Thursday, August 2, 2012

Artist-RICH MAVOKO Song-SILALI

MRISHO NGASSA...PWAAAAH MSIMBAZI


Mrisho Ngassa

Mabingwa wa kabumbu nchini, Simba wamewabwaga watani wao Yanga katika vita ya kumwania winga wa Azam FC, Mrisho Ngassa, na sasa nyota huyo anatarajia kutinga kwa mara ya kwanza uzi wa rangi nyekundu na nyeupe msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.Ngassa aliyekuwa pia akiwania na klabu yake iliyompa chati, mabingwa wa Kombe la Kagame, Yanga ya Dar es Salaam, amejiunga na Wekundu hao wa Msimbazi kwa mkopo.

Awali ilitegemewa kuwa, Ngasa aliyechoka kuendelea kukosa namba kikosi cha kwanza cha Uwanja wa Chamazi, angejiunga na timu yake ya zamani ya Yanga.

Azam ilitangaza kupitia tovuti yao mwanzoni mwa wiki hii, kwamba iko tayari kumuuza Ngasa kwa timu yoyote itakayofika dau la dola 50,000.

Taarifa hiyo ya kwenye tovuti ilikuja siku chache tangu Ngasa aonekana akiibusu nembo ya klabu ya Yanga wakati akishangilia bao kwenye mechi ya Kombe Kagame.

Katika ofa yao, Yanga ilisema ingekuwa tayari kumtwaa mchezaji huyo kwa dau la Sh20 milioni, huku wapinzani wao Simba wakija na dau la Sh25 milioni.

Lakini mwenyewe Ngasa alipoulizwa kuhusu kupelekwa kwa mkopo Simba, alionekana kushangazwa na habari hizo na kusema hafahamu lolote.

"Na mimi nimesikia watu wanasema kwamba natakiwa kwenda Simba kwa mkopo. Naloweza kukuambia ni kwamba, mimi naheshimu mkataba wangu," alisema Ngasa.

"Sijaambiwa lolote na viongozi wangu, kwa maana hiyo basi mimi bado mchezaji halali wa Azam mpaka itakapotangazwa tofauti."

Meneja wa Azam, Patrick Kahemela aliithibitishia Mwananchi jana kuwa, klabu yao imeamua kumpeleka kwa mkopo Ngasa klabu ya Simba.

"Kwa sasa bado ana mkataba na Azam, tumeamua kumtoa kwa mkopo kwenda Simba mpaka mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu," alisema Kahemela.

Kahemela alisema ameshangazwa na hatua ya Yanga kushindwa kufika kwenye mazungumzo ya kumsajili mchezaji huyo kama walivyokuwa wamepanga.

"Yanga walikuwa wa kwanza kuleta ofa yao, na sisi tuliwapa wao zaidi nafasi kuliko Simba, lakini walipopaswa kuja kwa ajili ya mazungumzo ya mwisho hawakutokea," alisema.

Aliongeza: "Yanga walifanya mzaha katika suala hili. Tulimtafuta Katibu Mkuu [Mwesigwa Celestine] lakini hakuonyesha kujali."

Taarifa za Ngasa kutua kwa mkopo Simba pia zilithibitishwa na Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Godfrey Nyange.

"Tumemalizana na Azam kuhusu suala la Ngasa. Huyu sasa ni mchezaji wetu, atasaidia kuimarisha safu ya ushambuliaji," alisema Kaburu.

Monday, July 30, 2012

P SQUARE Ft RICK ROSS-Btfl Onyinye.

PICHA ZA MATUKIO OLYMPIC 2012

Olympics Day 2 - Basketball
Mchezaji wa Kikapu wa Ufaransa Ronny Turiaf akitupiamo kikapu katika mechi baina ya Ufaransa na Marekani.

Olympics Day 2 - Cycling - Road
Shabiki mtoto wa timu ya Taifa ya Uingereza ya baiskeli kwa upande wa wanawake akiwa katika swaga za kiuzalendo zaidi.

Olympics Day 2 - Gymnastics - Artistic
Jennifer Pinches wa Uingereza akifanya vitu vyake katika raundi za mtoano mchezo wa Artistic Gymnastics kwa upande wa kina dada.
Olympics Day 2 - Badminton
Chen Xu anaepiga mpira wa unyoya na nyuma yake Jin Ma wa China katika mpambano dhidi ya Peng Soon Chan na Liu Ying Gohon wa Malaysia katika mchezo wa Mchanganyiko ndani ya dimba la Wimbley Arena.

Olympics Day 2 - Weightlifting
Valentin Hristov wa Azerbaijan akibeba kitu kizito Ndani ya uwanja wa Excel

Olympics Day 2 - Volleyball
Michal Lasko(7) na Alessandro Fei(14) wa Italia wakijaribu kuzuia mchomo kutoka kwa Zbigniew Bartman(9) wa Poland katika mchezo wa Volleyball uliopigwa ndani ya dimba la Earls Court jijini London.

Olympics Day 2 - Volleyball
Mashabiki wa Poland wakilipuka kwa shangwe katika mechi ya Volleyball kati ya Poland na Italia.

Olympics Day 2 - Basketball
Mke wa Rais Barrack Obama wa Marekani,Michelle Obama akimtuliza mzuka Kobe Bryant wakati timu ya mpira wa kikapu ya Marekani ilipotifuana na Ufaransa.

Olympics Day 2 - Basketball
Kobe Bryant wa timu ya mpira wa kikapu ya Marekani akipambana vilivyo na Tony Parker wa Ufaransa timu hizo zilipooneshana ubabe katika kiwanja cha Basketball Arena jijini
London.

Olympics Day 2 - Basketball
Kobe Bryant na LeBron James wa Marekani wakifurahia jambo katika mpambano wa Mpira wa kikapu baina ya miamba miwili ya Marekani na Ufaransa.

Olympics Day 2 - Around the Games
Mashabiki wakiwa wamepigilia miwani zenye kuonesha mwaka 2012 kuashiria michuano ya Olimpiki jijini London Uingereza.

Olympics Day 2 - Cycling - Road
Lucy Martin (Katikati) wa Uingereza akivuka mstari wa mwisho kumaliza mbio za Baiskeli kwa wanawake jijini London.

Olympics Day 2 - Around the Games
Mashabiki wa michezo mbalimbali wakiingia katika viwanja vya Olympic Park,jijini London nchini Uingereza

Olympics Day 2 - Beach Volleyball
Zara Dampney na Shauna Mullin wa Uingereza wakipongezana katika mechi ya mchezo wa Volleyball ya Ufukweni ndani ya Horse Guards Parade jijini London.

Olympics Day 2 - Canoe Slalom
Sideris Tasiadis wa Ujerumani akichanja mbuga katika mchezo wa kukimbiza mashua yanayofanyika Lee Valley White Water Centre jijini London.

Olympics Day 2 - Table Tennis
Kasumi Ishikawa wa Japan akirudisha mchomo katika mechi ya mpira wa meza(Table Tennis) dhidi ya Li Qiangbing wa Austria ndani ya uwanja wa Excel jijini London.

Olympics Day 2 - Swimming
Kushoto kwenda kulia, Nick Thoman (U.S.A),Matthew  Gravers(U.S.A) na Ryosuke Irie(Japan) wakimalizia ngwe katika mchezo wa Kuogelea uliofanyika Aquatics Centre jijini London.

Olympics Day 2 - Sailing
Lain Percy na Andrew Simpson wa Uingereza wakitiririka katika mchezo wa majahazi huko Weymouth &Portland Venue

Olympics Day 2 - Sailing

Friday, July 27, 2012

KABURU ALIETAKA KUMUONDOA MANDELA DUNIANI ATIWA HATIANI

Mike Du Toit amepatikana na hatia ya kutaka kumuua Nelson Mandela mwaka 2002
Mike Du Toit akiwa mahakamani

Nelson Mandela

Mtu aliyepanga njama za kutaka kumuua rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amepatikana na hatia.

Mahakama ya Pretoria imemtia hatiani kiongozi wa kundi la -Boeremag linaloamini kuwa mtu mweupe ni bora kuliko mtu mweusi alipatikana na hatia ya kupanga kumuua Mandela mwaka 2002.

Bwana Mike du Toit ndiye aliyepanga milipuko tisa katika eneo la Soweto mjini Johannesburg mwaka 2002.

Kiongozi huyo wa kundi la ki-baguzi ni mtu wa kwanza kupatikana na hatia tangu utawala wa wengi uanze mwaka 1994 nchini Afrika kusini.

Wataalamu wa mambo wanasema kuwa bado kuna hali ya kutopendana kati ya watu wa rangi tofauti nchini Afrika kusini.

Hata hivyo kundi kama la Boeremag,inayomaanisha Nguvu za Makaburu miongoni mwa Makaburu ,halina ufuasi mkubwa.

Mahakama hiyo ya Pretoria imempata Du Toit, ambaye alikuwa msomi baada ya kusikiliza kesi hiyo kwa miaka tisa.

Thursday, July 26, 2012

AZAM YATINGA FAINALI KOMBE LA KAGAME

Timu ya soka ya Azam F.C ya jijini Dar es salaam imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Kagame baada ya kuitandika AS Vita ya DRC katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa katika dimba kuu la Taifa jijini Dar es salaam.
AS Vita ndio walikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za Azam kabla ya John Bocco"Boko haram" kutupia kwa kichwa baada ya krosi maridhawa ya Erasto Nyoni. Mtanange ulikuwa mkali na wakushambuliana kwa zamu na ndipo mchezaji machachari alieingia kipindi cha pili Mrisho Halfan Ngassa alipotupia kambani bao la pili katika dakika za majeruhi na kuipeleka Azam fainali ya michuano ya Kagame.
Sasa Azam ambayo iliwaondosha mabingwa wa soka Tanzania bara Simba S.C katika mchezo wa robo fainali kwa mabao 2-1, Inabidi isubiri mshindi wa nusu fainali nyingine ambayo inaendelea hivi sasa kati ya Yanga na APR ni dakika ya 8 hakuna timu iliyoliona lango la mwenzake.

VIWANJA VITAKAVYOCHIMBIKA OLYMPIC 2012



Aquatics Centre
Olympic Park, Eneo hili linajumuisha viwanja vitakavyotumika katika mashindano ya Olympiki 2012 jijini London nchini Uingereza. Olympic Park inajumuisha Aquatics Centre,Basketball Arena,BMX Track,Copper Box,Olympic Stadium,Riverbank Arena,Velodrome na WaterPolo Arena.

OLYMPIC STADIUM

Olympic Stadium una uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000 wakiwa wamekaa. Ulikamilika Machi 2011 na mpaka sasa Mashindano 42 yameshafanyika uwanjani hapo.

AQUATICS CENTRE
Aquatics Centre
Uwanja huu wa ndani una uwezo wa kuingiza watazamaji 17,500 ambao ulimalizika kujengwa julai 2011. Michezo ni pamoja na Kuogelea,Kuzamia.

BASKETBALL ARENA



Basketball Arena una uwezo wa kuingiza watazamaji 12,000 wakiwa wamekaa na unatumika kwa michezo ya Mpira wa kikapu(Basketball) na mpira wa mikono(Handball)

COPPER BOX



Copper Box una uwezo wa kumeza watazamaji 7,000 na michezo inayohusika humo ni Mpira wa mikono(Handball) na Modern Pentathlon


WATER POLO ARENA


Water Polo Arena una pakia watazamaji 5,000 mchezo ni mmoja tu wa Water Polo


BMX TRACK


Khalen Young - LOCOG Test Events for London 2012 - BMX UCI World Cup
Khalen Young - LOCOG Test Events for London 2012 - BMX UCI World Cup

BMX Track inakusanya watazamaji 6,000 na mchezo ni wa Kukimbiza baiskeli aina ya BMX


RIVERBANK ARENA



Riverbank Arena una uwezo wa kuwakalisha chini watazamaji 16,000 na mchezo ni Mpira wa magongo(Hockey)


RICOH ARENA




Ricoh Arena ni uwanja wa Coventry City ya jijini London, uwanja una uwezo wa kukusanya watazamaji 32,609 wakiwa wameweka makalio chini, mchezo ni mpira wa miguu pekee.


VELODROME



Veldrome unaingiza watazamaji 15,000 mchezo ni Baiskeli


EARLS COURT


Earls Court wanaingia watazamaji 16,000 mchezo ni Volleyball


ETON DORNEY


The Australian Ladies & Mens Coxed Eights squad practise during rowing training at Eton Dorney on July 24, 2012 in London, England.
Eton Dorney watazamaji 20,000 wanaweza kuangalia michezo ya Rowing na Canoe sprint.


EXCEL



Excel ni uwanja wa ndani wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 10,000, michezo ni Ngumi(Boxing),Kunyanyua vitu vizito(Weightlifting),Table Tennis,Fencing,Judo,Taekwondo,wrestling(Mieleka)


GREENWHICH PARK


Katika viwanja hivi watazamaji zaidi ya 23,000 wanaweza kushuhudia mbio za farasi na michezo mingine


HADLEIGH FARM




Hadleigh farm watazamaji wapatao 20,00 wanaweza kushuhudia michezo ya baiskeli


HAMPDEN PARK


Hampden Park uwanja huu unauwezo wa kuingiza watazamaji 52,063 wakiwa wamekaa kushuhudia mchezo wa soka