Friday, July 29, 2011

MAN CITY YAKAMILISHA USAJILI WA SERGIO AGUERO

Sergio Aguero anasema ameshajiunga na timu ambayo " Itajitahidi kila mwaka kushinda mataji makubwa". baada ya kukamilisha kuhama kwake kutoka Atletico Madrid hadi Manchester City.

Sergio Aguero
Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Argentina aliwasili England siku ya Jumatano kukamilisha mipango ya kuhama kwa kiasi kinachosemekana kuwa pauni za Uingereza milioni £38m.

Siku ya Alhamisi jioni timu hiyo ilitangaza kuwa Aguero ametia saini kandarasi ya miaka mitano.

Man City wanasema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, anatarajiwa kuwa miongoni mwa kikosi kitachocheza mechi ya kombe la Dublin mwishoni mwa juma.

Aguero, atakayevaa nambari 16, amesema katika mtandao rasmi wa Man City: " Nafkiri sisi ni timu ambayo katika siku zijazo tutakuwa tukijitahidi kushinda mataji makubwa kila mwaka.

" Wakati tukifanya mazungumzo niliwaambia mawakala wangu wafanye kila wawezalo kwa sababu hii ni timu nzuri na nilitaka sana kucheza kwenye ligi kuu ya soka ya England. Nimeridhishwa kwa hilo.

Nafkiri sitokuwa na tatizo kwenye timu hii. Nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu kufanya kile meneja anachotaka nifanye na kujaribu kuwajibika vile yeye anavyotaka mimi niwajibike."

Alipoulizwa kuhusu kuzowea maisha ya England, aliongeza: " Kwanza sipendi hali ya hewa ya joto kwa hiyo hapa nitakuwa sawa. Nina hakika nitafurahi hapa na nitakuwa sawa."

Mapema siku ya Alhamisi, Aguero aliandika kwenye mtandao wa Tweeter: " Mimi tayari ni mchezaji wa City. Nimefurahi kuwa kwenye timu hii na pia mji huu wa Manchester."