Tuesday, September 18, 2012

DARAJA LA KIGAMBONI KAZI IMEANZA





















Ujenzi wa Daraja la Kigamboni ukiendelea, na pichani ni daraja la muda

Ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam, umeanza kwa kishindo na jana Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli alitembelea eneo hilo na kuwahimiza makandarasi kukamilisha kazi hiyo kwa muda uliopangwa.

Daraja hilo linalojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), linatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu huku likigharimu Sh214 bilioni.

Ujenzi wa daraja hilo unafanywa na Kampuni ya China Railways Construction na China Major Bridge Engineering Company, zote za nchini China.

Akizungumza na makandarasi hao, Waziri Magufuli aliwataka waongeze kasi ya ujenzi na kuahidi kwamba Serikali itatoa ushirikiano wa hali na mali ili kukamilisha kazi hiyo.

"Nataka niwahakikishie kwamba Serikali itaendelea kuwa bega kwa bega nanyi. Lakini najua nyie ni wachapa kazi, mnaweza kufanya kazi usiku na mchana na kufanya ujenzi uchukue miezi 30 badala ya 36 ya sasa," alisema Dk Magufuli.


Wajomba kazini




Waziri wa Ujenzi Dkt John Magufuli sambamba na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam wakiangalia vifaa vya kampuni inayotengeneza daraja linalounganisha Kigamboni na Kurasini. 

Friday, September 14, 2012

SHILOLE AFUNGUKA ALIVYOBAKWA NA KUPACHIKWA MIMBA


Zuwena Mohamed "Shilole"

Msanii wa Filamu za kibongo "Bongo Movies" na muimbaji wa Nyimbo za kibongo "Bongo Flavour" Mwanadada Shilole amefunguka jinsi jamaa lenye uchu lilivyombaka na kumtoa bikra na ujauzito juu.

Shilole akielezea historia ya maisha yake katika kipindi cha Leo tena kinachendeshwa na Dina Marios kupitia kituo cha Radio cha Clouds Fm cha jijini Dar es salaam, amefunguka kwa kuelezea majaribu aliyokutana nayo kuanzia utoto wake kuelekea ukubwani.
Pamoja na mapito yote ikiwamo kunyanyaswa na kuteswa na wifi na shemeji zake aliowahi kuishi nao kikubwa zaidi katika mapito hayo ni jinsi alivyobakwa na hatimae kutolewa usichana wake"Bikra" na kupata ujauzito.

Majaribu hayo yalimpata mwanadada Shilole alipokwenda kuchota maji majira ya usiku kipindi anaishi na ndugu zake huko Igunga mkoani Tabora. Akielezea mkasa huo Shilole anasema kwa uchungu na hisia kali kuwa siku ya tukio alikuwa amekwenda kisimani kuchota maji." Nilikuwa nimeenda kuchota maji usiku ndipo ghafla akatokea jamaa na kunikamata kwa nguvu, nikajaribu kupiga kelele hazikusikika na akawa ameshatimiza haja yake" Alielezea.

"Nilipata wakati mgumu kurudi nyumbani na kuelezea kilichotokea" aliendelea. Akielezea mkasa huo pamoja na kubakwa alipofika nyumbani na kuelezea tukio hilo alipokea kipondo kitakatifu na akidaiwa kuwa ndio ulikuwa mchezo wake, alijaribu kukataa lakini haikusaidia kitu aliendelea kupata kipondo mpaka mtoa kipondo aliporidhika.

Mwisho wa siku akiwa na ujauzito na kutafakari sana katika maisha magumu, huku akitaka kuitoa lakini mwisho wa siku aliendelea kufanya biashara mitaani na mwisho wa siku akajifungua salama salmini, mtoto huyo wa kwanza anaitwa Rahma.

Mtoto wa kwanza wa Shilole,Rahma

Shilole na Masanja mkandamizaji


Shilole jukwaani


Shilole akiwajibika jukwaani na wacheza shoo wake


Shilole na JB


Shilole katika Pozi matata

AUNT EZEKIEL "KUFULI" NJE NJE HAPANA CHEZEA YEYE


Aunt Ezekiel katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012



Aunt Ezekiel na Steve Nyerere katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012


Kama mgongo ninao..mnasemajeeeee?


Mauno timeee..Aunt akimwaga mauno mbele ya Steve Nyerere katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012

Wednesday, September 12, 2012

HAKUNA KAMA MNYAMA..SIMBA..SIMBA..SIMBA


Nahodha wa Simba Juma K Juma akinyanyua juuu Ngao ya Hisani

Mabingwa wa soka Tanzania Bara, kombe la Urafiki na Super 8 Simba SC wametawazwa rasmi kuwa mabingwa wa Ngao ya Jamii baada ya kuilaza Azam FC kwa mabao 3-2 kwenye mchezo uliopigwa katika dimba kuu la Taifa jijini Dar es Salaam. Mpaka mapumziko, Azam FC walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-1, mabao yaliyowekwa kimiani na John Bocco"Adebayor" na Kipre Tchetche wakati la Simba likitupiwa kambani kwa penati na Mghana Daniel Akuffo. Simba walijipatia ushindi katika kipindi cha pili kupitia kwa mshambuliaji hatari hatari, Emmanuel Okwi akisawazisha na kuwa 2-2 na maafa yakapelekwa kwenye kiwanda cha lambalamba na kiungo mstaarabu Mwinyi Kazimoto akitupia kambani bao la tatu na la ushindi. Mpaka mwisho wa mchezo Simba 3, Azam FC 2 na hivyo Simba sports Club ama wekundu wa msimbazi wakiibuyka mabingwa wa Ngao ya Hisani ambapo sehemu ya mapato ya mtanange huo yatapelekwa katika hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam.

Ngao ya Hisani


Emmanuel Okwi akijaribu kumchomoka beki kisiki wa Azam Agrey Morris


Homoud wa Azam akimfanyia madhambi mchezaji wa Simba.


Umati wa mashabiki wa soka wa Simba waliofika kushuhudia mtanange huo


Mlinda mlango wa Azam Deogratius Munishi"Dida" akinyaka mchomo wa Akuffor


Mgeni rasmi naibu waziri wa kazi na ajira Makongoro Mahanga akimkabidhi Ngao ya hisani nahodha wa simba Juma K Juma


Sekeseke katika lango la Azam


Sekeseke langoni mwa Simba


Beki wa Simba "Chollo" akiangushwa katika eneo la hatari na mlinda mlango wa Azam "Dida"


Wachezaji wa Simba wakienda mapumziko hapa walikuwa wameshalala 2-1 duuh


Hapa Azam


Hapa Simba

Tuesday, September 11, 2012

RATIBA YA MECHI ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2014

RATIBA KIMATAIFA


KWA SAA ZA AFRIKA MASHARIKI (EA, GMT+3)

Tuesday 11 September 2012
New Zealand v Solomon Islands Auckland 010:35
Japan v Iraq Saitama 13:34
Uzbekistan v South Korea Tashkent 16:00
Lebanon v Iran Beirut 17:00
Jordan v Australia Amman 18:00
Czech Republic v Finland Teplice 19:00
United Arab Emirates v Kuwait Abu Dhabi 19:00
Cyprus v Iceland Larnaca 20:00
Israel v Russia Ramat Gan 20:00
Romania v Andorra Bucharest 20:30
Georgia v Spain Tbilisi 20:30
Bulgaria v Armenia Sofia 21:00
Turkey v Estonia Istanbul 21:00
Norway v Slovenia Oslo 21:00
Gabon v Saudi Arabia 21:00
Bosnia-Herzegovina v Latvia Zenica 21:15
Slovakia v Liechtenstein Bratislava 21:15
Austria v Germany Vienna 21:30
San Marino v Montenegro Serravalle 21:30
Serbia v Wales Novi Sad 21:30
Hungary v Netherlands Budapest 21:30
Sweden v Kazakhstan Malmo 21:30
Switzerland v Albania Lucerne 21:30
Republic of Ireland v Oman London 21:30
South Africa v Mozambique Mbombela Stadium 21:30
Italy v Malta Modena 21:45
Northern Ireland v Luxembourg Belfast 21:45
Belgium v Croatia Brussels 21:45
Poland v Moldova Wroclaw 21:45
Greece v Lithuania Piraeus 21:45
France v Belarus Saint-Denis 22:00
England v Ukraine Wembley 22:00
Scotland v Macedonia Glasgow 22:00
Chile v Colombia Santiago De Chile 22:30
Portugal v Azerbaijan Braga 23:00
Uruguay v Ecuador Montevideo 24:30

Wednesday 12 September 2012
Paraguay v Venezuela Asuncion 01:25
Peru v Argentina Lima 03:25
Tahiti v New Caledonia Papeete 08:00

SOMALIA YAPATA RAIS

Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud
 
Bunge la Somalia limemchagua Hassan Sheikh Mohamud kuwa Rais mpya wa nchi hiyo.

Hassan ameshinda kinyang'anyiro hicho kutoka wagombea 22 walioshiriki uchaguzi huo, akiwemo Rais anayeondoka Shariff Sheikh Ahmed na waziri mkuu Abdiweli Mohamed Ali.
Hassan Sheikh Mohamud alishinda kufuatia duru ya tatu ya upigaji kura, ambapo alikuwa anachuana na Rais anayeondoka Shariff Sheikh Ahmed.

Katika raundi ya kwanza Sheikh Ahmed alikuwa amepata ushindi mwembamba wa kura 64 dhidi ya 60 alizopata Sheikh Mohamud.

Kwa jumla wabunge 271 walipiga kura.

Katika duru ya mwisho wabunge wengi waliowaunga mkono wagombea waliochujwa walimuunga mkono Sheikh Mohamud , akapata kura 190 dhidi ya 70 alizopata Rais anayeondoka.

Hii ni mara ya kwanza kwa uchaguzi wa Rais kufanyika katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, tangu kuondolewa kwa serikali ya kijeshi mwaka 1991.

SIMBA USO KWA MACHO NA AZAM TAIFA LEO HII



Leo ndio leo wakati Mrisho Ngassa wa Simba anatarajia kuwa kiini cha utamu wa mchezo wa soka, pale atakaipoikabili kwa mara ya kwanza timu yake ya zamani, Azam FC katika mechi ya Ngao ya Jamii, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Mrisho Ngassa

Simba, mabingwa wa soka Bara walimsajili Ngassa kutoka kwa washindi hao wa pili wa Ligi Kuu Azam. Kabla ya kutua Simba, Ngassa alikuwa akiwaniwa na Yanga ya Dar es Salaam.

Mbali na Ngassa, mwingine ambaye leo huenda akawa kivutio, ni Ramadhan Chombo 'Redondo' atakayekuwa na timu yake mpya Simba.

Redondo ambaye usajili wake ulizua utata, alisajiliwa na Simba kutoka Azam FC, ambao nao awali walimsajili kutoka kwa Wekundu hao wa Msimbazi.

Pambano la timu hizo ni ishara ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu mwishoni mwa wiki hii, kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Ramadhan Chombo "Redondo"

REKODIKwa mwaka huu pekee, Simba na Azam zimekutana mara tano katika mechi za mashindano mbalimbali. Hazijawahi kutoka sare, huku Simba ikishinda michezo mitatu na Azam miwili.

Mechi ya karibuni ni ile ya nusu fainali ya michuano ya Super8, ambapo Simba iliyochezesha kikosi 'B' dhidi ya kikosi kamili cha Azam, ilishinda mabao 2-1.

"Majembe"
Kwa kiasi kikubwa Simba itakuwa na mwonekano tofauti kwa vile ina sura kadhaa mpya kutoka ndani na nje ya nchi.

Miongoni mwa nyota wapya mbali na Redondo na Ngassa kwenye jeshi la Simba leo, wengine ni mshambuliaji wake mpya kutoka Ghana, Daniel Akufo na beki raia wa Mali Komanbill Keita na Mkenya, Pascal Ochieng.

Nayo Azam kama ilivyo kwa wenzao wa Simba, inatarajiwa kuwa na mabadiliko kidogo hasa hasa katika mpangilio wa kikosi na hii ikitokana na kutokuwapo kwa Ngassa na Redondo.

Mfumo:
Wakati Simba itakuwa na kocha mwenye uzoefu na timu hiyo Milovan Cirkovic, Azam itaongozwa na kocha wake mpya Boris Bunjak aliyeukwaa ubosi, baada ya kutimuliwa Mwingereza Stewart Hall.

Timu zote zinatumia mfumo mmoja wa 4-4-2 na hata aina ya soka lao pia linafanana, likipingwa pasi nyingi fupifupi.

Wakizungumzia pambano baina yao, makocha wa timu hizo wakiwa katika hali ya kujiamini walijinasibu kila moja kufanya kweli na kuibuka na ushindi.

"Itakuwa mechi ngumu, lakini ni wakati wa sisi kulipa kisasi baada ya wao kutufunga Kombe la Kagame. Tupo vizuri kiakili na kisaikolojia," alisema Cirkovic.

Naye Bunjak alisema, "Ili ushinde unahitaji maandalizi, na kwa upande wetu tumejiandaa kikamilifu kuhakikisha tunashinda mechi hiyo na kutuongezea morali katika ligi."

Kwa upande mwingine, wachezaji wa kuchungwa zaidi leo ni pamoja na mshambuliaji nyota wa Simba Mganda Emmanue Okwi, kama itakavyokuwa kwa mpachika mabao hatari wa Azam John Boko 'Adebayor'.


Rekodi kamili Simba/ Azam mwaka 2012.

Mapinduzi Cup: Azam 2-0 Simba
Ligi Kuu: Simba 2-0 Azam
Urafiki Cup: Simba 3 -1 Azam (pen)
Kagame Cup: Azam 3- 1 Simba
Super 8: Simba 2- 1 Azam.