Mawimbi makali na hali mbaya ya hewa baharini
imetatiza juhudi za utafutaji na uokoaji wa takriban watu mia tatu baada
ya feri ya abiria kuzama katika pwani ya Korea Kusini.
Watu tisa wamethibitishwa kuaga dunia katika mkasa huo.Wengi wa abiria kwenye meli hiyo walikuwa ni wanafunzi wa shule ya upili. Takriban watu mia moja sabini wameokolewa. Kapteni wa jeshi la wanamaji la Marekani Heidi C. Agle anashiriki katika operesheni ya uokoaji.
Ameiambia BBC kuwa maandalizi yanafanywa kupeleka mtambo wa kuinua chombo hicho.
Wakati huohuo Rais Park Geun-hye, amewataka waokozi kuharakisha juhudi zao za kuwatafuta manusura wa ajali hiyo.
Rais Park -- ambaye amejionea meli hiyo mwenyewe, amesema kuwa kila dakika ni muhimu katika kuhakikisha kuwa manusura wanapatikana.
Wapiga mbizi wamekuwa wakikabiliana na mawimbi makali kujaribu kukifikia chombo hicho kilichozama hapo jana.
Duru zinasema kuwa meli hiyo ilipoteza mwelekeo huku baadhi ya familia za waathriwa zikihoji mwenendo wa nahodha wa meli.
Hata hivyo nahodha huyo Lee Joon-seok aliomba msamaha na kusema ana majuto tele na kuwa hata hajui la kusema.
Dauru zinseama kuwa miongoni mwa wliofariki ni wanafunzi wanne wenye umri wa miaka 17 na mwaliamu wao mwenye umri wa miaka 25 pamoja na mfnyakazi mmoja wa meli hiyo.
Wengine wlaiofariki bado hawajatajwa.
Takwimu za hivi karibuni zinasema kuwa wtu 475 walikuwa kwenye meli hiyo huku 287 wakiwa bado hawajapatikana.