Monday, January 28, 2013

CLUB YA USIKU YA KISS YATEKETEA KWA MOTO WATU 233 WAFARIKI DUNIA

Raia wa Brazili wanaomboleza vifo vya watu mia mbili thelathini na watatu waliofariki dunia katika ajali ya moto iliyotokea kwenye ukumbi wa muziki katika mji wa kusini wa Santa Maria.

Maafisa wanasema kuwa wengi wa waathiriwa walikuwa ni wanafunzi waliokufa baada ya kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa .

Wengine zaidi ya mia moja wanapata matibabu hospitalini . Serikali ya Brazil imetangaza siku tatu za maombolezo . Taarifa zinasema kuwa moto huo ulianza wakati waimbaji wa bendi moja walipowasha fataki.


Baadhi ya ndugu ya waliopoteza maisha wakilia kwa uchungu

Maswali sasa yamekuwa yakiulizwa kuhusu usalama wa kumbui za starehe, huku kukiwa na madai kuwa cheti cha huduma za zima moto kilikuwa kimepitwa na wakati. Hili ni jana kubwa la moto kuwahi kuikumba Brazil kwa zaidi ya miongo mitano

Familia za waathiriwa wamekuwa wakiomboleza juu ya majeneza za jamaa zao katika ukumbi wa mamozezi ambao unatuimika kama jumba la kuhifadhia maiti.
Kwa sababu ya heshima kwa waliofariki, serikali iliakhirisha sherehe iliyotarajiwa kufanyika leo Jumatatu katika mji mkuu, Brasilia, kuadhimisha siku 500, kabla ya kombe la dunia kungo'a nagna nchini humo mwaka ujao.

Mazishi ya kwanza mjini Santa Maria yanatarajiwa kufanyika leo , kwa mujibu wa magazeti ya nchi humo.

Maafisa wa utawala wametoa majina ya waathiriwa hao,230 huku maiti watatu wakisalia kutotambuliwa.

Kulingana na taarifa za kituo cha televisheni cha Globo,wengi wa waathiriwa walikuwa kati ya umri wa miaka16 na 20.

Zaidi ya watu 100 wanapokea matibabu baada ya kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa.

Watu wakitimua mbio wakati moto ukiendelea kuwaka ukumbini hapo






Vikosi vya zima moto vikijaribu kuzima moto katika club ya disco ya Santa Maria








































Thursday, January 24, 2013

ANAMILIKI MAGARI YA KIFAHARI 7,000 YENYE THAMANI YA DOLA BILLIONI 7

Sultani wa Brunei ni mpenzi mkubwa wa magari ya kifahari, anamiliki magari ya kifahari yapatayo 7,000 yenye thamani ya dola za kimarekani billioni 7 ambayo yamepaki katika garage kubwa katika kasri lake.  Ili aweze kuendesha magari yote bila kurudia hata siku moja itamchukua miaka 20 kuweza kumaliza kuyaendesha magari yote..mhhh mbongo wa kawaida baiskeli ni kitendawili hayaaa!!
Fun & Info @ Keralites.net
Sultani wa Brunei

Kwa mujibu wa gazeti mashuhuri la Daily Mirror la tarehe 30 juni 2010, anamiliki magari yafuatayo;
604 Rolls Royce’s, 574 Mercedes-Benzes,
452 Ferraris,

382 Bentleys,
209 BMWs,
179 Jaguars,
134 Koenigseggs,

21 Lamborghinis,
11 Aston Martins,
and 1 SSC.

Fun & Info @ Keralites.net
Gereji ya magari ya Sultani kwa juu

Fun & Info @ Keralites.net
Kwa mbele

Fun & Info @ Keralites.net
Kwa ndani

Fun & Info @ Keralites.net
SSC ultimate aero  ($740,000 )
 

Fun & Info @ Keralites.net
Leblanc Mirabeau ($765,000 )

Fun & Info @ Keralites.net
Koenigsegg CCX ($1.1 Million )

 
Fun & Info @
Keralites.net
Koenigsegg CCXR ($1.3 Million)

Fun &
Info
@ Keralites.net


Maybach Landaulet ($1.4 Million )

Fun & Info
 @ Keralites.net
Lamborghini Reventon ($1.42 Million)

Fun & Info @ Keralites.net
Lamborghini Reventon Roadster ($1.56 Million )

Fun & Info @ Keralites.net
Pagani Zonda Cinque Roadster ($1.8 Millions)

Fun & Info @
Keralites.net
Bugatti Veyron 16 4 Grand Sport 57 ($1.67 Million )

Fun & Info @
Keralites.net
 Koenigsegg Trevita  ($2.21 Million )




Wednesday, January 23, 2013

TUNISIA YAICHAPA ALGERIA

Tunisia imeizamisha Algeria 1-0 katika mchezo uliopigwa katika dimba la Royal Bafokeng na kuhudhuriwa na watazamaji wapatao 8,000.
Katika mtanange huo timu zote zilicheza kandanda safi na la kuvutia na watazamaji kuwa na kiu ya kuona bao kwa dakika zote 90 kabla ya Y M'sakni kuondoa mzimu wa droo katika mashindano hayo alipotupia bao katika dakika ya 90.



Kambaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Tazama mechi yote

KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA IVORY COAST YAIANGAMIZA TOGO

Mechi za awali za kombe la mataifa ya afrika zimemalizika jana huku kila timu ikiwa imeshacheza mchezo mmoja, Timu ya soka ya taifa ya Ivory Coast ikiwa imesheheni nyota "ma-father" wanaocheza soka la kulipwa kama Drogba,Yaya Toure,Kolo Toure,Didier Zokora"Maestro",Ya Konan,Solomon Kalou,Emmanuel Eboue na Gervinho iliweza kuiadabisha timu ya taifa ya Togo iliyokuwa ikiongozwa na Emmanuel Adebayor kwa bao 2-1 katika mchezo uliopigwa katika dimba la Royal Bakofeng na kushuhudiwa na watazamaji wapatao 2,000.

Ilikuwa katika dakika ya 7 tu ya mchezo pale Yaya Toure alipotupia kambani goli la kwanza kabla ya Jonathan Ayite kusawazisha katika dakika ya 45 sekunde chache kabla ya mapumziko. Timu zote zilirudi uwanjani na nguvu mpya kila moja ikitafuta ushindi lakini katika mchezo huo uliotawaliwa zaidi na nyota wa Ivory Coast na dakika 3 kabla mchezo kumalizika mshambuliaji "mchoyo" wa Arsenal Gervinho aliweza kuipatia Ivory Coast goli la pili na la ushindi. Mpaka mwisho Ivory Coast 2-1 Togo.

Yaya Toure akishangilia goli na wachezaji wenzake

Adebayor chini ya ulinzi mkali

Togo wakishangilia goli la kusawazisha


Drogba akionesha udambwidambwi..

Gervinho wa Ivory Coast akitiririka na gozi la ng'ombe


Gervinho akishangilia goli
Ivory coast 2-1 Togo

Monday, January 21, 2013

SIMBA YATAKATA OMAN YAIBANJUA AHLI-SIDAB,NYOSSO APATA TIMU OMAN

Mabingwa wa soka Tanzania bara, Simba s.c "wekundu wa msimbazi" wamepata ushindi wao wa kwanza nchini Oman baada ya kuiadabisha Ahli Sidab kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Oman ambako Simba wamepiga kambi kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Viungo Kigi Makassy na Amri Kihemba walikuwa mashujaa kwa upande wa Simba baada ya kutupia kambani mabao katika kila kipindi cha mchezo huu.
Makassy alitupia kambani bao la kwanza dakika 21 kabla ya kutolewa nje baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Amri Kiemba ambaye aliingia na kutupia kambani bao la pili na la ushindi katika dakika ya 68.

Wakati huohuo, baada ya kumrudisha kundini beki Juma Nyosso wiki iliyopita, uongozi wa Simba sasa upo mbioni kumuuza beki Juma Nyoso nchini Oman.
Simba kwa sasa ipo kambini Oman na viongozi wake wapo kwenye mazungumzo na wakala Said Ally aliyeonyesha nia ya kumtafutia timu Nyoso.

Nimeshazungumza na Simba na kila kitu kinaenda sawa, tukifikia mwafaka nitaweka wazi ni timu gani atachezea na kiasi ambacho atauzwa, alisema wakala huyo.

Simba wiki iliyopita walimaliza tofauti zao na Nyoso aliyedaiwa kushuka kiwango na kumlazimisha kuchezea timu B, jambo lililopingwa vikali na beki huyo.


Juma Nyosso

MATOKEO KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA 2013

Kombe la Mataifa ya Afrika |MATOKEO


20 January
Mali1 - 0Niger
S Keita (83)
Nelson Mandela Bay Stadium Attendance (20000)
20 January
Ghana2 - 2Congo DR
E Agyemang-Badu (39)
K Asamoah (48)
TM Mputu (52)
D Mbokani (pen 68)
Nelson Mandela Bay Stadium Attendance (7000)
19 January
Angola0 - 0  Morocco
National Stadium Attendance (25000)
19 January
South Africa 0 - 0  Cape Verde Islands
National Stadium Attendance (50000)

TOTTENHAM YAIDAI MAN U "CHENJI" DAKIKA YA 90

Washikilia usukani wa ligi kuu ya England, Manchester United imeambulia pointi moja baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Tottenham.

Mshambuliaji Robin Van Persie aliiwezesha timu yake ya Manchester United kuongoza kipindi cha kwanza baada ya kufunga bao katika dakika ya 25.

Van Persie alipata goli hilo akiunganisha kwa kichwa krosi ya Tom Cleverly baada ya Welbeck kufanya kazi nzuri.

Man United wakiamini kuwa tayari wamepata ushindi katika mechi hiyo,Tottenham waliendelea kudai Chenji kwa kulisakama lango la Man United na  katika dakika ya 90 ya mtanange huo Climp Dempsey aliwanyanyua mashabiki wa Tottenham waliofurika katika dimba la White Hart Lane.Mpambano huo ulishuhudiwa na mashabiki wapatao 35,956

Matokeo hayo bado yanaiacha Manchester United kuendelea kushika usukani wa ligi hiyo ikiwa na pointi 56, huku ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi 51.

Tottenham iko katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 41, pointi nne nyuma ya Chelsea yenye pointi 45, ikikakalia nafasi ya tatu ya ligi kuu ya England.

Timu zote nne mpaka sasa zimeshacheza mechi 23.

Van Persie akipiga kichwa kilichoelekea moja kwa moja wavuni

Robin Van Persie akishangilia goli

Mshikemshike



Dempsey akishangilia goli baada ya kubadili matokeo katika dakika ya 90
Tottenham 1-1 Man U