|
Wednesday, December 19, 2012
INDIA Vs CHINA
KUUNGANISHA UMEME SASA BEI CHEE
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), limetangaza rasmi kupunguza viwango vya kuunganisha umeme kuanzia Januari Mosi, 2013 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliyoitoa katika Bunge la Bajeti lililopita.
Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud amesema kupunguzwa kwa viwango hivyo kutasaidia wananchi wengi kuunganisha umeme.
Badra alisema gharama za kuunganisha umeme vijijini katika umbali usiozidi mita 30 bila nguzo sasa itakuwa Sh177,000 na wateja wa mijini watatakiwa kulipia Sh320,000 badala ya Sh455,108 za sasa akisema punguzo hilo ni sawa na asilimia 61.11 kwa wateja waishio vijijini na asilimia 29.48 kwa wateja wa mijini.
Alisema kwa wateja wanaoishi vijijini wanaohitaji umeme wa njia moja na nguzo moja watatakiwa kulipia Sh337,740 wakati wale wa mijini watalipia Sh515,618 badala ya Sh1,351,884 zinazolipwa na wateja hivi sasa.
“Punguzo hilo ni sawa na asilimia 75.02 kwa wateja waishio vijijini na asilimia 61.86 kwa wateja waishio mijini.”
Alisema wateja wa vijijini watakaojengewa njia moja na nguzo mbili watatakiwa kulipia Sh454,654 na wa mijini watalipia Sh696,670, badala ya Sh2,001,422 ambazo zinalipiwa hivi sasa.Alisema punguzo hilo ni sawa na asilimia 77.28 kwa wateja waishio vijijini na asilimia 65.19 kwa wateja wa mijini.
Meneja mawasiliano wa Tanesco,Badra Masoud akifafanua jambo.

MESSI BADO YUPO SANA BARCELONA
Lionel Messi amekubali kusaini mkataba mpya na klabu ya
Barcelona, utakaodumu kwa mwaka wa 2018.
Nyota huyo kutoka Argentina, mwenye umri wa miaka 25, amekuwa na miaka minne ya mafanikio na klabu hiyo na pia kwa taifa lake.
Kufikia sasa Messi amefunga jumla ya magoli 90 mwaka huu pekee.
Mlinda langu Carles Puyol, 34, na mcheza kiungo Xavi Hernandez, 32, pia wamesaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Barcelona.
Ripoti zinasema kuwa wachezaji hao sasa watasalia na Barcelona hadi mwaka wa 2016.
Kwa mujibu wa tangazo kutoka kwa klabu hiyo, Puyol, Messi na Xavi wanatarajiwa kusaini mkataba mpya katika muda wa siku chache zijazo.
Afisa mmoja wa klabu hiyo amesema ni jambo la kutia moyo kuona kuwa Barcelona imefanikiwa kudumisha huduma za wachezaji wake nyota.
Kandarasi ya Messi na Barcelona inakamila mwa wa 2016 ili hali kandarasi ya Puyol inamalizika mwaka wa 2013 huku kandarasi ya Xavi inakamilika mwaka wa 2014.
Leonel Messi
HAPPY BIRTHDAY BARBARA AMINA HASSAN
Leo ni siku ya kuzaliwa ya mtangazaji wa Clouds entertainment Group Ltd wa kipindi cha Power Breakfast, Barbara Amina Hassan. Napenda kuchukua nafasi hii kumtakia maisha mema alizaliwa lini ana miaka mingapi kwasasa sitaki umbea mtafute mwenyewe ninachojua amezaliwa siku kama ya leo 19 Dec .......
Subscribe to:
Posts (Atom)