Monday, December 17, 2012

KINA DADA/MAMA FUNGA MWAKA NA STYLE MPYA YA RANGI ZA KUCHA

 


WANYAMA NAO SIKUKUU YA X-MAS INAWAHUSUCORINTHIANS YAIDUNGUA CHELSEA FAINALI YA KOMBE LA KLABU BINGWA YA DUNIA

Klabu ya Corrinthians kutoka Brazil, imeibuka kidedea katika michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa duniani baada ya kuidungua Chelsea ya Uingereza kwa bao moja kwa "nunge" katika mechi ya fainali iliyochezwa nchini Japan.
Paolo Guerrero ndie aliepeleka msiba Uingereza akitupia bao la pekee na la ushindi kwa Corinthians.
Hata hivyo Chelsea, ilipoteza bafasi nyingi za kufunga wakati wa mechi hiyo pale washambuliaji wake walipokuwa wakipepesa macho na kutetemeka miguu kutupia kambani pindi wanapofika katika eneo la hatari la Corinthians.
Katika muda wa ziada Fernando Torres, alipoteza nafasi nzuri sana ya kuzawazisa licha ya kuwapiku walinzi wa Corinthians na kubakia yeye na mlinda mlango Cassio alieonekana "mnoko" kwa kuchomoa hatari nyingi zilizoelekezwa langoni mwake ambapo Torres alijaribu kumlamba chenga kipa huyo wa Corinthians na kuachia fataki lakini kombora lake likawa hafifu na kudakwa kwa urahisi na kipa.

Chelsea ilimaliza mechi hiyo ikiwa na wachezaji kumi baada ya Gary Cahil, kupewa kadi nyekundu baada ya kumfanyika madhambi mchezaji wa Corrinthians Emerson.
Bao la chelsea lililofuingwa kwa kichwa na Fernando torres lilikataliwa na hivyo vijana hao kutoka brazil wakaibuka na ushindi.

Paolo Guerrero akitupia bao pekee kwa kichwa katika mpambano huo...mtazame Ramires na Ashley Cole wanatamani waudake lakini waaaapi baaadae sanaaaa!!Guerrero akishangilia goli huku Ashley Cole akisafisha vyombo kambani na David Luiz akiwa tayari kumsaidia.


Ashley Cole akimthibiti Henrique

Hazard akipata kichapo..hapa braza mawili, mpira ubaki wewe uende au mpira uende wewe ubaki..upo!?


Tulia nimwage majaro weweee...


Aiyaaaaaaah tumekosa!!?? Tulieni nyinyi tumetumwa kombe sisi alaaaaahh


Wachezaji wa Corinthians wakiwashukuru mashabiki kwa support baada ya mtanange kuisha


Inauma sana unajuaa . Nahodha wa Chelsea Frank Lampard akiwa na majonzi ya kulikosa kombe.


Emerson wa Corinthians akimfariji Mbrazil mwenzake Ramires..ndio ukubwa kaka kama vipi rudi home ushangilie makombe.Kazi tuliyotumwa kutoka Brazil imetimia hureeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!