Monday, May 12, 2014

MAN CITY VIDUME EPL......OOOPS THEY DID IT AGAIN


Mabingwa wapya wa Uingereza 2014-2015 Manchester City.

Vijana wa Manuel Pelligrini walitawazwa mabingwa katika siku ya mwisho ya ligi kuu ya Uingereza baada ya kuilaza West Ham mabao 2-0.

Samir Nasri nahodha Vincent Kompany ndio waliomhakikishia Pelleigrini alama tatu muhimu zilizotosha kuipiku Liverpool iliyomaliza katika nafasi ya pili alama 86 mbili nyuma ya City ambao wametwaa taji lao la pili katika kipindi cha miaka mitatu.
Umati uliojaa uwanjani Etihad ulimiminika uwanjani baada ya kipenga cha mwisho.
Kocha huyo kutoka Chile alifaidika na kichapo cha Liverpool mikononi mwa Chelsea na hivyo alihitaji sare ya aina yeyote kujihakikishia ushindi.
Mancity iliititima West ham 2-0 na kutamatisha msururu wa mechi tano bila ya kushindwa .
Pelligrini, atakumbukwa kwa kuirejesha kombe Etihad baada ya Roberto Mancini kupigwa kalamu kwa kushindwa kutetea taji msimu uliopita .
Kocha huyo mwenye miaka 60 anajivunia mabao 102.
Kwa upande wao Liverpool walisajili ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Newcastle United uwanjani Anfield.
 
Mashabiki wa Man City wakishuhudia timu yao ikitwaa ubingwa wa EPL.


Samir Nasri akitupia kuihakikishia Man City ubingwa.



Nahodha wa Man City Vicent Kompany akinyanyua juuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu kombe la ligi kuu ya uingereza 2014-2015




Kocha wa Man City Manuel Pellegrini akiwa amebeba kombe la ligi kuu Uingereza 2014-2015

Wachezaji wa Man City wakiwa wamembeba kocha wao Pellegrini baada ya kunyakua kombe la ligi kuu ya UIngereza