Thursday, September 19, 2013

MNIGERIA ASHINDA SHINDANO LA UREMBO WA KIISLAMU (MISS WORLD MUSLIMAH 2013)

Mwanadada wa Nigeria ndiye mshindi wa shindano la urembo kwa wasichana wa kiisilamu mjini Jakarta Indonesia.
Obabiyi Aishah Ajibola, 21, alishinda shindano la kimataifa la wasichana wa kiisilamu kwa jina Muslimah mwaka 2013 siku ya Jumatano.
  
Obabiyi Aishah Ajibola, 21, akivishwa taji la urembo
 
Washindani 20 walishiriki mashindano hayo kuonyesha mitindo ya kiisilamu pamoja na maadili ya kiisilamu wakati wa mashindano hayo.
Mashindano yalifanyika kabla ya shindano kubwa zaidi la mwanamke mrembo zaidi duniani, ambalo limeghadhabisha makundi ya watu wenye msimamo mkali nchini Indonesaia kwa kutaka kuandaliwa huko.
Waliofuzu kwa fainali ya mashindano hayo, walichaguliwa kutoka miongoni mwa watu 500 waliochaguliwa kwa kutumia njia ya mtandao.
Moja ya vikwazo vya kuruhusiwa kushirki kwenye mashindano ilikuwa kusimulia kisa chako na ambavyo ulianza kuvalia Hijab au mtandio, ambacho kilikuwa kikwazo kwa wote waliotaka kushiriki.
Washiriki walitoka Bangladesh, Iran, Malaysia, Nigeria na Brunei.
Kabla ya fainali, washindani walihitajika kuamuka kwa sala ya asubuhi na kuswali pamoja huku wakijifunza kusoma Koran.
Bi Ajibola, mwenye umri wa miaka 21, alilia na kusoma aya kutoka kwa Korani, jina lake lilipotajwa. Alituzwa dola 2,200, pamoja na ziara ya mji mtukufu wa Mecca na nchini India.
Kabla ya kushinda alisema kuwa nia yake ya kushiriki mashindano hayo ilikuwa tu kuonyesha dunia nzima kuwa dini ya kiisilamu ni nzuri sana.
Eka Shanti, aliyefutwa kazi kwenye televisheni kwa kukataa kuvua mtandio wake, ndiye alianzisha shindano hilo miaka mitatu iliyopita.
Aliambia shirika la habari la Agence France-Presse kuwa walifanya shindano hili siku chache kabla ya shindano la kimataifa la mwanamke mrembo zaidi duniani kuonyesha wasichana kuwa kuna njia zengine tofauti ambazo unaweza kuwa mrembo.
Indonesia ndio nchi yenye idadi kubwa ya waisilamu duniani.
 


Obabiyi Aishah Ajibola akishindwa kujizuia Baada ya kutangazwa mshindi.




Obabiyi Aishah Ajibola akitoa neno la shukrani







MREMBO WA LEO


LIGI YA MABINGWA ULAYA CHELSEA YACHAPWA BARCELONA, ARSENAL KAMA KAWA KAMA DAWA



Ligi ya mabingwa barani ulaya imeendelea tena hapo jana huku wapenda soka ulimwenguni wakishuhudia Vijana wa Mourinho Chelsea wakitandikwa na FC Basel palepale darajani kwa bao 2-1.
Huku nako ikishuhudiwa timu mbili zenye soka safi na la kuridhisha yaani FC Barcelona ya Uhispania na Arsenal ya Uingereza zikifanya mauaji, Barcelona wakiiadabisha Ajax ya Uholanzi nayo Arsenal ikiitandika Marseille ya Ufaransa.

Oscar akishangilia goli la kwanza la Chelsea
 
Marco Streller akishangilia goli lililoizamisha Chelsea darajani


Wachezaji wa FC Basle wakishangilia ushindi dhidi ya Chelsea
 
CHELSEA 1-2 FC BASLE

Katika mpambano kati ya Chelsea waliokuwa wenyeji wa mchezo huo pale darajani mabao ya timu zote mbili yalitupiwa kambani na Oscar (44) na yale ya Basle yalitupiwa kambani na M Salah (70) na Steller (81).

Katika mtanange baina ya Arsenal na Marseille mabao yalitupiwa kambani na Walcott (64) na Ramsey (83) na la kufutia machozi lilitupiwa kambani kwa mkwaju wa penati na Jordan Ayew (90).
 
Theo Walcott Walcott akitupia kambani bao la kwanza

Walcott akishangilia
 
Ramsey akishangilia baada ya kutupia kambani bao la pili

Giroud na Ozil wakimpongeza Ramsey
 
Ozil kibaruani
 
MARSEILLE 1-2 ARSENAL

Barcelona na Ajax mabao yalitupiwa kambani na Leonel Messi (21,54 na 74) na Pique (68).

Messi akifanya mauaji


Zuia hiyooooooooooooooooooooooo
 
Messi akipiga faulo iliyoenda moja kwa zote kambani




Iniesta akifanya udambwidambwi

Messi akitoka na mpira wake baada ya kutupia kambani mabao matatu ''Hat Trick''
 
BARCELONA 4-0 AJAX

Matokeo ya mechi zote

AC Milan 2-0 Celtic
Chelsea 1-2 FC Basle
Marseille 1-2 Arsenal
Atletico Madrid 3-1 Zenit St Petersburg
Austria Vienna 0-1 Porto
Barcelona 4-0 Ajax
Napoli 2-1 Borussia Dortmund
Schalke 04 3-0 Steaua Bucharest