheza mchezo wa kiwango duni.
Sweden tayari walikuwa wameondolewa katika mashindano baada ya kushindwa katika mechi zao mbili za mwanzo, lakini nia yao ilikuwa ni kucheza kadri ya uwezo wao kabla ya kurudi nyumbani.
Jumapili iliyopita, wachezaji hao walikataa ushauri wa meneja Erik Hamren wa kupumzika, na badala yake waliamua kuitumia siku hiyo katika kufanya mazoezi zaidi.
Subscribe to:
Posts (Atom)