Tuesday, August 2, 2011

KONA YA WATU MAARUFU

Rihhana ndani ya bikini na kofia ya asili alipokuwa kijijini kwao nchini Barbados alipozaliwa katika kuazimisha siku maarufu nchini humo ijulikanayo kama Kadoomant Day Parade.J Lo akiwa katika maisha mapya ya u-single,hapa akiwa amembeba mwanae Emma mwenye miaka 3 na Max hayupo pichani wakiwa katika hifadhi moja ya Atlanta jumapili iliyopita alipokuwa akichukua picha za filamu yake mpya "WHAT TO EXPECT WHEN YOU'RE EXPECTING"Jennifer Antison na Beau Justin wakiwa katika mitaa ya Hawaii jumapili iliyopita.Mjamzito Jessica Alba akiwa katika onesho la filamu mpya jijini Los Angeles siku ya jumapili.Anna Kendrick akifurahia keki aliyoandaliwa wakati wa siku yake ya kuzaliwa,Hafla hiyo ilifanyika ndani ya klabu ya usiku ya Vanity iliyopo katika Hoteli ya Rock Hotel & Casino jijini Las Vegas, Kendrick alitimiza miaka 26.Angelina Jolie na Bradd Pitt wakiwapungia mikono mashabiki wao jijini London walipokuwa wakielekea kwenye tamasha la filamu la Sarajevo.


WENGER AMUWANIA MIYAICHI

Ryo Miyaichi
Arsene Wenger has dropped his biggest hint yet that Japanese youngster Ryo Miyaichi could be involved in Arsenal's first-team this season.
The Gunners swooped for the 18-year-old in January, although he was almost immediately loaned to Feyenoord where he spent the second half of the campaign while he awaited the clearance needed to play for the Emirates Stadium outfit.
It had been thought the starlet may return to Holland again this season to continue his education, however, Wenger wants him to stay at Arsenal.
The vastly-experienced French tactician is hoping Miyaichi, who is yet to win a full cap for his country, will be able to obtain a work permit.
"My plan is to get a work permit for him and to put him on the pitch for Arsenal," he told the club's official website.

"MAITI" YAAMKA AFRIKA YA KUSINI, APIGA YOWE NA KUWATISHA WAHUDUMU

Raia mmoja wa Afrika Kusini aliamka akajikuta yupo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti mwishoni mwa juma, na akaanza kupiga kelele akitaka atolewe- akiwatisha wahudumu wakidhani ni mzimu.

Jeneza
Familia yake ilidhani amekufa baada ya kushindwa kumwamsha Jumamosi usiku na kuwasiliana na ofisi moja yenye vyumba vya kuhifadhia maiti ya mtu binafsi katika kijiji kimoja mjini Eastern Cape.

Alikuwepo kwenye chumba hicho kwa muda wa saa 24, msemaji wa idara ya afya mjini humo aliliambia shirika la habari la Sapa.

Wahudumu hao baadae walirejea na kupiga simu kuita gari la wagonjwa.

Mtu huyo ambaye jina lake limehifadhiwa, alitibiwa hospitalini kwa kukosa maji mwilini.

Msemaji wa idara ya afya ya Eastern Cape Sizwe Kupelo alisema, "Daktari walimfanyia uchunguzi na kuona kuwa anaendelea uzuri."

"Hakuhitaji matibabu ya ziada."

Bw Kupelo alisema mtu huyo aliamka saa tisa za Afrika Mashariki siku ya Jumapili, akitaka kutolewa kwenye chumba hicho chenye baridi kali kwenye kijiji cha Libode, na kuwatisha wahudumu waliokuwa zamu.

Bw Kupelo alisema, "Mwanzo watu hao walikimbia kwa kasi."

Maafisa wameusihi umma kuwasiliana na madaktari au wanaotoa huduma za dharura ili waweze kumtangaza mtu kufariki dunia kabla ya kuwaita wahudumu wa vyumba vya kuhifadhi maiti.

Bw Kupelo alisema, "Unaanza kujiuliza ni watu wengine wangapi waliokufa kwa namna hiyo katika chumba cha kuhifadhia maiti."

VALENCIA ASAINI MKATABA MPYA MAN UNITED

Mchezaji wa pembeni wa Manchester United, Antonio Valencia amesaini mkataba mpya wa miaka minne ambao utamuweka Old Trafford hadi msimu wa mwaka 2015.

Antonio Valencia
Valencia mwenye umri wa miaka 25 amefunga mabao 10 katika mechi 69 tangu alipojiunga na Manchester United akitokea Wigan Athletic mwaka 2009.
Ameeleza katika mtandao wa klabu hiyo: "Ninafuraha sana kubakia Manchester United. Natumai nitaendelea kukuza kipaji changu.
Mshambuliaji huyo wa pembeni raia wa Ecuador msimu uliopita alianza kucheza mechi nane tu baada ya kuvunjika kifundo cha mguu na hakuweza kuwemo katika kikosi cha timu yake kilichozuru Marekani hivi karibuni baada ya kuumia kifundo cha mguu.
Lakini meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson amefurahi kuweza kumbakisha Valencia kwa miaka minne ijayo.
"Antonio ametoa mchango mzuri sana tangu alipowasili katika klabu hii. Kasi yake, uwezo wa kuchonga krosi na wepesi wake vimekuwa ni vitu vya thamani kubwa kwetu," alisema Ferguson.

WILSHERE KUIKOSA MECHI YA ENGLAND DHIDI YA UHOLANZI, THIERRY HENRY AKATALIWA KUICHEZEA ARSENAL.

Jack Wilshere inaonekana atakosa mechi ya kirafiki kati ya England na Uholanzi tarehe 10 mwezi wa Agosti, baada ya kuumia kifundo cha mguu wakati Arsenal ilipocheza mchezo wa kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu.

Jack Wilshere
Meneja wa Arsena, Arsene Wenger alilazimika kumtoa kiungo huyo kama tahadhari siku ya Jumapili walipocheza na New York Red Bulls kuwania Kombe la Emirates.
Wenger alisema hakuumia sana ila kifundo cha mguu wake kilivimba.
"Iwapo hataweza kucheza wiki ijayo, basi hataweza kucheza mechi dhidi ya Benfica, kwa hiyo kwa vyovyote hataichezea England," alisema Wenger.
Timu ya utabibu ya Gunners imetabiri hataweza kucheza kwa muda wa wiki moja, lakini Wenger amesema bado kuna nafasi anaweza kupona haraka na kucheza siku ya Jumamosi katika mechi ya mwisho ya maandalizi ya Ligi dhidi ya Benfica.
"Wameniambia huenda wiki ijayo atakuwa sawaswa," alisema. "Lakini kwa kawaida yeye huwa anapona haraka, ni kijana mkakamavu, kwa hiyo ninatumaini atapona haraka tofauti na madaktari walivyotabiri."
Meneja wa England Fabio Capello tayari atawakosa Steven Gerrard na Theo Walcott kwa ajili ya mchezo huo wa kimataifa kwenye uwanja wa Wembley.
Wakati huo huo mshambuliaji wa New York, Thierry Henry alikataliwa kuichezea Arsenal dakika tano za mwisho katika mechi hiyo ya Jumapili.
Alikubaliana na Wenger kwamba atabadilisha timu dakika tano kabla ya kumalizika mchezo huo wa kirafiki.
Lakini mwamuzi Kevin Friend alikataa kuruhusu hilo kwani kanuni za Fifa zinaeleza kwamba mchezaji haweza kuchezea timu zote mbili katika mchezo mmoja.