Tuesday, June 21, 2011

MAONESHO YA MAGARI YA MBWEMBWE YAFANA LEBANON










THIERRY HENRY ALIMWA KADI NYEKUNDU KWA KUMPIGA MOFFAT.

Thierry Henry alifunga goli lake la nane kwa msimu huu wakati timu yake ya New York ilipotoka sare ya 3-3 na Portland jumapili iliyopita, na kumfanya kuongoza kwa ufungaji katika ligi ya Marekani sambamba na London Donovan. Katika mechi hiyo Henry alilimwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kichogoni mchezaji wa Portland Moffat baada ya kutokea majibizano baina ya wawili hao.
Kwa kile kilichoonekana kuwa ni utani wachezaji hao walipatana laki ni muamuzi wa mechi hiyo alionekana akijadiliana na mshika kibendera na aliporudi uwanjani akampatia Henry kadi nyekundu na kumpa Moffat kadi ya njano, kitendo hicho kiliwapandisha jazba wachezaji wa New York na walionekena kumzonga mwamuzi lakini Henry kwa upande wake alipeana mikono na wachezaji wa Portland na mwisho alimpa mwamuzi mkono na kutoka nje. Kitendo hicho cha mwamuzi kumpa Henry kadi kilikemewa vikali na uongozi wa New York na katika mtandao wa New York malalamiko yalimshutumu mwamuzi kwa kuchezesha vibaya mechi hiyo,ambapo uongozi ulilalamikia timu ya Portland kwa kucheza faulo nyingi na mwamuzi aliwapendelea,uongozi wa New York ulikiambia chama cha soka Marekani kutowaendekeza waamuzi kama hao kuchezesha mechi kwani wanadidimiza soka la Marekani.

Monday, June 20, 2011

MIJI IMARA KIUCHUMI MAREKANI.

LITTLE ROCK,Arkansas.
Little Rock ni mji wenye utajiri mkubwa ikihusisha kuwa na Hospitali kubwa,Taasisi za matibabu na pia mji huu una idadi kubwa ya shule na vyuo vyenye kutoa elimu bora. mji una idadi ndogo ya watu wasio na ajira kwani ni  7.7% kiasi ambacho ni kidogo ukilinganisha na kiasi cha Taifa ambacho idadi ya wasio na ajira ni 9.7% . Chuo cha sayansi ya madawa cha Arkansas ndio kinatoa ajira kwa jamii kwa idadi kubwa na masaa ya kufanya kazi ni Dakika 17.6, mji huu una wakazi 189,515. ukiwa  ni mji wa kwanza kwa utajiri, 29 kwa elimu, 22 kwa afya , 61 kwa usalama.

BILLING,Montana.
Mji huu una idadi ya wasio na ajira kwa 6%. una idadi ya watu wanaofikia 103,994. Ni mji wa 65 kwa kutoa elimu bora, wa 41 kwa huduma za afya ,59 kwa kuwa na usalama, ni namba 2 kwa uchumi mzuri. Utajiri wa mji huu unaletwa na hifadhi za Yellowstone,Grand Teton na Little Bighorn.Muda wa kufanya kazi ni dakika 15.

SIOUX FALLS,South Dakota
Mji huu una mbuga na hifadhi ndani ya eneo la heka zipatazo 2913, Mji huu unaonekana kama ndio kituo cha utamaduni, Na ni mji wenye idadi ndogo ya uhalifu,msongamano mdogo wa magari na idadi ndogo ya uchafuzi wa mazingira huku ukiwa na uwiano wa 13/1 ya wanafunzi na kuufanya kuwa mji bora kwa elimu. Idadi ya watu inafikia 154,997. Ni mji wa 60 kwa elimu bora, 3 kwa afya bora na huduma za afya, 45 kwa usalama, 3 kiuchumi.

SALT LAKE CITY,Utah.
Mji huu una idadi ya watu inayofikia 181,698. Masaa ya kufanya kazi ni dakika 20, ni mji wa 59 kwa kutoa elimu bora, 27 kwa huduma nzuri za afya, 75 kwa usalama, na wa 4 kwa uchumi. Uwapo Salt lake usafiri kufika popote pale kwa urahisi na uhakika ambapo kutoka mjini mpaka uwanja wa ndege ni dakika 10 tu na usafiri upo kila kona ya mji.

TULSA,Oklahoma.
Mji huu una idadi ya watu wapatao 385,635. Muda wa kufanya kazi ni dakika 17.8, Ni mji wa 5 kwa utajiri, 57 kwa usalama, 52 kwa huduma bora za afya, wastani wa walimu nawanafunzi ni 15/1. 



TETESI USAJILI LIGI KUU UINGEREZA.

Everton waamini wanaweza kuipiku Bayern Munich kumnasa mjapani Usami.

Roma wapo tayari kupandisha dau kufikia paundi za uingereza milioni 8 kumnasa Clichy na kuipiku Liverpool ambayo nayo inamuwania beki huyo wa Arsenal.

Wolves waungana na Sunderland kumuwania Gardner.

Wolves wamhitaji Konchesky toka Liverpool.

Ron Green kwenda Celtic.

Lua lua akataa aamua kuitosa Southampton.

Stoke City wakamilisha usajili wa wachezaji wawili kutoka Birmigham Cameron Jerome na Scott Dann kwa paundi za uingereza milioni 11 kwa wote wawili.

Yobo kwenda Celtic kwa mkopo,taarifa kamili wiki hii.

Guus Hiddink kutua Chelsea,taarifa zaidi wiki ijayo.

Preston kumsajili Chris Iwelumo kutoka Barnley kwa paundi a uingereza 450,000 na Burnley kumsajili Keith Treacy kutoka Preston kwa paundi milioni 1.4.

Liverpool kuwasajili Nzogbia,Zapata,Downing, Adam and Wickham na kuwauza Konchesky,Kyriakos,Poulsen,B Jones,N'gog na pia huenda wakamuuza Aquillan.

Alex Smithies asaini Burnley kwa paundi milioni 1.5 baada ya mazungumzo marefu na Eddie Howe jana mchana na kulipwa paundi 6000 kwa wiki na mkataba wa miaka mitatu.

Newcastle kukamilisha usajili wa Gabriel Agbenlahor ijumaa hii kwa kitita cha paundi za uingereza milioni 7.

Abdoulaye Meite kutua Norwich, pia kumchukua Stephen Caldwell bure.

Reo-Cooker kurudi uingereza na huenda akasaini Westham.

Steve Morisson toka Millwall kwenda Norwich City

Jamie O'hara toka Tottenham kwenda Wolves.

Christophe Samba toka Blackburn kwenda Arsenal.

Ali Al-Habsi toka Bolton kwenda Wigan.

James MarCathy toka Wiga kwenda Liverpool.

Ashley Young toka Aston Villa kwenda Man United.

Matt Jarvis toka Wolves kwenda Aston Villa.

Peter Crouch toka Tottenham kwenda Sunderland.

David Vaughan toka Blackpoolkwenda Albion.

Scott Parker toka Westham kwenda Tottenham.

Rob Green toka Westham kwenda Arsenal.

Carlton Cole toka Westham kwenda Stoke City.

Frederic Piquionne toka Westham kwenda Albion.

DJ Campbell toka Blackpool kwenda Sunderland.

David Jones huru kwenda Stoke City.

Shane Long toka Reading kwenda Newcastle.

Samir Nasri toka Arsenal kwenda Man United.

Emmanuel Adebayor toka Man City kwenda AC Milan.

Kaka toka Real Madrid kwenda Man City.

Mathew Mills toka Reading kwenda Norwich City.

Sam Vokes toka Wolves kwenda Southampton.

Adam Lallana toka Southampton kwenda Newcastle United.

Alex Oxlade-Chamberlain toka Southampton kwenda Arsenal.

Niklas Bendtner toka Arsenal kwenda Juventus.

Richard Dunne toka Aston Villa kwenda Wolves.

Federico Macheda toka Man United kwenda West Bromwich Albion.

Danny Graham toka Watford kwenda Queen's Park Rangers.

Kayle Walker toka Tottenham kwenda Queen's Park Rangers.

Gabriel Obertan toka Man United kwenda Swansea City.

Jimmy Kebe toka Reading kwenda Swansea City.

Defoe kwenda Newcastle kwa paundi za uingereza milioni 8.9

Emily Heskey kurudi Leicester kwa paundi za uingereza 500,000.

Sevilla watoa ofa ya paundi za uingereza milioni 8 kumnasa Denilson toka Arsenal.

KAMA BEI YA PETROLI ITAENDELEA KUPAA JUU,MAMBO HUENDA YAKAWA HIVI.

Saturday, June 18, 2011

PICHA YA LEO

WACHEZAJI GHALI NA WANAOLIPWA ZAIDI 2011.

Unaweza kuwaita kuwa ndio wachezaji ghali na matajiri,vilevile ukawaita ndio wachezaji bora zaidi duniani. Kwa hivi sasa wachezaji ghali zaidi ni kama ifuatavyo;

1} CHRISTIAN RONALDO, Huyu ndiye mchezaji ghali zaidi aliyegharimu uhamisho wa paundi za uingereza milioni 80, kutoka Man U kwenda Real Madrid. Huu ndio uhamisho ghali zaidi kuwahi kutokea katika soka ambao mpaka sasa bado ni gumzo.

2} RICARDO KAKA, Huyu anasadikika kuwa ndiye mchezaji bora na mwenye kasi aliyewahi kutokea katika ulimwengu wa soka. Ambapo aliigharimu Real Madrid kitita cha Paundi za uingereza milioni 56 kumng'oa katika kikosi cha AC Milan ya Italy. Pamoja na kuwa na kipaji na ujuzi, Kaka hakuweza kuonesha makeke yake akiwa Real kutokana na kuwa majeruhi mara kwa mara lakini hamna shaka anaweza kurudi katika kiwango chake pale atakaporejea katika hali yake.
3} ZLATAN IBRAHIMOVIC, Huyu alikuwa ni mmoja kati ya wachezaji bora duniani,na alikuwa katika kiwango cha hali ya juu katika kipindi cha mwaka 2007-2008 katika msimu wa ligi ya Italy. Alinyakuliwa na Barcelona kwa kitita cha paundi za uingereza milioni 60.7 kutoka Inter Milan ya Italy.

4} FERNANDO TORRES, Huyu ni mmoja kati ya wachezaji bora katika ligi ya Uingereza ambapo mwaka 2007-2008 alishika nafasi ya pili kama mchezaji bora wa ligi kuu Uingereza namba moja akiwa ni Christian Ronaldo. Torres alinyakuliwa na Chelsea ya Uingereza kwa kitita cha paundi za Uingereza milioni 50 kutoka Liverpool pia ya Uingereza. Pamoja na kutokufanya vizuri akiwa Chelsea Torres bado ananafasi ya kufanya vizuri akiwa na Chelsea katika msimu ujao wa ligi.
5} ZINEDINE ZIDANE, Huyu ni mmoja kati ya wachezaji wenye ujuzi "skillfull" duniani, amliichezea Ufaransa mara mbili katika kombe la dunia na kuiwezesha Ufaransa kutinga fainali mwaka 2006.

6} LUIS FIGO, Huyu alikuwa ni ni mchezaji mzuri sana na inaaminika katika kipindi chake alikuwa mchezaji bora duniani ambapo aliigharimu Barcelona kumng'oa kutoka Real Madrid kwa paundi za Uingereza milioni 37.

7} HERNAN CRESPO, Crespo alikuwa ni mchezaji wa hali ya juu kipindi Figo yupo kwenye chati,na inaaminika Crespo ni kati ya wachezaji bora duniani ambapo alinunuliwa kwa paundu za Uingereza milioni 35.5 na timu ya Lazio ya Italy akitokea Parma pia ya Italy.

8} ANDY CAROLL, Huyu alipata uhamisho sio siku nyingi sana ni 2011 kutoka Newcastle kwenda Liverpool zote za Uingereza kwa kitita cha paundi za Uingereza milioni 35.
9} DAVID VILLA, Huyu hivi sasa ndio yupo katika kiwango chake,alipata kiatu cha dhahabu na akiwa ni miongoni wa wafungaji bora katika fainali z kombe la dunia 2010 akiichezea Uhispania. Alinyakuliwa na Barcelona Uhispania kwa kitita cha paundi za Uingereza milioni 34.2 akitokea Valencia pia ya Uhispania. Villa anategemewa kufanya mazuri zaidi kama atabaki Barcelona.
10} GIANLUIGI BUFFON, Ukiongelea golokipa bora katika historia ya soka....Buffon anasadikika kuwa golikipa bora zaidi duniani baada ya Oliver Kahn wa Ujerumani. Huwa haijalishi ni timu gani anachezea ana uwezo wa kupangua michomo ambayo huwafanya wachezaji wenzake warudi mchezoni, alisajiliwa na Juventus kwa paundi za Uingereza milioni 32.6 akitokea Parma zote za Italy. Buffon amemuoa mwanamitindo wa Czeck Seredova.