Tuesday, May 31, 2011

TUBADILIKE KATIKA HILI.

Imekuwa ni kama desturi watu kupuuza kanuni na taratibu zinazowekwa sehemu mbalimbali nchini aidha kwa makusudi au kwa kutokujua na bado wahusika wakafumbia macho uvunjwaji wa kanuni na taratibu hizo. Utathibitisha haya utakapopita mitaani na kukuta maeneo yamejaa takataka ili hali pameandikwa usitupe taka hapa lakini ndio panakuwa dampo la kimataifa hali hii ninaweza kusema imechangia kwa kiasi kikubwa miji mingi Tanzania kuwa michafu kupita kiasi. Sielewi ni kwa faida au hasara ya nani mtu anapoamua kutupa takataka sehemu ambayo hairuhusiwi maana inaonekana kila mtu anapuuza na hata wanaohusika katika kusimamia mazingira inawezekana mtu anaacha kama vile anasema kwani ni nyumbani kwangu hapo aaah acha pawe pachafu,jamani kumbukeni hayati baba wa taifa Mwl J.K. Nyerere aliwahi kusema kuwa mwenye kujenga ama kubomoa nchi ni mwananchi mwenyewe sasa katika hili kwanini tunataka mpaka mtu atumie nguvu?
Siku hizi kumezuka mtindo watu wanakusanya uchafu majumbani mwao wanajaza kwenye mifuko ya plastic au kwenye viroba halafu wanasubiri usiku au gizagiza na kwenda kuvitelekeza katika maeneo ya wazi yaani kana kwamba ameambiwa pale ndio jalalani.

wafanyabiashara wakifanya biashara eneo lisilo rasmi.

Hali hii ya kukaidi kanuni na taratibu ndio leo hii inaleta mgogoro kati ya halmashauri ya jiji na wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga,kuna maeneo yametengwa kwa biashara lakini wao wanataka tubanane humuhumu mijini jamani kwa staili hii hatutofika hakuna kitu nkizuri kama kufuata sheria,kanuni na taratibu zinazowekwa kwa manufaa ya wote. Pichani wafanyabiashara wakiendeleza biashara sehemu isiyo rasmi tena huku kukiwa na tangazo kubwa tu ambapo hata asie na macho anaweza kuliona.naomba nisichonge sana alieelewa kaelewa na ambaye anajifanya hajaelewa mimi najua kaelewa.