Thursday, July 21, 2011

MAN UNITED YAICHAKAZA SEATTLE SOUNDERS 7-0 NGASSA NDANI

Rio Ferdinand akiondosha mpira mbele ya Mrisho Ngassa

Mshambuliaji wa Man United Wyne Rooney amepiga Hat-Trick katika mechi yao dhidi ya Seattle Sounders wakiwa ziarani nchini Marekani, Rooney alipiga mabao matatu akitokea benchi. Goli la kwanza la Man lilifungwa na Michael Owen Dk 14 baada ya kazi nzuri ya kupasiana mpira kati ya Ashley Young na Evra.Goli la pili lilipatikana Dk 29 mfungaji akiwa ni Macheda kabla ya Rooney kupiga goli Dk 51 na Park akapiga lingine Dk52  na Rooney kuchomeka lingine.
Rooney alipiga goli lake la tatu Dk 71 na la sita kwa Man kabla ya Gabrieol Orbertan kuhitimisha karamu hiyo kwa goli la saba katika Dk 88.
Katika mechi hiyo mtanzania Mrisho Khalfan Ngassa alicheza upande wa Seattle Sounders ikiwa ni mechi yake ya majaribio. mpaka gmechi inakwisha kina Ngassa walikuwa wameloa goli 7 kwa buyu.
 Zifuatazo ni picha katika mechi hiyo


Rooney na Nani

Giggs akichuana vikali

Van Der Sar akipangua mchomo

Umati wa mashabiki

Uwanja wa Seattle Sounders

MACHAFUKO YAZUKA LILONGWE MALAWI

KISA NI KUPANDA KWA GHARAMA ZA MAISHA

Machafuko yamezuka mji mkuu wa Malawi, Lilongwe, wakati makundi ya upinzani yakipinga serikali ya Rais Bingu wa Mutharika.
Mwandishi wa BBC mjini Lolongwe Joel Nkhoma, amesema waandamanaji walikuwa wanachoma vizuizi barabarani na kupora.
Rais wa Malawi Bingu Wa Mutharika
Serikali imezuia radio kutangaza moja kwa moja ghasia hizo.
Matatizo yalianza baada ya mahakama kutoa hukumu siku ya Jumanne kwamba maandamano ya nchi nzima, yaliyoitishwa kupinga kupanda gharama za maisha, ni haramu.
Mwandishi wa BBC amesema licha ya uamuzi huo wa mahakama, maandamano pia yamefanyika katika mji mkuu wa kibiashara Blantyre, na katika mji wa kaskazini wa Mzuzu.
Lakini hali imekuwa mbaya zaidi mjini Lilongwe, ambapo waandamanaji wenye hasira walikuwa wakipiga kelele, "Mutharika aondoke", amesema mwandishi wetu.
Mwandishi huyo amesema polisi walifyatua mabomu ya kutoa machozi na wameweka vizuizi barabarani kuzuia waandamanaji kuingia katikati ya mji wa Lilongwe, ambapo maduka yote yamefungwa na mitaani hakuna watu.
Kwa mujibu wa mwandishi wetu ghasia zipo zaidi katika miji midogo iliyo karibu na Lilongwe ya Biwi, Kawale na Nchesi.
Kumekuwa na majibizano ya kushambuliana kati ya polisi na waandamaji, kwa mujibu wa msemaji wa Tume ya Haki za Binadamu ya Malawi Mike Chipalasa.
"Watu wana hasira sana. Hali si nzuri hapa," amesema.
Duka linalomilikiwa na Mbunge kutoka chama kinachotawala cha Democratic Progressive Party (DPP) na ghala la mfanyabiashara mwenye uhusiano na Rais Mutharika yameporwa kwa mujibu wa mwandishi wa BBC.
Pia kuna taarifa za kuchomwa moto nyumba za askari polisi watatu mjini Lilongwe.
Polisi pia wamezuia kamera ya mpiga picha mmoja aliyekuwa akipiga picha maandamano hayo.
Kuna taarifa nyingine zinasema polisi walimpiga risasi sikioni mwandamanaji mmoja, wakati mali ya waziri mmoja iliposhambuliwa.
Maandamano hayo yaliitishwa kupinga kupanda bei ya mafuta, upungufu wa hazina ya fedha za kigeni, kukosekana utawala bora na uhusiano mbaya wa kimataifa.
Wiki iliyopita Uingereza ilisimamisha misaada kwa Malawi baada ya kutokea mzozo wa kidiplomaisa na serikali ya Mutharika.
Uingereza iliishutumu Malawi kwa kushindwa kusimamia uchumi na haki za binadamu.
Hivi karibuni serikali ilipitisha hatua za kubana matumizi, ikapandisha kodi na kupunguza utegemezi wa misaada.
Malawi ni moja ya zilizo masikini sana duniani, ikikadiriwa asilimia 75 ya watu wa nchi hiyo wanaishi chini ya dola moja kwa siku.

JAPAN MABINGWA WA DUNIA SOKA LA WANAWAKE

Japan imeilaza Marekani kwa mikwaju ya penalti 3-1 na kuwa nchi ya kwanza kutoka bara Asia kushinda Kombe la Dunia kwa wanawake.
Wachezaji wa Japan Wakishangilia ubingwa wa dunia kwa wanawake

Saki Kumagai ndiye aliyefunga mkwaju wa penalti wa ushindi baada ya mlinda mlango wa Japan, Ayumi Kaihori kuokoa mikwaju mwili ya penalti kati ya mitatu ya wanadada wa Marekani.
Alex Morgan alikuwa wa kwanza kuifungia Marekani bao, kabla ya Aya Miyama kusawazisha dakika za mwisho za muda wa kawaida.
Abby Wambach aliipatia Marekani bao la pili katika muda wa nyongeza, lakini Homare Sawa alihakikisha kutakuwa na kandanda ya kusisimua ya fainali baada ya kusawazisha zikiwa zimesalia dakika nne mchezo kumalizika, alipounganisha mpira wa kona ulioingia moja kwa moja wavuni.
Marekani watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kuweka rekodi ya kunyakua Kombe la dunia kwa mara ya tatu, baada ya kumiliki mchezo kwa kipindi kirefu. Lakini pia wanadada hao wa Marekani walishindwa kutumia vyema nafasi walizopata kufunga mabao hasa kipindi cha kwanza.
Wambach mshambuliaji wa Marekani alikuwa tishio kwa ngome ya Japan na alikaribia kufunga wakati mkwaju wake kugonga mwamba na kutoka nje.
Japan, ambao walikuwa hawajawahi kuishinda Marekani katika michezo 25 waliyokutana siku za nyuma, ambapo walifungwa mara 22, walionekana kuwazidi wapinzani wao katika mashambulio ya kushtukiza. Mbinu hiyo ya kushambulia kwa kushtukiza iliwasaidia sana walipocheza na wenyeji Ujerumani katika hatua ya robo fainali na vile vile walipoitoa Sweden hatua ya nusu fainali, lakini ngome ya Marekani ilikuwa ikikabiliana na wanadada hatari wa Japan, Nahomi Kawasumi na Kozue Ando ambao kwa kiasi fulani walifanikiwa kuwatia mfukoni.

BARCELONA HAIJAKATA TAMAA KWA FABREGAS

Csec Fabregas
Kocha wa Barcelona Pep Guardiola amesema klabu yake "itapigana hadi mwisho" mpaka imnase kiungo wa Cesc Fabregas.
Mabingwa hao wa Ulaya mwezi wa Juni mwaka huu waliweka dau la paundi milioni 27 kwa ajili ya kumsajili Fabregas, lakini dau hilo lilikataliwa na Arsenal.
"Barcelona imetoa maombi mengine kwa Arsenal na tuna muda hadi tarehe 31 mwezi wa Agosti kujaribu kufikia makubaliano," alisema kocha huyo wa Barca Guardiola.
"Tunaendelea kupigana hadi mwisho kujaribu kumpata Cesc kwa sababu tunaamini ataisaidia timu na kikosi kizima."
Ameongeza: "Kuna kiasi cha pesa kwenye hazina yetu zinasubiri kumsajili Fabregas, lakini iwapo haitawezekana pesa hiyo itatumika kwa nyingine."
Fabregas ni zao la chuo cha vijana wa Barcelona kabla ya kujiunga na Arsenal akiwa na umri wa miaka 16 mwaka 2003. Hakusafiri na kikosi cha Arsenal kilichokuwa bara Asia kwa mazoezi ya kujinoa kwa ligi.
Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Barcelona Andoni Zubizarreta, amesema jukumu kubwa la timu hiyo kabla ya kukamilika usajili ni kumpata mshambuliaji mpya, huku wakimlenga zaidi mshambuliaji wa Udinese anayechezea pia timu ya taifa ya Chile Alexis Sanchez.

KWANINI WABUNGE MNAPENDA USHINDI TU NA SI KUSAIDIA TIMU ZINAPOJIANDAA KUWAKILISHA TAIFA?

KUITA TIMU AMA WACHEZAJI BUNGENI PINDI WANAPOFANYA VIZURI HAINA TIJA NA HAILETI MAANA...KWANI NYINYI WABUNGE HUWA MNAKUWA WAPI WAKATI TIMU ZINAJIANDAA KWENDA KWENYE MASHINDANO? ITALETA MAANA ZAIDI KAMA MTAZIITA TIMU BUNGENI MKAZISAIDIA KWANI ITAWAPA ARI NA MOYO WASHINDANI WANAPOLIWAKILISHA TAIFA NA SIO MSUBIRI MPAKA TIMU IFANYE VIZURI..AIBU YENU..HIVI SASA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE TWIGA STARS WANAJIANDAA KWENDA KULIWAKILISHA TAIFA KATIKA MASHINDANO YA "ALL AFRICAN GAMES"..PESA NI TATIZO MMEKAA KIMYA, HALAFU KWA HARAMBEE IKIFANIKIWA KWENDA IKARUDI NA USHINDI MTAJICHOMEKA NA KUIITA BUNGENI..ATI KUIPONGEZA,HAINA MAANA. WASAIDIENI SASA HIVI WANAPOJIANDAA NDIO WATAKAPOSHINDA TUTAWASHUKURU NA KUWAPONGEZA KWA KUSAIDIA MAANDALIZI YALIYOLETA USHINDI.