Wednesday, September 30, 2015

BARCELONA, BAYERN ZATAMBA HUKU ARSENAL,CHELSEA ZIKIANGUKIA PUA



Timu za soka ambazo ni Tishio barani ulaya Barcelona, na Bayern Munich zimeshinda katika michezo yao ya pili ya klabu bingwa ulaya.
Barcelona, waliwachapa Bayern 04 Leverkusen, kwa mabao 2-1 mabao ya Barcelona yakitupiwa kambani na Luis Suárez na Sergi Roberto, huku la Bayern likitupiwa na Kyriakos Papadopoulos.
 
Suarez akishangilia baada ya kutupia kambani goli la kwanza

Bayern munich ya Ujerumani iliifanyia ukatili timu ya Dinamo Zagreb kwa kuitatika kamba 5-0 mshambuliaji Robert Lewandowski, akizifumania nyavu mara tatu na nabao mengine yakitupiwa kambani na Douglas Costa, na Mario Gotze.
 
Muuaji wa magoli matatu Lewandowski akishangilia na wachezaji wenzake

Chelsea, wakicheza ugenini huko nchini Ureno, walipokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa FC Porto ya Ureno mabao yakitupiwa  kambani na Brás André na Maicon, huku lile la kufutia machozi la Chelsea, likifugwa na Mbrazil Willian.
 
Mshikemshike dimbani hatumwi mtoto gengeni mpaka kieleweke
 
 Maicon akishangilia baada ya kuitengeneza Chelsea


Bwana mdogo tulia usilete shida alaaa

""Oyaaaaah mnanitia aibuuuu"" Kocha wa Chelsea Jose Mourinho akiwahimiza vijana kufanya kweli

Washika bunduki wa London ,Arsenal wakiwa katika uwanja wao wa Emirates walitolewa nishai kwa kutandikwa mabao 3-2 na Olympiakos,
 
Wachezaji wa Olympiacos wakishangilia baada ya kuiteketeza Arsenal
 
Wachezaji wa Arsenal wakiwa hawaamini kinachotokea katika Dimba la Emirates

Matokeoa mengine ya michezo ya klabu bingwa ulaya
 BATE Bor 3 – 2 Roma
Maccabi Tel Aviv 0 - 2 Dynamo Kiev
Lyon 0 – 1 Valencia
Zenit St P 2 – 1 KAA Gent