Thursday, September 15, 2011

BEAUTIFUL AQUA TOWER OF CHICAGO

http://groups.yahoo.com/group/babes_in_blue/

http://groups.yahoo.com/group/babes_in_blue/

KWANINI VIONGOZI TANZANIA HAWAWAJIBIKI PINDI YANAPOTOKEA MAJANGA?

Nakwazika sana na matukio na shida zinazowakabili wananchi wa Tanzania bila ya viongozi wanaohusika kuwajibika ama kuwajibishwa..mfano hili swala la ajali ya meli kama ingekuwa limetokea nchi zenye viongozi wanaojua nini uongozi na wenye maadili katika utumishi wa umma lazima wahusika wangejiuzulu,

Tumeshaona mifano nchi nyingi viongozi wakijiuzulu pindi mambo yanapokwenda kombo katika idara ama vitengo vyao iwe wamesababisha wao ama wamesababisha watendaji wao likishatokea janga ni kujiuzulu tu hakuna mjadala..kwa masikitiko hali ni tofauti hapa Tanzania, madaraka yanatumiwa vibaya na waliopewa dhamana kwani wanajali zaidi maslahi yao kuliko Taifa lenye watu waliowachagua. Na hii inatokana na udhaifu wa kiongozi mkuu ambaye ni Raisi, yeye ndie mwenye kusimamia Taifa na viongozi wake lazima awe na msimamo katika kuhakikisha watendaji wake wanawajibika kwa mujibu wa kanuni na taratibu za nchi.

Sioni sababu ya Viongozi ambao wizara ama idara zao zina kashfa za mikataba mibovu,matumizi mabaya ya ofisi,maafa kutokana na uzembe wa watendaji wao,hali ya maisha kuwa ngumu kutokana na upandaji na ukosekanaji wa bidhaa muhimu katika taifa,wizi na ufujaji wa mali za umma na wengineo wengi kuendelea kubaki katika nyazifa zao.

Kwa staili hii ya viongozi wazembe kuendelea kuonekana kama miungu watu Daima taifa litaendelea kuwa masikini, kwani kutokana na ajali na vifo vya majanga ya kizembe vinapoteza watu ambao ni nguzo muhimu katika ujenzi wa Taifa, Kutokuwa na uwajibikaji katika idara nyeti zinadumaza huduma muhimu kwa wananchi na kufanya kuwa na maendeleo duni,hivyo kama wananchi hawana la kufanya taifa haliwezi kupata kipato.
Inauma na inakera sana kuona nchi inakosa mwelekeo kwasababu ya watu wachache, Jamani enyi viongozi hivi mliingia katika uongozi ili muwatumikie wananchi kweli?
Nilichogundua ni tofauti ya kuwa kiongozi hapa Tanzania na kuwa kiongozi nchi zingine, tofauti ni hii:
Nchi zilizoendelea mtu anagombea uongozi kwa hulka ya kuwa kiongozi ya kuwatumikia wananchi waliomchagua tofauti na viongozi wetu swala la kuwa kiongozi wameligeuza ajira, hapa ndio matatizo yalipo ndio maana kiongozi ukimwambia ajiuzulu ama awajibike inamuwia vigumu kwasababu hana mbele wala nyuma uongozi ndio kila kitu kwake.


Imefikia wakati sasa viongozi muone uongozi kuwa ni dhamana halisi ya kuwatumikia watu na sio ajira kama mlivyogeuza kwa hivi sasa, mkiwa na jinsi nyingine ya kuishi na mkauchukulia uongozi kuwa ni dhamana ya kuwatumikia wananchi lazima mtakuwa na maadili mema ya utumishi wa umma, pindi unapoonekana umeshindwa kuwajibika basi swala la kuachia ngazi halitokuwa gumu kwako kwani ilikuwa ni sehemu ya maisha yako na sio maisha yako.

Watanzania wenzangu kwa kulifahamu hili na mkagundua viongozi wetu wameufanya uongozi ndio njia yao ya kuishi hamtoshangaa kwanini wanafanyaufisadi na wamekuwa wagumu kuwajibika ama kuchukua maamuzi magumu. Uongozi sio ajira kama tunavyofikiria,mshahara unaopewa kiongozi ni malipo ya muda na busara zako unazozitumia katika kuwajibika kwa wanachi na Taifa kwa ujumla. Na sababu hizi za kuufanya uongozi kama ajira zinapelekea viongozi kutokuwajibika ipasavyo katika nyazifa zao kwakuwa muda mwingi wanapanga mipango ya kujipatia pesa ama kufanya kazi aile tu zenye kuwapatia pesa ama zenye 10% na kazi za mshahara huwa hazifanyiki kwa jinsi inavyotakiwa zifanyike.
Nitaendelea na mada hii........+255 684 887 525.

SIMBA IKO JUU KAMA "ROCKET" YAWACHEZESHA KWATA POLISI DODOMA


Ulimboka mwakingwe akijaribu kuska mpira bila mafanikio

MSHAMBULIAJI Gervais Kago aliisaidia timu yake ya Simba kuichapa Polisi Dodoma bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi.

Matokeo hayo yameifanya Simba kufikisha pointi 13 na kuendelea kubaki kileleni mwa ligi kuu wakifuatiwa na JKT Ruvu wenye pointi tisa, huku Yanga ikishikilia mkia ikiwa na pointi tatu.

Kocha wa Simba, Moses Basena alisema amefurahishwa na matokeo yaliyompa pointi tatu muhimu.

Mshambuliaji Kago alifunga bao lake la pili msimu huu kwa Simba katika dakika ya 25 akipokea pasi ya kifua kutoka kwa Felix Sunzu na kupiga shuti kali lililojaa wavuni.

Katika mechi hiyo Bryton Mponzi alipoteza nafasi ya kuisawazishia Polisi Dodoma baada ya kushindwa kuunganisha krosi ya Salmin Kiss Kiss huku kiungo wa Simba, Jerry Santo naye alijitahidi kufunga bao katika dakika ya 22 kwa kichwa, lakini beki wa Polisi alizuia mpira huo kwenye mstari wa goli.

Wakati Polisi Dodoma wakijitahidi kutafuta bao la kusawazisha Mponzi alipiga kichwa dhaifu kilichoishia mikononi mwa kipa Juma Kaseja, ambapo Simba walijibu mapigo katika dakika ya 43, baada ya Kago kujaribu kumtungua kipa wa Polisi Dodoma, Agathon Mkwandiko, lakini mpira huo ulitoka nje.


Uhuru Selemani wa Simba akichuana na beki wa Polisi Dodoma

Simba walirudi kipindi cha pili kwa kasi hasa katika dakika za 53, 56, ambapo Kago na Emmanuel Okwi walipoteza nafasi za kufunga wakiwa wao na kipa Mkwandiko kwa mashuti yao kutoka nje.

Mwamuzi Charles Mchau alitoa kadi za njano kwa Bantu admin wa Polisi Dodoma na Nassoro Said wa Simba kwa mchezo mbaya katika mechi hiyo.

Kocha wa Polisi Dodoma, John Kanakamfumu akizungumzia mechi hiyo alisema makosa ya mabeki wake katika kipindi cha kwanza ndiyo yaliyosababisha matokeo hayo.

"Nimegundua mapungufu kidogo, lakini tunakwenda kurekebisha kabla ya mchezo ujao," alisema Kanakamfumu.
Licha ya uwanja wa Azam kuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 5000, mashabiki walishindwa kuujaza uwanja huo na sababu mojawapo ikiwa ni ulanguzi mkubwa uliokuwa ukifanywa na wauza tiketi katika vituo mbalimbali.


Uhuru Selemani akikwepa daruga la mlinzi wa Polisi Dodoma

Hamasa kubwa ya mashabiki wa Simba waliotaka kuiangalia timu yao ikicheza kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi ilitumbukia nyongo kutokana walanguzi wa tiketi hizo.

Pamoja na TFF kutangaza tiketi ya kiwango cha chini kuwa shilingi 7,000 baadhi ya magari yalionekana yakiziuza tiketi hizo kati ya Sh 9,000 hadi 10,000.

Gari lililokuwa linauza tiketi Mbagala mwisho Toyota Hiace namba tunazo walitoa tiketi kwa watu waliokuwa wakiziuza eneo la Big Bon Mbagala kwa bei ya ulanguzi.

Huku gari hilo lilikuwa likizunguka mitaani na kusimama kwenye kituo cha mabasi yaendayo Mbande na Msongola na kuuza tiketi kwa bei kubwa kinyume na eneo walilotakiwa kusimama na kuuza tiketi.

Pia, nje ya eneo la TFF majira ya saa tano asubuhi watu wengi walikuwa wanauza tiketi za Sh 7000 kwa sh 10,000 wakati huo magari yalikuwa hayajaanza kuuza tiketi.


Brcelona,Arsenal,Man United zashindwa kutamba Chelsea,Real Madrid,Bayern zang'ara Ligi ya mabingwa Ulaya

Ligi ya mabingwa ulaya iliendelea tena wiki hii na kuona vigogo vikishindwa kutamba kwa kulazimishwa suluhu na timu pinzani. matokeo ya mechi hizo ni kama ifuatavyo.

13-9-2011

Barcelona        2-2     A.C Milan
F.C Porto         2-1    Shaktar Donetsk
B/ Dortmund   1-1    Arsenal
Olympiakos     0-1    Marseille
Chelsea           2-0    Leverkusen
Genk               0-0    Valencia
Opoel Nicosia 2-1    Zenit
 Plzen               1-1    Bate

14-9-2011

D/Zagret   0-1   R.Madrid
Ajax         0-0    Lyon
Benfica    1-1    Man United
Basel        2-1   Otelul Galat
Inter         0-1   Trabzosper
Lille         2-2   CSKA Moscow
Villareal  0-2   Bayern Munich
Man City 1-1   Napoli

                                              Matukio mechi Barcelona vs AC Milan



Matukio mechi ya Chelsea vs Leverkusen


Matukio mechi ya Borussia Dortmund vs Arsenal


Matukio mechi ya Man United vs Benfica


Matukio mechi ya D/Zagreb vs Real Madrid


Matukio mechi ya Villarel vs Bayern Munich


Matukio mechi ya Man City vs Napoli