Wednesday, June 24, 2015

TAZAMA GOMA JIPYA LA CHAMELEONE-BWERERE


LIVERPOOL YANASA SAINI YA MBRAZIL FIRMINO


Firmino akiwa katika uzi wa Brazil


Firmino akiwa na uzi wa Hoffenheim

Klabu ya Liverpool imefanikiwa kumnasa Mbrazil Firmino aliekuwa akikipiga nchini Ujerumani na klabu ya Hoffenheim na kumsainisha mkataba wa ''Nyundo'' tano unaogharimu paundi za Uingereza Milioni 29 kuitumikia Liverpool.
Mkataba huo utakamilika sambamba na ukaguzi wa matibabu baada ya Firmino kurudi toka Chile ambako anaitumikia timu yake ya taifa ya Brazil katika michuano ya Copa Amerika.

Firmino akiwa ametikisa nyavu mara 47 katika mechi 151 alizokipiga na klabu ya Hoffenheim katika ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani anakuwa mchezaji wa pili ghali katika klabu ya Liverpool baada ya Andy Caroll kunyakuliwa kwa kitita cha paundi za Uingereza milioni 35 mwaka 2011 akitokea Newcastle United.