Thursday, July 26, 2012

AZAM YATINGA FAINALI KOMBE LA KAGAME

Timu ya soka ya Azam F.C ya jijini Dar es salaam imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Kagame baada ya kuitandika AS Vita ya DRC katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa katika dimba kuu la Taifa jijini Dar es salaam.
AS Vita ndio walikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za Azam kabla ya John Bocco"Boko haram" kutupia kwa kichwa baada ya krosi maridhawa ya Erasto Nyoni. Mtanange ulikuwa mkali na wakushambuliana kwa zamu na ndipo mchezaji machachari alieingia kipindi cha pili Mrisho Halfan Ngassa alipotupia kambani bao la pili katika dakika za majeruhi na kuipeleka Azam fainali ya michuano ya Kagame.
Sasa Azam ambayo iliwaondosha mabingwa wa soka Tanzania bara Simba S.C katika mchezo wa robo fainali kwa mabao 2-1, Inabidi isubiri mshindi wa nusu fainali nyingine ambayo inaendelea hivi sasa kati ya Yanga na APR ni dakika ya 8 hakuna timu iliyoliona lango la mwenzake.

VIWANJA VITAKAVYOCHIMBIKA OLYMPIC 2012



Aquatics Centre
Olympic Park, Eneo hili linajumuisha viwanja vitakavyotumika katika mashindano ya Olympiki 2012 jijini London nchini Uingereza. Olympic Park inajumuisha Aquatics Centre,Basketball Arena,BMX Track,Copper Box,Olympic Stadium,Riverbank Arena,Velodrome na WaterPolo Arena.

OLYMPIC STADIUM

Olympic Stadium una uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000 wakiwa wamekaa. Ulikamilika Machi 2011 na mpaka sasa Mashindano 42 yameshafanyika uwanjani hapo.

AQUATICS CENTRE
Aquatics Centre
Uwanja huu wa ndani una uwezo wa kuingiza watazamaji 17,500 ambao ulimalizika kujengwa julai 2011. Michezo ni pamoja na Kuogelea,Kuzamia.

BASKETBALL ARENA



Basketball Arena una uwezo wa kuingiza watazamaji 12,000 wakiwa wamekaa na unatumika kwa michezo ya Mpira wa kikapu(Basketball) na mpira wa mikono(Handball)

COPPER BOX



Copper Box una uwezo wa kumeza watazamaji 7,000 na michezo inayohusika humo ni Mpira wa mikono(Handball) na Modern Pentathlon


WATER POLO ARENA


Water Polo Arena una pakia watazamaji 5,000 mchezo ni mmoja tu wa Water Polo


BMX TRACK


Khalen Young - LOCOG Test Events for London 2012 - BMX UCI World Cup
Khalen Young - LOCOG Test Events for London 2012 - BMX UCI World Cup

BMX Track inakusanya watazamaji 6,000 na mchezo ni wa Kukimbiza baiskeli aina ya BMX


RIVERBANK ARENA



Riverbank Arena una uwezo wa kuwakalisha chini watazamaji 16,000 na mchezo ni Mpira wa magongo(Hockey)


RICOH ARENA




Ricoh Arena ni uwanja wa Coventry City ya jijini London, uwanja una uwezo wa kukusanya watazamaji 32,609 wakiwa wameweka makalio chini, mchezo ni mpira wa miguu pekee.


VELODROME



Veldrome unaingiza watazamaji 15,000 mchezo ni Baiskeli


EARLS COURT


Earls Court wanaingia watazamaji 16,000 mchezo ni Volleyball


ETON DORNEY


The Australian Ladies & Mens Coxed Eights squad practise during rowing training at Eton Dorney on July 24, 2012 in London, England.
Eton Dorney watazamaji 20,000 wanaweza kuangalia michezo ya Rowing na Canoe sprint.


EXCEL



Excel ni uwanja wa ndani wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 10,000, michezo ni Ngumi(Boxing),Kunyanyua vitu vizito(Weightlifting),Table Tennis,Fencing,Judo,Taekwondo,wrestling(Mieleka)


GREENWHICH PARK


Katika viwanja hivi watazamaji zaidi ya 23,000 wanaweza kushuhudia mbio za farasi na michezo mingine


HADLEIGH FARM




Hadleigh farm watazamaji wapatao 20,00 wanaweza kushuhudia michezo ya baiskeli


HAMPDEN PARK


Hampden Park uwanja huu unauwezo wa kuingiza watazamaji 52,063 wakiwa wamekaa kushuhudia mchezo wa soka

VIGOGO WAGAWANA VIWANJA DAR,WALALAHOI WACHINJIWA BAHARINI

MANISPAA ya Temeke imetoa orodha ya majina ya wananchi waliopewa viwanja katika manispaa hiyo, ambayo inaonyesha kuwamo kwa vigogo wanaojumuisha mawaziri, wabunge, watendaji wakuu wa Serikali pamoja na baadhi ya watoto wa vigogo hao.Katika orodha hiyo, jumla ya watu 1,800 walipatiwa viwanja hivyo, huku majina hayo ya vigogo yakiwa ni zaidi ya 50, ambao baadhi wamejiandikisha wenyewe, wengine wake zao, ndugu na watoto wao.
Orodha ya Vigogo hao iliyobandikwa katika ofisi za manispaa ya Temeke gazeti la Mwananchi 25 Julai 2012 limeyanyaka kama ifuatavyo;

Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama; Naibu Spika, Job Ndugai; Waziri wa Mawasiliano, Sanyansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.

Kwa upande wa Makatibu Wakuu wa Wizara wapo, Dk Florence Turuka (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Ramadhan Kijjah; Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo na Dk Idris Rashid ambaye ni Gavana wa Zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Pia wamo Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa; Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleinan Kova.

Wengine ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Haruna Masebu; Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH),Marina Njelekela.

Kwa upande wa wabunge wamo Dk Augustine Mrema (Vunjo - TLP), Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe; Mbunge wa Kibaha Mjini (CCM), Sylvester Koka; Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan; Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Dk Cyril Chami na Mbunge wa Singida Kusini (CCM), Mohamed Misanga.
Wengine ni Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila; Mbunge wa Igunga (CCM), Dk Peter Kafumu na Mbunge wa Bukene (CCM), Seleman Zedi.

Wabunge wa Viti Maalumu (Chadema), Maulida Komu na Suzan Lyimo, Viti Maalumu CCM, Dk Mary Mwanjelwa na Zakhia Meghji ambaye ni mbunge wa kuteuliwa.

Orodha hiyo pia inaonyesha majina ya ukoo yanayofanana na majina ya baadhi ya viongozi ambao ni Miraji Kikwete, Khalfan Kikwete, Juanita Mramba, Suzan Mkapa, Zainab Mkomwa, George Rupia, Maimuna Mfutakamba, Mary Membe, Pharles Ngeleja, Judith Kahama na Wilfred Mwanri.

Mkurugenzi apepesa macho na kung'ata maneno ashindwa kutoa maelezo yaliyonyooka
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Magreth Nyalile alipoulizwa kuhusu orodha hiyo alisema kuwa, majina hayo hajayaona na kwamba waliobandika wamefanya uamuzi huo bila ya yeye kuupitia.

Majina yenyewe sijayaona, hivyo basi siwezi kujua ni kina nani waliopewa viwanja hivyo, kwa sababu wako zaidi ya 1,000, jambo ambalo litakuwa vigumu kwangu kubaini tatizo hilo,” alisema Nyalile.

Aliongeza kuwa, kutokana na hali hiyo hawezi kusema lolote kwa sababu yuko nje ya ofisi kwa ajili ya shughuli nyingine za ujenzi wa taifa.

Hata hivyo, Nyalile alisema mchakato wa ugawaji wa viwanja hivyo ulifuata taratibu za kisheria na kwamba hakuna mtu au kiongozi yeyote aliyependelewa, jambo ambalo linaweza kusababisha mgongano wa hapa na pale.

Nyalile alisema kuwa kama kuna viongozi walipewa kwa njia zisizo sahihi, au kwa rushwa wakati wa uwasilishaji wa majina hayo, walipaswa kutoa taarifa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.