Tuesday, February 4, 2014
CHELSEA YAITULIZA MASHETANI MAN CITY
Ivanovic akitupia kambani bao la pekee.
Muuaji Ivanovic akishangilia goli la pekee dhidi ya Man City
Manchester City imevutwa shati na Chelsea kwa kucharazwa bao 1-0 katika uwanja wao wa nyumbani. kabla ya mechi hiyo Man City ilikuwa imeshinda mechi zote 11 ilizokuwa imecheza katika dimba la nyumbani Ettihad Stadium kabla ya kukutana na Chelsea.
Mtanange huo umeweka historia mpya kwa mara ya kwanza kwa Manchester City kushindwa kufunga bao katika mechi za nyumbani tangu mwaka 2010.Bao la Chelsea lilifungwa na Branislav Ivanovic katika kipindi cha kwanza .
Kutokana na matokeo hayo Manchester City na Chelsea zinalingana pointi lakini Man City imetupia kambani mabao mengi.
Liverpool iko katika nafasi ya nne, Everton ni ya tano ilhali Tottenham ni ya sita huku Manchester United ikishikilia nafasi ya saba.
Kwangu mimi huyu dogo,Hazard ndio alikuwa "Man of the Match"
Hali tete Wachezaji wa Man City ''wameshavurugwa"
Hii ndio hali ilivyokuwa baada ya kukosakosa magoli
Hii ni hali na vituko vya Mourinho pale alipohisi mwamuzi hatendi haki
TAZAMA VIDEO YA MPAMBANO HUO
Subscribe to:
Posts (Atom)